SOMO:WITO WA MUNGU
SOMO; WITO WA MUNGU
Vitabu Rejea
Kutoka;3:2-7 Yona;1;1_10
YEREMIA;1;1-10 Waefeso;4;1_6
Naitwa Bishop Richard
Nipo Morogoro Veta Dakawa
FB; Kanisa la Moto Wa Yesu
Akaunt Bishop Richard Tz
Tiktok :Moto wa Yesu
WITO Ni nini?
Ni sauti unayoisikia kufanya kazi ya Mungu.
Au Ni Sauti inayokuita nakukupa maelekezo ya kufanya au Ni Kaulitz mbiu ya Maisha Yako.
UTOFAUTI KATI YA WITO NA HUDUMA
Wito ni Sauti ya mtu kuitwa na Mungu Akaitika
HUDUMA ni Mzingo anaopewa na Mungu
Mfano; Unasikia kuchukia dhambi au kuumia watu wanavyoteseka ujue unawito wa kuwasaindia hao watu na Huduma inakuwa jinsi utakavyojitoa kuwawezesha waondokane na mateso hayo.
UTOFAUTI KATI YA MAONO NA HUDUMA
MAONO; Ni Picha Ya baadae katika HUDUMA yako
HUDUMA ni Mzingo ulioubemba au ni ujumbe uliomo ndani yako uliopewa ufikishe kwa walengwa au wahusika anaowalenga Mungu.
WITO HUZAA MAMBO MAWILI.
1:HUDUMA huzaliwa na mtu aliyeitwa na Mungu.
2;MAONO huzaliwa na mtu aliyeitwa na Mungu
JINSI HUDUMA NA MAONO YANAVYOHUSIKA KATIKA WITO
πππππππππππ
Huduma huongozwa na msingi mwema ndani yako
MSINGI YA HUDUMA
1:Neno la Mungu mwenyewe
2;Maombi Uwe mtu wa Maombi
3:MTU Aliyeitwa akaitika
4:ENEO La Kutendea Kazi Huduma yako
5.Muda sahihi wa kuanza HUDUMA yako
Maono ndiyo Muongozo mzima wa unachotaka kukifanya kifanikiwe
✍πΎMAONO Ni Picha halisi ya unachotaka kukifanya.
A. MAONO MAKUU
B.MAONO MAKUBWA
C.MAONO TEKELEZI
MAMBO MSINGI KATIKA MAONO KUYAJUA
1;Kuyajua maono yako nakusimamia mwenyewe
2;Kujua Kazi ya Maono Yako ndani yako
3.Ujifunze Jinsi ya Kuyakamilisha maono yako
4.Vizuizi kuvijua na Kuvitatua vinavyozuia maono yako
5.Kujiongeza na Kuwa na Ufahamu mkubwa wa kumiliki maono tuliyo nayo
MAMBO HAYA YANAKUJULISHA UPO SAHIHI KATIKA WITO WAKO
______________________________
1 Amani na Furaha ya moyoni
Isaya 55:12,
“Maana mtatoka kwa furaha, mtaongozwa kwa amani” katika kuujua wito wako jiulize maswali hay, Je! Hili ninalolifanya ndani yake ninapata furaha na amani au najilazimisha tu,
Filipi 4:4-7,
“Furahini katika Bwana siku zote; tena nasema furahini. Na Amani ya Mungu ipitayo akili zote itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu” katika mistali hii inaweza kukusaidia kujipima katika kila huduma unayoifanya je ni yako au ya mtu mwingine.
Unapotumika katika eneo hilo ndandi ya moyo wako kunajawa na furaha na Amani au unakuwa kawaida tu au unafanya kwa kusukumwa.
Kolosai 3:15
“Na Amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani” Je amani ya kristo ndani yako inaamua nini, Au jambo gani unapolifanya unasikia Amani katika Mungu.
Zab 16:11,
Kwenye wito wako lazima utapata furaha tele na mema
2. Kupenda na Kuridhika
Kutoka 33:12-14
Mungu anamwambia Musa “Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha” kwamba katika wito huo hutanitumikia tu bali nitakupa raha. Moyo wako hautapungukiwa katika kufurahia wito wako, huta kaa ujute.
Math 11:29-30
“Jitieni nira yangu” kuambatana na Yesu/Ukikaa katika wito wako “Nanyi mtapata raha nafsini mwenu” utapata raha. Ukiona unafanya huduma Fulani na katika hali ya kuifanyia kazi moyo wako haupokei kitu kwa Mungu jiulize Je! Huu ni wito wangu kweli au ni eneo linguine.
