SOMO : MAOMBI YA UKOMBOZI WA TABIA.

SOMO: UKOMBOZI WA MAOMBI YA TABIA.

Unajua Kuna Watu wateswa na tabia kiasi kwamba hata kuowa hawaowi kuolewa hawaolewi kutokana na tabia zao hata iwe ofisini makazini tabia inawagombanisha na watu na saa nyigine wamekosa msaada hata mtu aseme awasaindie Kwa Tabia zao anaweza Jutia. Nataka Niseme unaweza ukawa unaona kawaida Sana kumbe roho chafu roho za kipepo zinakuopareti kupitia Tabia na unabaki kuwa mtumwa wa shetani.
Kubali Leo hii ujikomboe ili ukamuone Mungu akitenda kwako.

Naitwa Pastor Richard 
Nipo Morogoro Veta Dakawa 

WhatsApp niinbox +255759861768


MAANA YA TABIA..?
Tabia ni Mwenendo wa kitu.
Kinachokitambulisha kitu juu ya anayekiona.

Ambapo huu mwenendo hutengeneza utambulisho wa kitu kukijua mfano Silika ambapo viumbe vyote isipokuwa mwanadamu. Vinasilika yake ukiona mbwa tabia zake zinakujulisha ukiona mahindi tabia zake zinakujulisha.

Mwanadamu huongozwa na Utashi wake wa kujua njema na mbaya kwa mtu mwenye tabia mbaya tunasema muovu kwa mtu mwenye tabia nzuri tunasema Mwema.

TABIA KWA MTU HUMPA MATOKEO MAWILI.

1:TABIA INAWEZA IKAKUFANYA USIFANIKIWE.

Wapo watu mpaka tabia zao wazirekebishe ndiyo watafanikiwa adui kawapiga kwenye eneo la tabia tu.


2;TABIA INAWEZA IKAKUFANYA UFANIKIWE

Kupitia tabia inaweza kukufanya ufanikiwe na uishi vizuri na watu na Jamii iliyokuzunguka.

Tusome huu mstari
👇👇👇👇👇
1 Wakorintho 15:33
[33]Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema. 

Hakika Mazungumzo Yasiyo na utukufu kwa Mungu huharibu tabia yako.


KUNA AINA ZA TABIA.

1:TABIA YA KUZALIWA NAYO.
Hii ni tabia inayokuja kwako bila kujifunza kutoka kwa watu ambayo huitwa tabia ya kurithi.

Mfano. Mama yako alikuwa anazaa watoto kila mtoto na Baba yake au Baba yaku alikuwa na wanawake kila kona nawewe unakuja kuanza kuishi hiyo tabia.


2:TABIA YA KULELEWA NA WAZAZI 

Hii ni Tabia na Mienendo unayoipata baada ya kufunzwa na wazazi au walezi Inaweza ikawa tabia nzuri au mbaya.

3:TABIA YA  KUJIFUNZA KUTOKA KWA WENGINE 

Hizi ni tabia mbalimbali ambazo mtu huweza kujifunza na kuziaga kutoka kwa marafiki wasanii Watu maarufu wazazi na walezi mtu unaweza kuiga tabia kutoka kwa haya makundi niliyoyataja.


NAMNA YA KUJIKOMBOA KUTOKA KWENYE TABIA HIZO.

Zingatia haya kabla hujaanza kuomba

1:Utambue tabia ipi inayokutesa

2:Anza Kubadilika na Kukataa kuwa mtumwa wa hiyo Tabia.

3:Utaomba kwa kufata maelekezo ya maombi

4:Muda utakaoutenga kuwa unaomba usipishanishe pia omba ukiwa umetulia.

5:Utakuwa na Sadaka Kiasi chochote katika maombi haya na hautaomba ukiwa umefunga.

6:Utaomba siku 7 Siku hiyo ya 7 Utatuma Sadaka yako na utanipigia nakuombea unaniambia ulikuwa maombi ya kujikomboa tabia.


