SOMO:2023 #IJUE NDOTO YAKO
SOMO:IJUE NDOTO YAKO MAANA YAKE UNAJULISHWA NINI?
Tunaongozwa na AYUBU:33:14-15 Mwanzo;37:5-20 Yeremia:23:23-32
Danieli:2;5-45
Motto : 2023 Ni Mwaka Wa Majibu.
ZABURI. 20:1
UTANGULIZI
Ndoto huwa ni taarifa anayopewa muotaji juu ya jambo litakalotokea au Linaloendelea wakati huo au lilishapita Siyo kila ndoto ni Ya Mungu hata shetani huweza kumuotesha mtu ndoto na si shetani tu hata akili ya mtu anapochoka na mawazo ya kufikiria Jambo au kulipenda jambo Sana Usiku akilala huweza kuota Sasa unawezaje kutofautisha Ndoto a Anayokuotesha shetani na Mungu fatana nami katika somo hili
Naitwa Bishop Richard kutoka Kanisa la Moto Wa Yesu Morogoro Veta Dakawa WhatsApp +255759861768 nakukaribisha katika Somo hili litakalokufanya ujue maana ya ndoto yako
NDOTO ZIPO MAKUDI MATATU.
1:NDOTO ZA MUNGU= Hizi huwa ni ndoto unazoziota zisizo za kutisha au kukimbizwa ndoto nzuri zote huwa za Mungu Na Lengo lake kukuotesha kukujulisha jambo linaloenda kutokea lilopo au lilishatokea
2:NDOTO ZA SHETANI =Hizi Huwa ni Ndoto zote utakazoziota za kutisha zisizoeleweka unaanza ndoto kuota bado haijaisha unauganisha nyigine au ndoto haina mwisho au mwanzo
Lengo LA Mungu kukuletea ndoto hizi za shetani ujue ni Jeshi lipi linakutesa na tatizo lipo wapi ili ikurahisishie kutatua tatizo lako.
3;NDOTO ZA UCHOMVU WA AKILI= Hizi ni Ndoto unazoziota unakuwa unawaza Sana au Unafikiria Sana au Unapenda Sana ukija kulala utakiota ulichokuwa unakiwaza.
Lengo La Mungu kuruhusu hizi ndoto kukujulisha akili inachoka inashindwa kutatua mengine sababu umeshindwa kuondoa vitu akilini mwako.
#NDOTO NA MAANA YAKE.
1:Ukiota inatembea Kwenye Tope= Unajulishwa acha mara moja tabia ya kuzini.
2:Ukiota unatembea unateleza upo barabarani=Unajulishwa njia au matendo yako hayampendezi Mungu uache hivi karibuni utajulikana
3:ukiota umefumaniwa =Unajulishwa siri inaenda kufichuka(Kujulikana).
4;Ukiota Unaujauzito na hauna mimba=Unajulishwa umefugwa tumbo lako usizae waone watumishi.
5;Ukiota umejifugua na hauna mtoto wala mimba=Unajulishwa kizazi chako kimefugwa
6:Ukiota unakimbizwa harafu ukajiona unapaa au unakuwa kama malaika= Unajulishwa Ukombozi upo kwako Utokolewa kutoka kwenye nguvu za kichawi.
7:Ukiota unapingwa kwenye ndoto=Unajulishwa umezidiwa na nguvu za wachawi wamekushinda.
8:Ukiota Unampiga mtu au unamfukuza mtu kwa fimbo=Unajulishwa umewashinda Wachawi usiku walikuja kwa sura ya mtu unayemjua.
9;Ukiota Unaendesha gari vizuri=Unajulishwa kazi yako ipo salama.
10;Ukiota Gari lako limeharibika=Unajulishwa kunatatizo kwenye kazi yako ombea kazi yako.
11:Ukiota Upo shule ya msingi na ulishamaliza=Unajulishwa Unaenda Kushindwa maendeleo kwa kukosa elimu ya unachokifanya.
12: Ukiota upo unafanya mtihani Darasani na mbele unamuona mwalimu= Unajulishwa unaenda kutana na jaribu ili kulivuka litaiji mtu mwenye ufahamu kukuzidi wewe akusaindie.
13: Ukiota unafanya mtihani =Unajulishwa utapitia pito kubwa.
14;Ukiota Jeneza la mtu unayemjua linapita =Unajulishwa omba kukataa roho ya mauti kwake usipoomba anaenda kufa mtu wa karibu yako.
15;Ukiota mtu aliyekufa unaongea naye= Unajulishwa mtu huyo alichukuliwa musukule waone watumishi wakuombee.
16:Ukiota ndoto harafu ikatokea kama ulivyoota=Unajulishwa kuwa makini na hicho kitu ulivyoota ni kweli.
17:ukiota unafunga ndoa na haujaolewa hata mchumba huna=Unajulishwa Acha kuwaza hivyo kama huwazi Unajulishwa umefugwa usiolewe au kuowa.
18:Ukiota upo kijijini ulikokulia= Unajulishwa Unafatiliwa na roho za mizimu
19;Ukiota unadumbukia kwenye Shimizu au upo kwenye =Unajulishwa kuna kesi ya uongo utazushiwa utapitia changamoto ya matatizo omba kemea.
20:Ukiota Unafanya mapenzi kwenye ndoto = Unajulishwa Umefugwa na jini mahaba
Anasababisha mahusiano kuvunjika Uchumi kuyumba Nk
HITIMISHO
Ndoto ili uweze kutafisri yaitaji ukumbuke ndoto yote na ujue mazingira ni Roho Mtakatifu pekee atakufunulia nakukujulisha Maana ya ndoto
Kila ndoto inatokea kwa sababu ya kukupa taarifa uweze kujua.
Mungu husema nasisi Sana kupitia ndoto.
WITO
Unaweza kunitumia sauti ya ndoto au ukaandika inbox hakikisha umejitambulisha unaitwa nani upo wapi kisha sasa niandikie ndoto na utume kwa WhatsApp +255759861768
Ndoto ni siri yako na anayekufasiri usipende kila mtu kumwambia.
Maoni
Chapisha Maoni