SOMO; KUSIFU NA KUABUDU
SOMO: SIFA NA VIGENZO VYA MTU WA SIFA NA KUABUDU KANISANI
Hizi sifa zinalenga watu wote wanaokuwa wanatuongozea sifa na kuabudu kanisani Kuna Vincenzo Mungu huvitazama ili ashuke katika ibada ya kusifu na Kuabudu
Karibu nakala hii imeandaliwa na mtumishi wa Mungu Pastor Richard yupo Morogoro Veta Dakawa WhatsApp yake mfate inbox +255759861768
sifa zifuatazo Za Mtu Anayemuabudu Mungu
1) Anakiroho kizuri/ameokoka vizuri –(Yoh4:23, Yak2:19)
2) Awe na kiu ya kumjua Mungu –msomaji wa Neno, mwombaji, mshuhudiaji na anaukulia wokovu
(1Pet2:2, Mith8:17-kumtafuta Mungu kwa bidii)
3) Awe na wito (1Kor12:28-maongozi, Efe4:11-15, kila kiungo kufanya kazi yake ,Mith17:8-
kipawa/kito cha thamani )
4) Ajitoe sadaka (sacrifice) (Rom12:1)/Moyo safi ,mikono safi ,unyofu wa moyo –Zab.24:3-4, 33:1,
51:17, Isa57:15,66:2b ,
5) Aishi maisha matakatifu (hana udunia wala haleti udunia kwenye ibada)-Mtakatifu
/aliyetakaswa/mtauwa –Zab149:5, Ebr13:15, Yoh13:3-10, 1Yoh1:9.
6) Dhamiri safi –Ebr10:22
7) Unyenyekevu –Zab89:7
8) Mavazi ya wokovu (si uchi )-Zab132:16, 1Kor3:16-17
9) Aliye tiwa mafuta /waliojazwa Roho Mtakatifu-Yoh 4:23,Ef2:18,5:18-19
10) Awe na mandalizi ya ibada na ya huduma (kuandaa nyimbo,kufanya mazoezi ,mavazi ya staha
/heshima ,sadaka ,maombi n.k )
11) Awe mtu wa kuwahi na kutunza muda kwenye matukio hususani ambayo Mungu ameahidi
kuwapa (Mat18:20), kukomboa wakati (Ef5:16,kol4:5)
12) Aimbe na /au kupiga vyombo kwa ujasiri /kujiamini na ustadi.
Kimsingi, Anaye sifu awe ameokoka vizuri –mtakatifu (Zab16:3)
Ipo haja ya kujifunza na kuendeleza kusifu na kuabudu kwa kuzingatia wasifu ulioelezwa hapo
juu.
MASHARTI YA IBADA YA KUSIFU NA KUABUDU KUKAMILIKA
Ili ibada ya sifa na kuabudu ikamilke inahitaji uwepo wa Mambo haya.
1) Anayeabudiwa Mungu uabudu katika roho(Yoh1:1-3, Yoh4;20-23)
2) Anaye/wanao-abudu Awe amejitakasa sababu anaabudu kitakatifuYoh4:23)
3) Vitendea kazi vya ibada Viwepo–vyombo vya mziki, utoaji wa sadaka,na watu (1Nya16:29, Kumb 16:16-
usitokee mbele za Bwana mikono
HITIMISHO
Sisi kama kanisa la Kristo Inatupasa kuiandaa ibada hii iwe nzuri watu wafunguliwe Tusisifu kwa mazoea au kumwimbia Mungu Kwa Mazoea.
Ni vyema Tuchangue nyimbo zitakazo ngusa pindo la Yesu nakumfanya ageuke atuhudumie tusiimbe nyimbo zisizompa sifa Mungu au Zenye kujifariji mfano.
Nyimbo za kujifariji
Fuga Miranda Pambana---Ninapendwa na Baba
Nyimbo zinazomsifu Mungu
Eeh Baba Pokea Sifa-----Naribariki Jina lako Baba wa mbiguni-----Sifa ni zako nk
Tunga wimbo unainua utukufu kwa Mungu kwa waalimu waandaji wa nyimbo makanisani.
Usiimbe nyimbo zakutiana moyo au kujifariji mwenyewe
:MWALIKO.
Tunaitaji Wanasifa kuanzia Leo makanisani mtunge nyimbo zinazomtukuza Mungu.
Pia uchezaji wa sifa na Kwaya ni vitu viwili tofauti
Kwenye sifa hatuna viduku au kukata mauno tunasifu kwa heshima na Kwa Adabu hasa ukijua unayemsifu.
Naitwa Pastor Richard
Nikuombe share kwenye magroup yote
Maoni
Chapisha Maoni