SOMO:MAOMBI YA UKOMBOZI WA NYOTA
SOMO ;MAOMBI YA UKOMBOZI WA NYOTA YAKO
UTANGULIZI :
Karibu Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa Tulia usome kisha tuombe wote tukomboe nyota zetu.
Fatana nami katika Somo hili Ujifunze uelewe nyota kibiblia. Kila mtu huwa amezaliwa na nyota yake kabisa isipokuwa katika kuishi watu wengi hujichanganya kwenda kwa waganga na kuanza kushiriki vitu vya kiganga au kuchanjwa chali kama watoto hawakufanya wazazi inawezekana walienda kwa waganga.
NYOTA; huchukuliwa katika mazingira yafatayo
-Kwenda kwa waganga
-Kuishi maisha yakuzini unatubu unaridia kuzini
-Dhambi ya uasi huharibu haraka nyota yako
.UDHIBITISHO WA DHAMBI
Mwanzo 3:9
[9]BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?
Dhambi ilisababisha uhusiano wa Adamu na Mungu kutoweka kuna kitu ndani ya Adamu kiliondoka. Nyota ya kuonekana ikapotea ndiyo maana Mungu anauliza upo wapi Adamu.
MAANA YA NYOTA;
NYOTA: Ni utambulisho wa wewe ni nani katika maisha haya hatima yako ni ipi Kusundi lako ni nini kuwepo ..?
UDHIBITISHO WA ANDIKO;
Mathayo 2:2
[2]Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.
Yesu alipozaliwa watu walianza kumjua na Kumtambua ni mfalme kupitia nyota iliyomo ndani yake. Kuna utofauti mkubwa kuzaliwa kwa Yohana mbatizaji na Yesu.
Kumbe Tunajifunza Nini Adui hushughulika kuiwinda nyota yako ilimo ndani yako Apate kuiuwa isiwemo ndani yako mfano.
πKuuwa malengo yako
πKuuwa hatima yako
πKuuwa Kusundi lako na Mungu.
UDHIBITISHO WA HILI KWAMBA ADUI HUDILI NYOTA YAKO
Mathayo;2;7
[7]Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota.
Adui Anapoona wewe unanyota ya mafanikio nyota kazi nyota ya ubunifu ataanza kukuwinda ili ahakikishe wewe hufanikiwi wewe hufikii hatua uliyokusundia ufike.
Mfano huyu mfalme Herode alitaka kuuwa malengo na kusundi la mtoto Yesu.
TUNAITAJI WAZAZI WA KIROHO WATAKAOTUKIMBIZA ADUI ASISHIKE NYOTA YETU.
Wazazi ni mhimu kwa maisha yako ya kiroho Tunaona Yusufu na mariamu kwa mtoto Yesu.
Mathayo 2:14-15
[14]Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri;
[15]akakaa huko hata alipokufa Herode; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema,
Kutoka Misri nalimwita mwanangu.
KAZI YA NYOTA NDANI YETU;
1:Nyota huleta Kibali.
Watu waliokosa kibali wapo wapo ni dhahiri nyota yao haionekani
TUSOMEπππππ
1samweli:2:26
2;NYOTA Hukupa Kazi.
Ukiwa na nyota kazi zitakufata mwenyewe kila unalofanya litaenda
Maoni
Chapisha Maoni