SOMO; Faida ya Hekima

       SOMO: FAIDA YA HEKIMA

Hekima kwako inafaida Sana kuliko kitu chochote Unachoweza Kutenda Tengeneza maisha yako yapate nafasi kuipa hekima iamue. 

1. Itakuwezesha kujanga nyumba imara na kuwa na mahusiano imara ya kifamilia.

Mithali 24:3 Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika.

Mithali 19:13 Mwana mpumbavu ni msiba kwa babaye; Na ugomvi wa mke ni kama kutona-tona daima.

2. Itakufanya upate kibali katika yale unayoyafanya.

Mithali 14:35 Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara; Bali ghadhabu yake itakuwa juu yake aletaye aibu.

Mithali 17:2 Mtumwa atendaye kwa busara atamtawala mwama atendaye mambo ya aibu;..

3. Itakuwezesha na vikwazo na upinzani

Mithali 21:22 Mwenye hekima huupandia mji wao wenye nguvu; Na kuziangusha nguvu za tumaini lao.

Mithali 24:5 Mtu mwenye hekima ana nguvu; Naam mtu wa maarifa huongeza uwezo.

Muhubiri 9:18a Hekima ndio bora kuliko silaha za vita;

4. Itakuwezesha kufanya kazi kwa werevu na ufundi na sio nguvu.Muhubiri 10:10

Iwapo chuma hakipati, wala mtu hakinoi; Ndipo hana budi kutumia nguvu zaidi. Walakini yafaa kutumia hekima na kufanikiwa.

5. Itakuwezesha kuzima ghadhabu

Mithali 29:8 Watu wenye dharau huwasha mji moto; Bali wenye hekima hugeuzia mbali ghadhabu.

Mithali 16:14 Hasira ya mfalme ni kama wajumbe wa mauti; Lakini mtu mwenye hekima ataituliza


NAITWA Pastor Richard WhatsApp +255759861768 

Nipo Morogoro Veta Dakawa 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.