SOMO. Tabia za Mkristo wa Kweli

SOMO:TABIA ZA MKRISTO. .

Tunaposema Tabia Mienendo Ya Mkristo Unapokuwa huna Tabia hizi Halafu Unatuambia wewe Mkristo Unatupa mashaka Sana Ambao ni Wakristo. Kuna wegine hata wakikutana na mchungaji wao wanamuita mtumishi  au Baba mchungaji Au Mchungaji hana Ujasiri wa kuita Baba kwakuwa hana Sifa na Tabia za Kikristo Mchungaji Yoyote anayekulea kiroho Haijalishi awe mdogo kwako au mzee muite Baba Hii ndiyo Sifa Ya ukristo Baba Si Kwamba unampa utukufu heshima kama amri ya Nne waheshimu Baba na mama upate miaka mingi heri na Baraka nyigi zipo kwa wazazi wa kiroho.

Naitwa Pastor Richard Nakukaribisha Somo hili Soma Kwa Utulivu na Kwa Umakini  Poiti hizi

1:Awe mtu wa Kuhudhuria ibada. Waebrania:10:25
Huwezi Ukajiita Mkristo halafu kanisani huendagi Hapana huo siyo ukristo ni upangani wa kiroho. 

2:Awe mtu wa ibada nyumbani Kwake.
Matendo.5:42
Huwezi Ukajiita Mkristo halafu Usiwe mtu wa Ibaada nyumbani Usiku ukifika nyumba haina ibada kila mtoto anaenda kulala hamjafanya ibada hii siyo tabia ya Mkristo ni tabia ya wapagani wa kiroho.

3:Awe mtu wa kuhubiri injiri kwa matendo na uvaaji wake
2;Timotheo.4:5
Huwezi Ukatuambia Mkristo Halafu tunakuona kila siku upo uchochoroni na vijani saa nyigine unabadilisha tu wanawake na wanaume kama Nguo au Tunakuona unaenda kwa mganga au Tunakuona uvaaji wako kama makahaba wanaojiuza au Unanyowa kama mhuni Jinsi Jamii inavyokuona inatakiwa ifikie hatua watu watafute makosa yako wasiyaone mpaka wanasema huyu kijana Ameokoka Kweli.

4;Mtu wa Kushirikiana na Wengine Kanisani na katika Jamii. YOHANA.17:21
Huwezi Ukawa Mkristo mtu Tunatangaza kanisani Tutakuwa na usafi kanisani hauji Yaani wewe unajitenga tenga Tu nakisingizio kila siku hushirikiani na wegine halafu unasema mimi nami mfuasi wa Yesu Kristo  Baadilika hiyo siyo tabia yake kristo.

5:Uwe Mtu wa Utoaji Unayependa Kazi Ya Mungu iende mbele.
Wagaratia:2:10
Kuna watu ukiwaambia Utoaji ndiyo ataanza kukuhesabia Changamoto zake Fomula ya Mungu Toa Nayeye Ajitoe Kukuhudumia mahitaji yako Jifunze kujitoa Mali zako Muda wako Mwili wako Hatuwezi Kukuhesabu mkristo wakati hata kujitoa Hutoi.

6:Uwe Mtu wa Maombi Na shukurani kwa Bwana
Wafilipi:4:6
Huwezi Tukakuita Mkristo halafu kuomba huombi huwa hupendi Kusali. Lazima Ujifunze Kuomba Na Ujizoeshe Kusali Hii ndiyo Tabia ya mkristo kusali


7:Uwe Mtu wa Kujishughulisha na Kazi Ya kimwili.
Mwanzo.31:42
Huwezi ukawa mkristo hutaki kufanya Kazi na Huwezi Ukaitwa mkristo bila Kujishughulisha Na Kazi au shughuli Yoyote inayokuingizia Kipato. Fanya Kazi ili upate hata Sadaka na Zaka ya Bwana. Pia ushiriki kuijenga kazi ya Mungu.

8:Awe mtu wa Kusamehe wegine na Kutokubemba moyoni.
Mathayo.6;14-15
Huwezi ukaitwa Mkristo halafu unabemba watu moyoni mwako huwa husamehi.

9:Awe mtu wa kushauriwa 
Mwanzo;27;10-20
Huwezi ukaitwa Mkristo halafu hupendi Kushauriwa na Kukemewa. SABABU unaposhauriwa na Kuonywa ujuwe huyo anayefanya hivyo anakupenda hataki upotee.

10:Awe mtu wa kuigwa na wegine Siyo mtu wa kuabatana tabia za watu wasioamini.
2wakoritho.6:14
Jamii inatakiwa iinge Kwako Siyo wewe Uwe mtu wa kuinga watu wa mataifa.


        #HITIMISHO 
TABIA ZA MKRISTO NI KIELELEZO TOSHA YA KILA MKRISTO AWE NA MWENENDO KAMA KRISTO YESU YEYE NI NURU Anatakiwa Awe Nuru Kweli Kweli.

WITO
Kwa Maoni na Mapendekezo Mtumie WhatsApp Pastor Richard +255759861768
Yupo Morogoro Veta Dakawa 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.