3. Bajeti ya Muda zaidi
Katika eneo ambalo ni wito wako utaona jinsi unavyo jishughulisha na jambo hilo kwa muda mrefu kuloko mambo mengine.
Mf. Mkulima utamjua kwa jinsi anavyojishughulisha sana na kilimo, mfugaji atajihusisha sana na ufugaji kuliko kitu kingine, hilo tu ni kiashiria cha kuonesha kuwa mtu huyo ni wa namna gani
SOMA Kut 33:7-11,
Musa sikuzote alikuwa anabeba hema la kukutania na kuhudumu watu wa Mungu, kwasababu huo ndio ulikuwa wito wake. Mungu alimuita katika eneo hilo.
Je! Wewe ni utumishi upi unaokuchukua muda mwingi?
4. Uwezo mkubwa wa Kazi hiyo
Mtu ambaye kaitwa katika eneo Fulani utaona uwezo mkubwa alionao katika kufanya jambo hilo.
Soma Kutoka 31:1-5,
Mungu anamwambia Musa “ nimemwita Bezaleli, nami nimemjaza Roho ya Mungu, katika Hekima na Maarifa, na Ujuzi na Mambo ya Kila aina. Ili abuni kazi za ustadi……….” Bezeleli alikuwa na uwezo mkubwa katika hekima, maarifa na ujuzi vitu vilivyo onesha dhahili wito wake kwa Mungu
SOMA Matendo 6:7-10.
Stefano alikuwa na uwezo mkubwa katika kufanya maajabu na ishara kubwa, hii ilionesha wazi wito wake.
Jiulize wewe una uwezo mkubwa katika kufanya NINI? Pia inawezekana ukawa na wito zaidi ya moja sio tatizo, muhimu kila wito Mungu aliouweka ndani yako uutumikie katika viwango ambavyo vinatakiwa.
5. Matokeo Mazuri
Kwenye wito huo unaotumika Je! Unapata matokeo gani? Mazuri au mabaya. Pia unaweza kukapata matokeo mabaya katika wito ambao ni wako kwasababu tu yakukosa maandalizi, kuishi maisha yasiyompendeza MUNGU nk.
SOMA Yohana 5:36,
Kazi unazozifanya na matokeo yake ndizo zikushuhudie kuwa wewe umeitiwa katika eneo gani
Marko 16:15-20,
“Na ishara hizi zitafuatana na…..” Matokeo ya mazuri ya kazi uliyoifanya ni dalili tosha ya kukujulisha wito wako.
Matendo 8:4-8.
6. Baraka na Mafanikio
Unapokuwa na wito wako Baraka na Mafanikio lazima vikufuate
SOMA Zaburi 1:3,
“Nae atakuwa kama mti uliopandwa; kando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; na kila alitendalo litafanikiwa.”
Mithali 10:22
“Baraka ya bwana hutajirisha, wala hachanganyi huzuni nayo” Katika eneo ambalo ni wito wako huwezi kuwa na huzuni bali utaambatana na Baraka tele katika wito huo.
Mith 17:8,
“Kipawa ni kitu cha thamani kwake yeye aliyenacho, kigeukapo hufanikiwa” kipawa ni wito wa mtu, anasema kila kigeukapo hufanikiwa”mtu akikifanyia kazi utafanikiwa, utapata mapokeo mazuri katika wito huo.
7. Ushuhuda mzuri wa Watu wengine
Math 18:16,
“Zawadi ya mtu humpatia nafasi, humleta mbele ya wakuu” wito wa mtu unampatia mtu nafasi/kibali katika eneo la wito wake, kwasababu watu wanaona ni eneo gani ambalo wewe unafanya vizuri.
Yoh 3:1-2,
Nikodemu alimshuhudia Yesu kuwa ni nani, Alikuwa anaona kilichopo ndani ya Yesu
Mdo 6:1-8.
Mitume alichagua watu saba watakaosimama kwa ajili ya kutoa huduma kwa wahitaji kulingana na wito wao. Wito ndani mtu hauwezi kijificha labda mtu mwenyewe asitake kutumika.
Nimeeleza kwa kifupi tu vigengele kadha vitakavyo kufanya uweze kuutambua kwa haraka wito wako kwa Mungu ili usigongane na watu wengine katika Wito wako.
HITIMISHO
Kila Aliyeokoka Anawito ndani yake nashauri simama katika wito ulipoitiwa utaona unavyofanikiwa bila kutumia hata connection
Chukua Elimu hii ibadili maisha yangu
Kwa Msaada Zaidi Wa Kiroho tuma ujumbe Whatsap Yangu Pastor Richard +255759861768
Maoni
Chapisha Maoni