SOMO: USHUHUDA WA KUJUA UNAEMTOLEA SADAKA KIBIBLIA

SOMO: USHUHUDA WA KUJUA UNAEMTOLEA SADAKA KIBIBLIA.

Karibu ujifunze kitu somo hili

Unapotoa sadaka hakikisha unajua unaemtolea ni Mungu wako aliye hai siyo mtu au mchungaji  toa Sadaka kwa imani 

Naitwa Pastor Richard 
Nipo Morogoro Veta Dakawa 
WhatsApp yangu +255759861768
Nifate nikuuge kwa group la maombi na mafundisho 

1:KONELIO BIBLIA INASEMA ALITOA SADAKA KUWAPA WATUMISHI WA BWANA NA WATU 👇👇👇👇
Soma kitabu; Matendo;10;1-33

Lakini kilichokuwa cha ajabu malaika alishuka na kumwambia Sadaka zako zimefika mbiguni Mungu Ameona Moyo wako. Unajiuliza Sadaka kawapa Watu Mbigu zinafugukaje Wakati anawapa watu.

Jibu. KONELIO Alijua Mungu anayemtolea Sadaka Alijua Siwapi watu mimi namgusa Mungu moja kwa moja. Haleluyaaa hebu jaribu nawewr mbigu kuzifungua kwa utoaji.

Jifunze hili kwa Konelio



2:HABELI BIBLIA INASEMA ALITOA SADAKA KWA IMANI BILA KUSITA SITA TENA NZURI.
👇👇👇👇👇
MWANZO; 4;1-10

Jifunze unapotoa Sadaka yako hebu uwe na imani Usitoe Sadaka huku huna imani na yule unayempa Sadaka Yako Kana Kwamba Ni Binadamu Unampa Kumbe ni Mungu

Hebu jifunze Kwa Habeli alichukua wazawa wa mifungo wale wakubwa wazuri akampa Bwana Na Mungu alipokea Sadaka Zake.

Acha mashaka na kutoa Sadaka ukiwa na wasiwasi toa kwa Mungu ukiwa na imani kama huna imani acha usitoe.


3:Doricas ALITOA SADAKA ZA KUWAVISHA TU WACHUNGAJI  NA WATU.
👇👇👇👇
Matendo:9:36-40

Tunajifunza Kumbe Sadaka Siyo mpaka Pesa hata nguo mnunulie mtumishi na mvishe hakikisha Anapendeza Unapofanya hivyo kwake. Yaani Anaposema tu Ansate mbigu zinafunguka

Toa Sadaka chochote ulichonacho.


4:HANA ALIKUWA KILA AKIOMBA MAOMBI YAKE ANAYATOLEA SADAKA. 
👇👇👇👇👇👇
1.SAMWELI.1 Soma yote habari hii.

Jifunze Maombi yako unapoomba Ambatanisha Sadaka mpe Baba yako wa kiroho au mchungaji Hiyo Sadaka itakuwa na nguvu kulifungua tumbo lisilo zaa au yaliyokufunga 

Jiulize hana Kupitia kuwa anatoa Sadaka kila anapoenda kuombea hitaji lake Mungu alijifunua akamjibu.

Lakini Sadaka alikuwa akimpa mchungaji Eli Ambaye alikuwa akimuongoza Maombi kipindi hicho lakini majibu aliyekuja kujibu ni Mungu. 


HITIMISHO 

Inawezekana Unatoaga Sadaka haya huyajui na unatoa tu kama mkumbo unatoa pasipo na imani unatoa unaona unampa mchungaji 

Badilika Ujue Mungu uliyenaye Anaguswa na Sadaka 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.