SOMO: NAMNA YA KUTOA SADAKA YA KUJENGA MADHABAHU

SOMO👉👈: NAMNA YA KUTOA SADAKA YA KUJENGA MADHABAHU YA BWANA  NDANI YAKO.

Naitwa Pastor Richard 
Nakuletea Somo hili ujifunze kitu
Nipo Morogoro Veta Dakawa 

Madhabahu ni mahari patakatifu panapo mfanya roho wa Mungu akae aanze kuhudumia watu kuwafugua na kuwaponya.

MADHABAHU ni mahusiano yako ndani Kati Yako Na Mungu. Haya Mahusiano Yako na Mungu ndiyo Yanayokufanya uombe uone matokeo ya ulichoomba. Pia ndiyo yanayokufanya wewe uombe usione matokeo Kama unaenda Kuomba huna mahusiano na Mungu.

NDIYO  sababu inayowafanya watu Waende kuombewa na mwigine waone matokeo kwa sababu wao hawana madhabahu ya Bwana Hawana uhusiano na Mungu.

KUNA AINA MBILI ZA MADHABAHU 

1:MADHABAHU ZA miungu.
Ambayo ni uchawi,uganga,mizimu nk

Tusome hapa
👇👇👇
Kutoka 34:13
[13]Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao,

Kumbe Basi Kama unataka Kujenga madhabahu Ya KIMUNGU ndani Yako

Lazima uziondoe Tabia zinazofanya uharibu uhusiano wako na Mungu 
1:Kuabudu miungu 
Kwenda kwa waganga,Kutabika,Uchawi,nk

2:Kuziondoa Tabia za Awali.
Kuzini,Kunywa pombe, Kwenda Disko, Kukata tamaa ,Kunug,unika, kuacha wokovu, Dhambi za kujirudia .Acha wizi wa zaka nk

Haya yatakufanya ubomoe ndani yako uhusiano wako na Mungu utajikuta huna madhabahu iletayo majibu ndani yako


2:MADHABAHU YA BWANA.

Hii ndiyo madhabahu ya Mungu inayoleta matokeo ya unachoomba au kuombewa 

Unakuta mtu madhabahu fulani imeniponya inamaana yake ilishindwa haina nguvu ya kuleta matokeo ni lazima nawewe ujenge madhabahu yako. Yaani uhusiano wako na Mungu.

Tusome
👇👇👇👇
Mwanzo 12:7
[7]BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu BWANA aliyemtokea. 

Ibrahimu Alitengeneza uhusiano  wake na Mungu vyema ndiyo maana Mungu alimtokea.
Alibarikiwa kutokana na Kujenga Madhabahu. 


SHUHUDA ZA WATU KWENYE BIBLIA WALIMUONA MUNGU KUPITIA KUJENGA MADHABAHU YA BWANA NDANI YAO.

Katika watu hawa tunaoenda kuwaona nakuwasoma kwenye Biblia walimuona Mungu akijidhihirisha kwenye maisha yao
Nitawataja baadhi.

1:NUHU: ALIPOTAKA KULINDA UHUSIANO WAKE NA MUNGU

; gharika lilipowapata watu wakafa na maji lakini Nuhu peke yake alionekana Yupo mwenye haki mbele za Bwana.
Kwa Lugha newesi Tunaona alikuwa na mahusiano mazuri kati yake Na Mungu.

Na Biblia inasema Alimjengea Madhabahu Bwana hii ndiyo iliyosababisha Mungu Amuone.

Nuhu alimtolea Mungu Sadaka ya Kujenga madhabahu kuimarisha uhusiano waoo
👇👇👇
Mwanzo 8:20
[20]Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. 


2;ELIYA: ALIPOTAKA KUUSHINDA UFALME WA NGIZA

Ni Nabii Eliya Pekee Biblia inasema Baada ya Kitendo cha Kujenga madhabahu kisha akatoa Sadaka ya Madhabahu Aliomba Moto ukashuka ukateketeza na kuyalaba maji mapipa manne
Bila kufanya kitendo hiki cha kujenga madhabahu Nabii Eliya asingeushusha moto maana mahusiano yake na Mungu yalikuwa yamevunjika kwa kumkibia Yezebeli na wachawi wezake wa eneo Bwana ndipo alipo mtuma kunguru na Malaika kumwambia arudi huko katika ufalme wa Ahabu.

Eliya hatua ya kwanza kabisa aliamua ajenge  madhabahu iliyovunjika.
👇👇👇👇👇👇👇
1 Wafalme 18:32
[32]Naye akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la BWANA; akafanya mfereji, kama wa vipimo viwili vya mbegu, ukiizunguka madhabahu. 

Mungu Anataka ili akujibu kama Elia Jenga madhabahu na utoe Sadaka katika hiyo madhabahu ulioijenga.


