SOMO:JINSI YA KUFIKIA MALENGO YAKO

SOMO: JINSI YA KUFIKIA MALENGO YAKO ULIYOJIWEKEA KATIKA MAISHA YAKO .

🍇🍇🍇🍇🍇🍇🍇🍇🍇🍇🍇🍇🍇

MALENGO NI NINI?

NI Ramani Zima Ya Maisha Yako Huwezi kufikia malengo kama Ramani yako kwenye akili yako na ufahamu wako.

Kupitia Somo Hili Linakupa mbinu na njia zitakazo kusaindia wewe Kufikia malengo Yako  Soma kwa umakini nakufatilia poit moja baada ya nyigine.


Naitwa Pastor Richard 

Nipo Morogoro wilaya ya Kilosa Kata Ya Mbigiri Kijiji cha Mateteni 

WhatsApp +255759861768


1:CHANGUA MALENGO YALIYO NDANI YA UWEZO WAKO.

Ni vyema unapopanga malengo uyaweke yaliyo ndani ya uwezo wako ili kukurahisishia kuyafikia malengo yako.

Mithali 22:1

[1]Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu. 

Matendo ya Mitume 15:7

[7]Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa tangu siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwenu ya kwamba Mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini. 

Mungu yeye ni mwanzilishi wa kuchangua vitu ambavyo anataka avitumie na Kufikia malengo yake anapofanya jambo.



2:WEKA MUDA WA KUYAFIKIA MALENGO YAKO.

Kila Jambo linatakiwa liwe na mwisho unapolipanga kulifanyia kazi usiweke malengo yasiyo na muda 

Muhubiri:3:1

Yohana 9:5

[5]Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu. 

Matendo ya Mitume 13:18

[18]Na kwa muda wa miaka kama arobaini akawavumilia katika jangwa. 


3:ANDIKA MALENGO YAKO .

Hakikisha moyo wako unayaweka malengo nakuyasimamia kuwa unajikumbusha mara kwa mara.

Kutoka 17:14

[14]BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu. 

Mungu alitumia hata watumishi wake hapo zamani walikuwa wakiandika ili iwe wanajikumbusha.

Yeremia 45:1

[1]Neno hili ndilo ambalo Yeremia, nabii, alimwambia Baruku, mwana wa Neria, alipoyaandika maneno haya katika kitabu kwa kinywa cha Yeremia, mwaka wa nne wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, kusema, 

4:WEKA MIKAKATI YA KUFANYA KITU KILA MWEZI KWA AJILI YA LENGO LAKO.

Jiwekee mkakati kabambe wa kufanyia kazi kutimiza malengo yako kila mwezi fanya jambo.

                     Mwanzo 2:2

[2]Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. 

1 Wathesalonike 4:11

[11]Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza; 


5:AMINI MUNGU NAMKABIDHI MALENGO 

Imani yako inatakiwa ijiaminishe inaweza kuyafanya malengo yako kutimia pasipo utengemezi wa mtu mwigine. 

Mwanzo 15:6

[6]Akamwamini BWANA, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki. 

Luka 8:13

[13]Na wale penye mwamba ndio wale ambao wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga. 

6: JIFUNZE KUKUBALIANA NA MAZINGIRA YAKO ULIYONAYO.

Maisha yako ili uweze kuyabadilisha yanaitaji ukumbaliane na wewe mwenyewe ulivyo ukiyakubali mazingira yako ndiyo yatakayokupa nguvu ya kuanza kuweka malengo yako.

Mithali 2:1

[1]Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu; 

Isaya 1:19

[19]Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; 


7:USISHIKILIE LENGO USILOLIWEZA.

Muda utakaokuwa umejiwekea utakupa picha nzima kuona lengo lako limetimia kama muda ukaisha lengo hujatimiza basi lipo nje ya uwezo wako.

Kutoka 16:28

[28]BWANA akamwambia Musa, Mtakataa kuyashika maagizo yangu na sheria zangu hata lini? 

Zaburi 31:6

[6]Nawachukia wao washikao yasiyofaa yenye uongo; Bali mimi namtumaini BWANA. 

8;ZUIA VITENDO VYOTE VINAVYOTISHIA KUA MALENGO YAKO.

Hakikisha unayaombea malengo yako na kujiepusha na vitendo vyote vinavyotaka kuua malengo yako jitaidi kulinda na kutunza malengo yako.

2 Mambo ya Nyakati 7:15

[15]Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa. 

Zaburi:20:1


TUFANYAJE SASA KUYAFANYIA KAZI HAYA YOTE 

✍✍✍✍✍✍🍇🍇🍇🍇🍇✍✍✍✍✍✍

Kwa kuwa Tumejifunza namna ya kufayafikia malengo Yetu ni vyema sasa kuyapima malengo tuliyonayo je yapo ndani ya uwezo wetu au nje ya Uwezo wetu kama yapo nje ni vyema kuachana nayo kwanza nakushika  yaliyo ndani ya uwezo wetu.


Tutumie hizi njia ili kufikia malengo yetu ya mwaka huu pia kwa msaada zaidi wa kiroho 


Nifate WhatsApp Pastor Richard +255759861768

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.