SOMO:JINSI YA KUWEKA NADHIRI
SOMO: JINSI YA KUWEKA NADHIRI KWA MUNGU
UTANGULIZI
Nadhiri huwa ni ahadi au kiapo unachokitoa kwa kupatana na nafsi yako pasipo kushawishiwa au Kulazimishwa na mtu.
Nguvu ya nadhiri huwa ni kubwa sana kwa mnadhiri yaani yule aliyeweka nadhiri kwa Mungu Sababu humfanya Mungu Atende Jambo hilo aliloweka nadhiri kwa kuabatanisha na kitu cha thamani au fedha au kitu kisichohamishika. Nadhiri huwekwa na Watu wanaojitambua nakujielewa Nini wanaweka na kwanani.
Nadhiri inaweza kuwekwa moja au Zaidi kila nadhiri ikiwekwa husimama na nakiapo chake na nadhiri yake.
Mfano; Mwaka huu nikjpata kazi mshahara wa kwanza ni wa Mungu
#Mwaka huu nikiolewa nitamtolea mshahara wangu wote
#Mwaka huu nikifanikiwa mtoto nitatoa viti kanisani
Hizi Nadhiri hupaswi ujumuishe Sadaka ya kwenye Kupata kazi ndiyo hiyo kwenye ndoa laa! Viginevyo utamke neno moja linalojumuisha sentence hii moja kwa wakati mmoja.
Mwanzo;28:20-22
Nakukaribisha Katika Somo hili Nayekuadalia nakala hii Naitwa Pastor Richard
WhatsApp +255759861768 Niinbox kama unataka kuweka nadhiri kwa Bwana.
MAANA YA NADHIRI: Ni Ahadi Inayotolewa na mtu kwa Mungu akibatanisha Kitu.
MAMBO AMBAYO UWE NAYO MAKINI KABLA HUJAWEKA NADHIRI.
_________^^^___________^^^^^^______^^^^^_____
1:Nadhiri huwa lazima ilete matokeo sawasawa na ahadi yako kwa Mungu.
Rejea 1samweli;1;11
2:Nadhiri huendana Sawasawa na Sadaka yako unayomtolea Mungu
Rejea Hesabu;6:21
3:Nadhiri utakayoitamka Huwa lazima itimie kama ulivyosema mwenyewe.
Rejea Hesabu:30:12-13
4:Nadhiri Usipoiondoa Itakuwa Dhambi kwa Mungu wako itakayokufata milele.
Rejea Kumb.Torati;23:21-22
5:Nadhiri Huondolewa Kupitia Madhabahu uliyowekea au Eneo Ulilotamka ukiwepo.
Mfano. Unasali T.A.G lakini umefika hapa Kanisa la Moto Wa Yesu ukasema Pastor Richard nitatoa mabati 100 Mia nikipata kazi halafu ukapata ukaenda kutoa T.A.G Tayari ni kosa nadhiri yako inakuwa haijafutwa.
Rejea 2Samweli:15;7-10
6:Ni Amri ukiweka Nadhiri lazima uiondoe mwenyewe Tena Usichelewe kuiondoa.
Rejea vitabu:Zaburi;76:11 Zaburi.116:14 Muhubiri:5:4
7:Nadhiri Usiweke Kama unaona hutaweza kutengua Nadhiri yako kuliko uweke kisha usiitegue.
Rejea Muhubiri;5:5
8:Usilete Mchezo au Kumdaganya Mungu Kwenye Nadhiri Halafu Ukamtolea Tofauti na ulivyosema.
Rejea Malaki;1:14
9:Weka msimamo wa Nadhiri yako
Rejea Matendo;18;18
Haya ndiyo Yatazame kabla hujaendelea kuweka Nadhiri
BAADA YA HAPO UNAWEZA KUINGIA MAHALI TULIVU AU KANISANI AU CHUMBANI
Utaongea siku tatu mpaka 7 ukimkumbusha Mungu lakini Soma kwanza mambo ya kuzigatia
Ongea hivi au Fata mfano huu.
1:Naweka Nadhiri Mbele zako Mungu Ukinipa ndoa mwaka huu nitakutolea sipika moja kanisani ili ihubiri injili yako na ikawalete watu kwako nitafanya hivyo baada ya kutolewa mahari tu nitafanya hivyo naomba mwaka huu mpaka mwezi wa Saba n. (KAMA WA KIUME TAMKA KINYUME)
2:Naweka Nadhiri mbele zako Mungu wangu nikipata kazi serikalini nitakutolea Mshahara wangu kanisani nitanunua viti mshahara wote ili watu wakae wakati wakifika nyumbani kwako kusikia Neno lako.
3;Naweka Nadhiri Kwa Mungu wangu Nikipata mtoto nitamtolea Bwana Kiwaja changu kilichopo Ilenje mbeya Lijengwe kanisa.
Kumbuka Nadhiri yako ielekeze unaitoa ikafanye nini na ni vyema hata ukija kuitengua nunua kile Ambacho Mungu ulimwahidi.
HITIMISHO
Tafadhali Fata mtiririko huu unapoweka nadhiri kwa Mungu na Kisha Ukitaka kuja kuitengua utaitengua kupitia hii madhabahu ya Moto Wa Yesu.
Kwa Wale Wanaotaka kufuta nadhiri zao
Nifate inbox upewe maelekezo
Kama unatimiza nadhiri nifate inbox uniambia uliweka nadhiri ngani nikuelekeze jinsi ya kuifuta.
WhatsApp Pastor Richard +255759861768
Maoni
Chapisha Maoni