VIPENGELE UTAKAVYOSHUGHULIKA KUJIKOMBOA 

1;TABIA YA KURITHI 

Mfano utakaoufata unapoomba.
Taja tabia uliyorithi kataa 

Baba Katika Jina la Yesu Kila tabia niliyoirithi kutoka Baba Yangu Mama yangu hii tabia ya Hasira Tabia ya umalaya siitaki ndani yangu Sitarithi Tabia mbaya mimi kwa Jina la Yesu Nakataa uvutaji Singara nakataa kuzaa nje ya ndoa kama mama yangu katika Jina la Yesu.Amen 

Omba kwa mfumo huu

Kisha Soma huu mstari

Yakobo 5:16-17
👇👇👇👇👇👇👇
[16]Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. 

[17]Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita. 



2;KUJIKOMBOA KWENYE TABIA YA KUJIFUNZA.
Hizi nitabia unazozipata kutoka kwa watu wegine ukajifunza sasa kuna tabia ambazo huwa mbaya unaweza Kuiga.

Mfano wa uombaji.

Tabia zote mbaya nilizojifunza kutoka kwa marafiki zangu tabia ya kusema uogo tabia ya kuzini tabia ya kutoa mimba tabia ya kwenda disco tabia kunywa pombe Tabia kupenda Pesa Kuliko utu naiharibu hizo tabia ndani yangu zibomoke zinitoke ziniachie katika Jina la Yesu.Amen 

Fata mfumo huu 

Soma hiki kitabu mistari hii simamia

   Waebrania 13:5-8
👇👇👇👇👇👇
[5]Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. 


[6]Hata twathubutu kusema, 
Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; 
Mwanadamu atanitenda nini? 


[7]Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao. 


[8]Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele. 

3:KUJIKOMBOA KUTOKA KWENYE TABIA YA MAKUBALIANO.

Hii huwa ni Ile tabia Unakubaliana na mtu mtaoana au muishi kama mke na mume gafla mtu  mmoja kati yenu anavunja hayo makubaliano kumbuka roho itakayokufatilia ni yale makubaliano yenu. Kama kudumu kwenye mahusiano inakuwq ngumu sababu unaishi katika ulimwengu wa roho unamakubaliano ya ndoa na mtu ambaye ulishaachana nae.

Utaomba kadiri roho atakavyokusaindia.

Mambo ambayo uyataje kuvunja kila makubaliano ambayo ulisha yafanya hapo mwanzo Jitenge na kila mapatano ambayo uliyaweka kwa wapenzi wako wa zamani .

Fata makubaliano ya kibiashara ambazo leo unaona zinakufa kube uliwahi kwenda kwa mganga ukakubaliana kitu.

Omba mpaka uone maneno yameisha.

Mfano wa uombaji.

Ninakiri makubaliano yote ambayo niliyaweka kwenye mahusiano kati yangu  na Richard kuwa kweli tulipatana ataniowa/nitamuowa lakini kwa tabia zake na mienendo yake sitaki kuolewa naye navunja haya makubaliano katika ulimwengu wa roho nataka yaniachie mimi niolewe/niowe mtu uliyemwandaa wewe Mungu wangu nafungua kila kifungo cha makubaliano ambacho nilkiweka sitakuja kumuacha au kuowa/Kuolewa na mwigine katika jina la Yesu.

Mfano kama ulienda kwa Waganga
Navunja kila makubaliano ambayo niliyafanya kwa mganga wa 1 Tabora wa 2 Iringa wa 3 Kigoma(Hapa utataja waganga wote ambao ulishawahi kuwafikia) Niliacha nguo zangu nikapeleka kuku au mbuzi ili kukamilisha makubaliano yangu na Madhabahu za kiganga ninazivunja katika Jina la Yesu.Amen 

Soma hii mistari
👇👇👇👇👇
1 Wakorintho 2:14-16

[14]Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. 


[15]Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. 

[16]Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo. 


HITIMISHO 

Maombi haya Ni hiyari kwa yeyote kifungo chake kipo kwenye tabia kuomba pia ni hiyari kuacha kuomba.

Ruhusu moyo wako ukuambie inawezekana matatizo yote unateseka ni tabia.


Mwisho 

Shukurani Zangu Kwa Mungu katika Roho Mtakatifu kunifunulia maombi haya pia nishukuru wote mnaozidi kuniombea katika kufanikisha kuhudumia watu mtandaoni na wanafunguliwa.

Naitwa Pastor Richard 
Nipo Morogoro Veta Dakawa 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.