3:IBRAHIMU:  ALIPOTAKA KUBARIKIWA

alienda yeye na Isaka mwanae Mpaka pale alipowataka Mungu atamjegea Madhabahu hapo ndipo alitoa  Sadaka ya Kujenga Madhabahu. Kupitia tendo hilo Ibrahimu aliinuliwa Kiuchumi na hata uzao wake ulizidishwa kama mchanga wa baharini

Tusome hapa unaweza Soma sura yote
👇👇👇👇
Mwanzo 22:9
[9]Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni. 


4:YOSHUA: ALIPOTAKA KUWEKA ANGANO LA UTUMISHI WAKE NA MUNGU. 

Alijenga madhabahu ya Bwana Hii ilimsaindia Yoshua kuweza kushinda kila vita alizokutana nazo. Ili Mungu atembee nawewe vyema akutumie katika nafasi ya Juu iwe ni huduma au kazi zako mjegee Bwana Madhabahu. 

Tusome
👇👇👇👇
Yoshua 8:30
[30]Ndipo Yoshua alijenga madhabahu kwa BWANA, Mungu wa Israeli katika mlima Ebali. 


Hawa ni Baadhi tu wapo wengi mno ambao walijenga madhabahu ya Bwana.



JINSI YA KUJENGA MADHABAHU YA BWANA NDANI YAKO 
🖊🖊🖊🖊🖊🖊🖊🖊🖊🖊🖊🖊🖊🖊🖊

Baada Ya Yesu Kuja madhabahu  ilijengwa ndani Yetu Uhusiano wetu na Mungu unajengwa ndani.

Namna Unavyoweza Kujenga Sasa.
Zingatia haya kwanza

1:Anza Kujishuguhulisha unaachana na Tabia zisizompa utukufu Mungu

2:Amua mwenyewe waitaji uwe na mahusiano na Mungu. Na mwenye kujenga huo uhusiano ni wewe.

3;Kubali ulikosana na Mungu kisha tubu.


JINSI YA KUITOA SADAKA HII.

Utafanya Jambo litakaloacha alama kanisani utajitoa kitu kitakachohubiri injili ya Bwana.

Kama vile Sadaka  za Kujenga Madhabahu 

1:Utajenga Kanisa peke yako.
2:utatoa bati Siment na Vifaa vya ujenzi.

2:Utanunu vyombo vya mziki

3:Utanunua viti,meza na vyombo vitakavyotumiwa kanisani au kwa mchungaji.

4:Utanunua Usafiri Utautoa uwe wa kanisa.

5; Utanunua Simu zenye uwezo, laptop, printing, nk utatoa kwa ajili ya kanisa.


6;Utatoa ng,ombe dume, Kondoo ,mbuzi, kuku watakauzwa kinunuliwe kitu kihubiri injili ya Bwana.


SADAKA YA MADHABAHU HAINA KIWANGO LAKINI INALENGA UNUNUE VITU VITAKAVYOHUBIRI INJILI YA BWANA HATA WEWE USIPOKUWEPO.


Kwa wezetu Wa Angano la Kale walikuwa wanajenga hadi makanisa kama Sulemani hata sisi tunaweza kujenga madhabahu ili Kufanya Tusiwe watu wa kuhagaika mpaka kwenda madhabahu ya mtu mwigine majibu yako uyapate.

Hii itakufanya utaomba majibu utayapokea wewe hutahagaika mpaka kwenda kwa Musa wakati wewe ni Yoshua Kwenda Kwa eliya wakati wewe ni Elisha.


KABLA SADAKA HII HUJAITOA  

Unatakiwa Unanieleza nataka nijenge madhabahu nitoe Sadaka ya kujenga madhabahu hii ni Sadaka ya kipekee Sana.

Namimi ndiyo nitakuongoza jinsi ya Sadaka hiyo kuiombea na maombi nitakutumia na muda wa kuomba. 

Hakikisha Umeamua kujenga uhusiano na Mungu dhibiti tabia zote zinazokutenga na Mungu.

Madhabahu hii inaitwa madhabahu ya Moto wa Yesu ipo chini Ya Pastor Richard (Bishop Richard)

Kama hujanielewa Basi uliza niinbox WhatsApp 


KANZIO:
Kujenga madhabahu ni maamuzi yako sababu ni wewe mmoja ndiye utakayetakiwa ujenge uhusiano wako na Mungu.

USITOE SADAKA HII BILA KUNIELEZA UPEWE MAELEKEZO YA KUIOMBEA SADAKA HII KABLA HUJATOA ITAENDANA Sawasawa NA MAHITAJI YAKO NA SADAKA UNAYOMTOLEA BWANA KUJENGA MADHABAHU 

MWISHO 
Namshukuru Mungu Kunipa Somo hili nawewe kulipokea Roho Mtakatifu akakuhudumie akupe kulielewa kwa upana.


WITO
Kama Bado hujaokoka Okoka sasa
Nifate inbox WhatsApp niambie nataka kuokoka +255759861768 Kisha nitakuambia upige

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.