SOMO:SIMU ISIYOOKOKA

SOMO: MADHARA YA SIMU AMBAYO HAIJAOKOKA.

UTANGULIZI. 

Simu ya mkristo aliye hai kiroho hutakiwa nayo imjue Mungu na Ihifadhiwe mambo yanayoendana na Tamanduni ya Misingi ya Kikristo ni  vyema kutokuruhusu Simu iwe chanzo cha wewe kumkosea Mungu au Kuharibu maisha yako ya wokovu uliyoyapata kwa gharama nyigi.

Napenda Nikukaribishe Katika Somo hili Kama wewe ndiyo mara kwanza kuanza kunifatilia Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa 
WhatsApp Pastor Richard +255759861768 

Rejea Vitabu. Mambo ya Walawi.25:14,17
Hawaii.1:5  Zakaria;1:4

SIMU ISIYOOKOKA INASIFA HIZI.

1:Imebemba majina ya uogo mengi kwenye file la majina yameseviwa kwa majina ya uogo.

2.Imebeba Picha mbaya za aibu za uchi  zisizoendana na maadili ya ukristo kabisa.

3;Imebemba Video chafu za ngono 
Kama wewe Mkristo unatazama video kama hizo utawezaje kuushinda uzinifu ni ngumu.

4:Inatumiana Sms Za Wapenzi wengi na chati zake za mahusiano hayupo mmoja na majina yao yanakuwa yameandikwa Tofauti Tofauti

5:Inapasword kila kona kwa sababu ya kujihami isije ikakamatwa na mtu mwigine akaona uchafu unaofanywa na mmiliki wa simu hiyo


MADHARA YAKE NI HAYA KAMA SIMU YAKO
HAIJAOKOKA

1:Unaudanganya Moyo wako kwa Mazungumzo yenye kupelekea uagamie mikononi mwa adui.
🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍐🍐
Tusome hili andiko
1 Wakorintho 15:33
[33]Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema. 

2:Hupelekea Simu ikufanye utende dhambi na dhambi ndiyo chanzo cha wewe kuanza kuwa na matatizo au magonjwa Kukosana na Muumba Wako kwanini usiepuke sasa hivi.
🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍇🍇🍇
Rejea hili andiko
1 Wakorintho 15:34
[34]Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe. 

3:Hukufanya Usipate nafasi ya Kuona Kosa lako utakuwa unajiona upo sahihi machoni pako kumbe inakuvuta kukuagamiza kabisa.
🍉🍉🍉🍉🍐🍐🍉🍉🍉🍉🍈🍈🍈🍈🍈
Rejea hili andiko.
Mithali 14:12
[12]Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, 
Lakini mwisho wake ni njia za mauti. 


4:Simu Yako Usipoiongoza maadili Yenyewe ndiyo itakupoteza na Kukuaminisha kitu kilicho chukizo kwa Mungu uone Kawaida tu.
🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉
Rejea andiko hili.
Mithali 14:15
[[15]Mjinga huamini kila neno; 
Bali mwenye busara huangalia sana aendavyo. 

5:Simu Isiyookoka huamsha Tamaa za kufanya uzinifu sababu haina mipaka ya jumbe na chati zake kutokana na mwenye simu mwenyewe anavyoitumia.
🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉
Rejea andiko hili
2 Timotheo 2:22
[22]Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi. 


HITIMISHO 

Ni kweli Simu inatusaindiya katika mawasiliano lakini ni nzuri Endapo mmiliki mwenyewe wa Simu ataamua imjue Mungu kwa hiyo itaelekezwa katika maadili na misingi kama watu waliokolewa na Kutengwa mbali na dhambi  lakini kama simu yako haitaokoka bado ndiyo itakuwa chanzo cha wewe kupotea na kukosana Na Mungu wako.

Itunze neema hii hata kama umeipata bure haina maana ndiyo ujiachie kuwa huru bila kujiwekea mipaka ya kiroho mwenyewe. 

Mungu awabariki Sana Somo hili likaponye hata ndoa zilizokuwa zinafarakana chanzo simu haijaokoka.

WITO

Je Unatamani uokoke au uombewe basi nipigie jioni saa 12:00 mpaka saa 2;00 Usiku
Simu +255759861768


Kama Unaweza Kushare Basi share hili Somo kwenye magroup mbalimbali. 




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.