Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO;UBATIZO WA MAJI MENGI

SOMO:
;UBATIZO WA KWELI NI UPI KI-BIBLIA*
             *KATI*
               *YA*
*MAJI MENGI AU MACHACHE*❓
⛪⛪⛪⛪⛪⛪⛪⛪⛪

Biblia inasema katika *WAEBRANIA 6:1-3:-“Kwa sababu hiyo , tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikie utimilifu; tusiweke misingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na imani kwa Mungu, na wa MAFUNDISHO YA MABATIZO, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele. Na hayo tutayafanya Mungu akitujalia*”
Kama waalimu wengine wa uongo watalitumia andiko hilo kupotosha watu na kusema , suala la ubatizo halina umuhimu sana kuhangaika nalo , kikubwa wewe ukishaokoka , basi ! Haijalishi kwamba umepatiza kwa ubatizo upi maji mengi au machache. 
Watu wanaofundisha hivyo hao ni wapotoshaji wakubwa wa kweli ya neno la Mungu. Wanakudanganya hao !!
Ni muhimu kuelewa *UBATIZO NI SUALA LA LAZIMA NA LENYE UMUHIMU MKUBWA KATIKA IMANI YETU YA WOKOVU”*
Bwana Yesu mwenyewe alisema MARKO 16:16:-

*” Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”*.
Maana yake ni kwamba kama ni mtu uliyeishia kumwamini tu Bwana Yesu , lakini hujabatizwa kwa *ubatizo ulio wa kweli 

Nakuambia pamoja na kudai kwako umemwamini tu Yesu, kama usipotafuta kubatizwa kwa ubatizo ulio wa kweli kibiblia, *UTAHUKUMIWA KWENDA MOTONI*. Na utashangaa, imekuaje !!
Kwa kuonyesha ulazima na umuhimu wa kubatizwa kwa ubatizo ulio sahihi . Yesu mwenyewe alimwambia , *MATHAYO 3:13-16:-“Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitajwi kubatizwa nawe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, KUBALI HIVI SASA (KUNIBATIZA);KWA KUWA NDIVYO ITUPASAVYO KUITIMIZA HAKI YOTE. Basi akamkubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa Mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu take*
Ndugu yangu UBATIZO WA MAJI CHACHE NI UBATIZO FAKE , HAUPO KI-BIBLIA.
Ndugu yangu mpendwa ukileta kiburi na ubishi, usipokubali *kuitimiza haki yote kwa kubatizwa kwenye maji mengi kama alivyobatizwa Yesu* . Utahukumiwa kwenda Jehanamu ya moto. Sikuhukumu , ila nakwambia ukweli mtupu kabisa.
WAEBRANIA6:1-3.Kulingana na neno hilo, linatufundisha kwamba nyakati za kanisa la kwanza , moja ya mafundisho ya kwanza ya wokovu yaliyozingatiwa kufundishwa kwa watoto wachanga kiroho, ilikuwa ni suala la ubatizo.
Ikiwa mtu leo ambaye ni mkristo bado ni kama hajui , anachangakiwa kutokuelewa ubatizo upi ni sahihi wa maji mengi au machache ki-biblia!! Mkristo wa namna hiyo hata kama anajiita mwalimu, bado ni mtoto mchanga kiroho anahitaji kufundishwa.
Katika pale tuliposoma inasema *WAEBRANIA 6:3-4:-“……na wa mafundisho ya MABATIZO ….Na hayo tutayafanya Mungu akitujalia*.
Neno hilo MABATIZO , maana yake linatufundisha kuna aina nyingi za ubatizo katika Biblia .
*SWALI:-“JE! NA UBATIZO WA MAJI MACHACHE UMO KWENYE BIBLIA AU ?*
Katika utangulizi wa somo letu , labda itakuwa ni muhimu kufaham kwanza kuna aina ngapi za ubatizo uliotajwa katika Biblia nzima, neno la Mungu.
Hakuna ubatizo wa maji machache katika Biblia, Asikudanganye mtu .
Kuna aina kuu nne tu za ubatizo uliotajwa katika Biblia. Ambao ni:-
(1) UBATIZO WA MAJI

(2) UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU.

(3) UBATIZO WA MOTO
[ MATHAYO 3:11-12; UFUNUO 20:11-15 ]

(4) UBATIZO WA DHIKI NA MATESO.
[ LUKA 12:49-50; 2 WAKORINTO 4:8-17; 1 PETRO 5:10 ]

 

Wakristo tuliokoka tunabatizwa kwa aina zote za ubatizo ambao ni *1, 2, 4*.
Lakini ubatizo wa aina ya tatu *(3)*, unawahusu hasa watu wote wenye dhambi waliokataa kumkiri na kumwamini Yesu kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha, wakaokolewa.

