SOMO:NGUVU YA MAOMBI YA KUOMBA KATIKA ROHO MTAKATIFU
SOMO; NGUVU YA KUOMBA KATIKA ROHO MTAKATIFU.
Vitabu: rejea Warumi:8:26 Waefeso.6:18
Kuna Watu Wanaweza Wakawa Wameelewa Namanisha Nini KUOMBA KATIKA ROHO Lakini Wegine Wanaona Kichwa cha Somo tu na hata hawaelewi hata hawajawahi Kuhisi nguvu na mtetemeko WA Roho Wakiwa Katika Kuomba.
KWANZA UJUE ROHO MTAKATIFU NI MUNGU MWENYEWE ndiye Anayekufundisha Kuomba na Kukuongoza Katika Wokovu wako.
Leo Tunataka Tujue Ili Mungu Tuweze Kumfikia Lazima Tujue hili.
Kuomba katika Roho Mtakatifu ni Nini?
Nikuomba Maombi Yenye hisia za Kumfikia Mungu na Kuwa Connect naye mfano nichukue mauganisho ya umeme yanavyoleta nguvu ya UMEME KUTOKEA Mwanga Ambayo huuganishwa.
Nawewe Maombi Yako Ili Yawe Connect Lazima Ujue Kujiugamanisha na Unakiomba.
AINA TOFAUTI ZA MAOMBI YA KUMFIKIA MUNGU AOMBAYO MWANADAMU.
Watu Wamekuwa na Aina tofauti tofauti za maombi ambayo Yanatusaindia Tumfikie Mungu Kutokana ROHO MTAKATIFU kuwafunulia kwa karama zao mbalimbali za uombaji.
1:MAOMBI YA KUTAFAKARI.
Haya ni Aina ya Maombi yanayomwelezea anayeomba masikitiko yake katika maisha yake Anaomba Anajiona Kama Mungu wake amemuacha kama nikanisa linaeleza masikitiko yake na hudhuni kwa Waumini wanayopitia.
MAOMBI Haya siyo Maombi lakini Unatakiwa uzame katika Roho usiende mbele za Bwana asikilize machozi yasiyomanisha moyoni Mungu hatajibu.
2:MAOMBI YA VITABUNI.
Haya ni Maombi Yaliyoandikwa Kwenye Vitabu Vya Watumishi mbalimbali kwa lengo la Kumfanya Mtu aombe na Aweze Kumfikia Mungu Wake Kupitia Kitabu cha Maombi.
Wengi hapa Husoma Juu Juu na Maombi ya Kitabuni watu hawaombi Kwa hisia za Kumfikia Mungu Na Wengi hawafati kama mwandishi wa kitabu alivyofunuliwa maombi hayo uombaje.
Mfano Umeambiwa omba rudia mara mbili maombi haya msomaji akija kuomba harudii.
Hii Hufanya roho asiweze kukuhudumia na kubemba unachoomba sababu Aliyeandika kitabu hicho alivuviwa kuandika kitabu cha maombi Kikupe msaada wa kumfikia Mungu.
3: MAOMBI YALIYOELEKEZWA.
Haya ni maombi unayoomba mtu anakuelekeza wewe unarudia
Kuna watu wengi wamekuwa wakitusaindia Kadiri Roho Mtakatifu anavyowaongoza wamekuwa wakitupa namna na mbinu mbalimbali Tunavyopaswa kuomba kwa Usahihi . Wapo wegine Wamekuwa wakituongoza Kuomba Nasi Tunaomba hali inayotufanya Tumfikie Roho Mtakatifu kwa haraka.
4:MAOMBI YA ORODHA.
Haya ni Maombi yaliyo katika orodha ya kichwa chako yanayokusumbua unayaandika nakuanza kuyaombea mwenyewe au unampa mtu akuombee hii ni njia moja wapo ya Kumfikia Mungu katika Maombi.
MAOMBI MABAYA YASIYOMFIKIA MUNGU.
(Yakobo;4:2-3)
Kuna maombi Tunayoomba yanakuwa hayamfikii Mungu kwa kuwa hatujui nasi Tunakazana Kumuomba Mungu Bila matokeo.
Maombi hayo ni Yapi ni haya.
1. KUOMBA KWA TAMAA.
(2 Tim.2:22)
Hii ni Hali ya mtu anamuomba Mungu kile kitu amekitamani
Mfano mtu ameolewa nawe unatamani uolewe unaingia maombi wakati huo ulikuwa huna mpago wa kuolewa au amenunua gari unatamani unaanza Kusema Mungu nipe" gari kama Richard "
Maombi hayo mabaya yaache.
2:KUOMBA VIBAYA.
Hii ni mtu Anaomba maombi yake vibaya pasipo kuzingatia heshima na mtiririko mzuri wa maneno . Mtu anaomba kwa huku Amebemba manug,uniko Anaomba huku Amebemba moyo wa Kisasi Anaomba Pasipo Kujishusha Kwa Mungu au mtu anaomba huku amekata tamaa
Hali hii wengi huwakosesha wasimfikie Roho Mtakatifu. Acha maombi ya hivi huzui usipokee kwa Mungu.
Zaburi:106:15
3;MAOMBI YA NIA MBAYA.
Haya ni Maombi Mtu anaomba akiwa ananiambaya moyoni na mwingine Anamawazo mabaya
Mawazo mabaya na Nia mbaya huondoa kabisa ndani yako nguvu Roho Mtakatifu na hata ukija kuomba unaomba ukiwa huna Roho Mtakatifu.
TUFANYE NINI.
Tunapaswa kuhakikisha Tunapoomba Tunaondoa Kila Kinachotuzuia Tusikutane na Mungu mifano Tamaa nia mbaya mawazo mabaya na kukata tamaa.
Tukifanya hivyo Tutakuwa Tunaomba Maombi yanayomgusa Mungu.
TUSIISHIE KUOMBA VIBAYA KAMA HILI ANDIKO Linavyotuonya👉👉Yakobo 4:2-3
[2]Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!
[3]Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.
HITIMISHO
Ninamshukuru Roho Mtakatifu kuniwezesha Kuandaa na Kuwasilisha Somo hili na Kitabu cha fimbo ya mchungaji kilichosaindia kunipa Mwanga Wa Somo hili.
WITO
Tumeitwa Kutumika wagapi uliowaleta kwa Yesu mpaka Sasa Basi share zaidi Somo hili
Kama unataka kuugwa kwenye group
La Maombi Mwambie Pastor Richard akuuge Tuma Jina na mahali ulipo kwenye inbox yake +255759861768
@2023
Pastor Richard
Maoni
Chapisha Maoni