SOMO; NYOTA YAKO NI UTAMBULISHO WAKO KIROHO NA KIMWILI

SOMO:NYOTA NI UTAMBULISHO WAKO KIROHO NA KIMWILI.

UTANGULIZI.
Tunajifunza Biblia Leo Tunaona Watu waliotambulishwa kwa nyota zao Yesu Wakuu wa nchi walimtambua na Wasomi mbalimbali. MUSA ni watu waliotambulishwa kuwa wananyota ya uongozi Mungu akaona anakitu. Kutoka sura 3; Tunaona Haruni naye anatambulishwa Ananyota ya uongeaji kwa hiyo Mungu akaamua ampe Musa Haruni kutokana Haruni alikuwa ananguvu ya ushawishi lakini hana uongozi ndani yake Kama Musa na Yoshua. Lakini Tunaona watu wengi kama Daniel Yusufu Kina Daudi Sara Hanna Kina Mariamu Biblia inawatambua kama watu waliokuwa na nyota Ambao Mbingu ziliwatambua ndiyo maana wakaitwa wanawake bora kuliko wote. Na wakapata upendeleo kwa Mungu kutokana na nyota.
Soma. MATHAYO;1;18-24
Mathayo 1:23
[23]Tazama, bikira atachukua mimba, 
Naye atazaa mwana; 
Nao watamwita jina lake Imanueli; 
Yaani, Mungu pamoja nasi. 


NAITWA PASTOR RICHARD 
NIPO MOROGORO VETA DAKAWA 
WHATSAPP +255759861768 

A:MAANA YA NYOTA. 

Nyota ni Utambulisho kwa watu au Jamii Kitu Kinachokutambulisha Kwa haraka ni nyota.

UDHIBITISHO UPO KWA YESU MWENYEWE 
MUSA, DAUDI, YUSUF NA MARIAM ,RUTH,DORICAS, RAHABU, ESTHER Na wengine wengi walitambuliwa kwa kile walichofanya na wakainuliwa Kimaisha.


KUMBE UKIJIONA HUNA KITU KINACHOKUELEZEA KWA HARAKA KWA MTU AU WATU AU KUNDI LA WATU. Ujue huna utambulisho kama huna utambulisho itakulazimu utoe maelezo mengi KAMA KAINI  AU ESAU Kwa Sababu ya Kutokuwa na Nyota au kuitambua walichonacho waliteseka Sana Soma Habari ya Kaini.
Mwanzo: 4 sura yote Tunaona Penina Naye alikuwa hana nyota ya kupendwa Soma 1Samweli;1 Sura yote. Hanna alipendwa Na mchungaji wake na mume wake kwa sababu ya utambulisho wake Kama Mke Anayefaa.

B:NYOTA HUSABABISHA MAADUI WAKUTAFUTE KWA SABABU YA NYOTA.

Kuna watu Kwenye Biblia walitaka kufa na kuuawa kutokana Na NYOTA ZAO KUWA HATARI.

1;DANIEL 
Dario aliandaa mpango ahakikishe Daniel anakufa kwa hiyo alichokifanya alimtupa Kwenyr Tundu la Simba ili wale simba wale nyama. Yote kwa Sababu ya nyota yake.
Soma habari hii Daniel sura ya 6 Yote.

Lakini Kwa Kuwa Daniel nyota yake Mungu alitaka ig,are Zaidi Alizidi kumtambulisha kwa Dario.

2.YESU MWANA WA MUNGU. 

Yesu alipozaliwa tu Herode aliona nyota ya utawala ndani ya mtoto Yesu Mfalme akahofia atabinduliwa akatengenza Njamaa Amue Yesu are na nyota Yake.
Soma Mathayo 2:7
[7]Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota. 

3:ELIA NABII WA BWANA
Nabii Elia nyota yake ilizidi kug,aa alipowauwa manabii 450 wanaotokana na Baali yaani Waganga wachawi Na mapepo ya utambuzi Mchawi mmoja Yezebeli Aliyekuwa mwenyekiti wa hao Akataka Kumua Elia.
SOMA 1WAFALME sura ya 19 yote.

4:SAMSON MWENYE NGUVU 

Samsoni anataka kuuliwa kwa sababu ya nyota yake kwa aliyokuwa anayafanya 
Soma Waamuzi sura yote ya 16


Hizi ni Baadhi Ya Udhibitisho kuwa nyota hutafutwa na maadui hasa wakijua Unanyota inayowafaa wao mfano nyota ya wateja nyota ya pesa nyota ya uchumi nyota ya huduma wataanza kutumia njia waibe nyota yako.




C:NYOTA HUFATWA NA WATU.

Acha nikuambie Hufatwi au hupendwi hakuna anayekufata hata kusema anakupenda hii ni hatari maana huna nyota wewe.

1:DELILA ALIMFATA SAMSONI KWA SABABU YA NYOTA YAKE.

Kuna watu wengi nimekutana nao katika kuwafanyia ukombozi roho za wachumba wao au ndugu za waliongea huyu ananyota kali sana hatutaki aolewe au aowe 
Wapo watu hawaolewi kwa sababu ulimwengu wa roho unawapa kinadelila wanaofata nyota zao tu. Soma Waamuzi sura ya 16




2:NYOTA HUSABABISHA MTU AKUFATE AKUPOSE NA UOLEWE.

Yosefu Mume wa Mariamu mama yake na Yesu Alikuwa Amempenda mariamu kwa sababu aliona anakitu cha tofauti kuliko wanawake wengine Yaani nyota inakutofautisha kati ya huyu na huyu.
Soma Mathayo Sura ya 2:

3:NYOTA HUFURAHIWA NA KUKUTANISHA NA CONNECTION MBALIMBALI. 

Huwezi ukapata kusaindiwa au ukafurahiwa na mtu kama huna nyota watu watakufurahia na kukupenda kwa kile ulichonacho nyota yako.
Mathayo 2:10
[10]Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno. 

 Yusufu alitambulika kutokana na nyota yake
Mwanzo 39:2
[2]BWANA akawa pamoja na Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri. 


D:MAMBO YANAYOUWA NYOTA YAKO NDANI YAKO:
Huwa Kuna Vitu Unatakiwa uvijuwe ili kuepuka nyota yako isiibiwe au kuharibiwa na Adui Herode.

1;LANGO LINALOONDOWA NYOTA  MAFANIKIO, UPAKO, HUDUMA, UCHUMI NA NDOA.
Ni wewe unapozini yaani kufanya tendo la ndoa na mtu ambaye hajakutolea mahari au hujamtolea mahari. MTU AMBAYE HATAMBULIKI.

Soma Mathayo:5:27

2:LANGO LA KUPOKEA VITU KUTOKA KWA WATU  USIOWAJUA.
Kuna watu wanapenda Sana Kupokea vitu na kuvaliana nguo kitu ambacho hufugua mlango wa adui kuiba nyota au kuiharibu.
SOMA HIKI KITABU.1samweli:12:4-7

3:LANGO LA KWENDA KWA WAGANGA.
Kuna watu nyota zao ziliharibiwa au kuibiwa kupitia kwenda kwa waganga wakienyeji
Wakapeleka Vitu kama nguo za ndani Pesa Mifungo nk

Hawakujua wanajiangamiza wao kama wao.
Soma huu mstari.
Isaya 44:25
[25]Nizitanguaye ishara za waongo, na kuwatia waganga wazimu; niwarudishaye nyuma wenye hekima, na kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga; 


E.DALILI ZA NYOTA ILIYOIBIWA

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.