SOMO:LENGO KUU LA MUNGU KUTUPITISHA KWENYE MAPITO
SOMO; LENGO KUU LA MUNGU KUTUPITISHA KWENYE MAPITO MAZITO.
UTANGULIZI.
Inawezekana Kabisa hata wewe saivi upo unapitia kipindi kigumu mapito mazito mpaka umewaza moyoni Umuache Mungu au Kuona Mungu Amekuacha Nataka nikuambie unayoyapitia Mungu alijua utayapitia kwanini basi ameruhusu iwe pito kwako kwa sababu kwanza anakupenda na Anaimani kubwa na wewe na anajua hutamsaliti ni vyema kuendelea kutunza uaminifu wako na Mungu.
Karibu ujifunze kupitia Somo hili.
Naitwa Bishop Richard nipo Tanzania Morogoro Veta Dakawa
WhatsApp +255759861768
KUNA MAMBO MANNE MUNGU HULENGA KUJIPATIA KUPITIA TUNAPOPITIA VIPINDI VIZITO.
1:KUTUSAFISHA NA KUJIHAKIKISHIA KAMA TUNA IMANI NEYE KATIKA MAJIRA YOTE.
Soma: Yakobo:1:2-4
Mungu hutumia majaribu kuchunja watu walio wake na wasiokuwa wake kujua watu wenye imani nayeye kujua watu wake walio wavumilivu ambao wataendelea kumwamini na kumtengemea. Ndugu yangu majaribu hutusafisha na kujua tunapokosea nakutengeneza upya na Mungu tena katika maisha yetu.
2:KUUMBA UTU MPYA NDANI YETU.
Soma: 2Wakoritho.4;8-17
Mungu hutuumbia utu mpya ndani yetu kama kumpenda zaidi Mungu Kuwapenda wegine kuwaombea wegine kuwa mabalozi wanzuri wa injili ya kristo Tabia Zetu kubadilishwa na hata kujifunza jinsi ya kuyaacha yanayomkosea Mungu. Hutufanya watu wengine wajue Tuna Mungu Kweli Kweli kama wakristo Anapokuwa Ametutendea.
3:TUNAPOSHINDA TUNAWASANDIA WEGINE
Soma:2wakoriho. 1:3-7
Mtu anayekuwa amepitia kipindi kigumu akija kupavuka hapo atawasaindia wengine wanaopitia kipindi kama chake utamwambia hata mimi niliweza Kupitia Kipindi kama chako lakini nilipona kupitia maombi tu. Yule naye ataamua kufata maombi na kumjua Mungu zaidi katika kipindi hicho naye akija kuvuka atamsaindia mwingine.
4:KUTUFUNDISHA KUMTENGEMEA MUNGU.
Soma: 2wakoriho.1:8-10
Hakika Katika Kipindi Kigumu ndicho pekee kipindi kinachomfanya mtu Amtafute Mungu Sana Zaidi ya Vipindi vyote anavyopitia mwanadamu hapa duniani na MUNGU HUJITUKUZA KWA KUTUTENDEA MAKUBWA HALI INAYOTUFANYA TUAMINI MKONO WA MUNGU UPO UNAWEZA KUFANYA TUSIYOYAWEZA KATIKA MAISHANI MWETU.
TUFANYE NINI SASA
✍✍✍✍✍✍✍✍
Hakikisha Humuachi Mungu Upitapo katika Kipindi Kigumu na Hurudi nyuma Vumilia na Kuwa na Subira Kwa Mungu hata kama amechelewa kutenda na Kujibu kwako Tabua lengo lake Mungu Ajiaminishe Kweli unampenda au umeokoka kufata tu uponyaji ukishaponywa umuache maana watu wengi wanapoteza imani wanapopita kwenye pito bila kujua wapo kwenye mchunjo wake Mungu kutambua walio wakristo kweli.
HITIMISHO
Lengo LA Mungu kukuweka Duniani Umwabudu na Kumtumikia Katika kile uchonacho au alichokupa lakini wengi huharibu mahusiano yetu na Mungu tukibarikiwa.
NIKUALIKE SASA.
Inawezekana umemkosea Mungu dhamira yako inakushuhudia utubu upatane na Mungu au uokoke
+255759861768 Nipigie Saa 12:00jioni mpaka saa 2:45 usiku
Share link ya Group WhatsApp kwa marafiki na ndugu wauge kwenye Group
Maoni
Chapisha Maoni