*⛪UBATIZO WA MAJI MENGI NDIO UBATIZO SAHIHI , UTOKAO KWA MUNGU*
Ubatizo wa maji machache huo ni ubatizo wa kipagani , ambao hautokanani na Mungu aliye hai, kwa sababu haupo kwenye maelekezo ya Mungu ki-biblia.
Biblia inasema hivi katika *LUKA 20:2-6:-“Wakamwambia, wakisema, tuambie, unatenda mambo hayo kwa mamlaka gani? Tena, ni nani aliyekupa mamlaka hii ? Akajibu akawaambia, Nami nitawauliza neno moja; NIAMBIENI, UBATIZO WA YOHANA, JE! ULITOKA MBINGUNI AU KWA WANADAMU? Wakahojiana wao kwa wao, wakisema, kama tukisema ulitoka mbinguni, atasema, basi, mbona hamkumwamini? Na tukisema ulitoka kwa wanadamu watu wote watatupiga kwa mawe, kwa kuwa wamemkubali Yohana kuwa ni nabii*”
Kuna ubatizo utokao kwa Mungu na kuna ubatizo mwingine unatokana tu na mapokeo ya wanadamu wenyewe na sio Mungu.
Sasa basi, tukitaka kujua *Ubatizo wa maji mengi au machache, ni upi ulio wa kweli utokao kwa Mungu mbinguni ?*
Jibu ni rahisi tu. Tazama ubatizo wa Yonana ambao pia Yesu alibatizwa nao. Ulikuwa ni wa maji Mengi au machache ?
Ni muhimu kufahamu kuwa Yohana mbatizaji alimbatiza Yesu katika maji tele (MATHAYO 3:13-17). Yesu Kristo alibatizwa katika mto Yordani kwasababu huko kulikuwa na maji tele. Yohana mbatizaji alikuwa akibatiza sehemu zenye maji tele ili watu waweze kuzamishwa katika maji kama tutakavyoona maana ya ubatizo na kwa nini kuzamisha katika maji tele. Yohana mbatizaji hakubatiza Yordani tu, alibatiza Ainoni karibu na Salimu kwa sababu huko kulikuwa na maji tele. 

*YOHANA 3:23 “Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, KWA SABABU HUKO KULIKUWA NA MAJI TELE (MENGI), watu wakamwendea wakabatizwa”*. 
Kwa maana hiyo, kumbe tunagundua kwamba *UBATIZO WA MAJI MENGI NDIO UBATIZO WA KWELI UTOKAO MBINGUNI KWA MUNGU. Haleluya!!*
Ubatizo wa maji machache huo ni ubatizo wa kipagani tu ulioanzishwa na kanisa la Roman Catholic. Na mtu wa kwanza kubatizwa kwa kunyuniziwa maji usoni, alikuwa ni mfalme Constantino. Alipongoka na kuwa mkristo. Kwa heshima yake ya juu ya kifalme, kanisa la Roman wakaona kumbatiza mfalme kwa kumzamisha kwenye maji mengi, itaonekana kama ni tendo la kumshushia hadhi yake. Wakabuni ubatizo mpya wa kumnyunyuzia maji .
Hapo ndipo ikawa ni mwanzo rasmi wa ubatizo wa maji kidogo ulipojitokeza na kusambaa mpaka Leo hata kwenye makanisa mengi yalipokea upotofu huo.
*MARKO 7:6-8:-” Akawaambia, Isaya alitabiri vyema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, watu hawa huniheshimu kwa midomo ila mioyo yao iko mbali nami; NAO WANIABUDU BURE, WAKIFUNDISHA MAFUNDISHO YALIYO MAAGIZO WANADAMU. Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadam. Akawaambia, vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu*.
Ndivyo ilivyokuwa, Kanisa la Roman Catholic liliamua kuupotosha msingi ulio wa ubatizo wa kweli kinyume na Biblia isemavyo.
UBATIZO WA KWELI KI-BIBLIA. lazima ufanye kwenye maji tele ya kumtosha mtu kuzamishwa majini.

*⛪MAANA YA NENO KUBATIZWA AU UBATIZO*
Watu wanaotetea ubatizo wa maji machache, hawajui hata nini maana ya neno ubatizo. Na kama wanajua , basi shetani anawatumia watu kama hao kufanya upotoshaji wa makusudi kinyume na Kweli. *2 PETRO 2:1-3:-“Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale, kama vile kwenu kutakavyokuwako WAALIMU WA UONGO, WATAKAOINGIZA KWA WEREVU UZUSHI WAKUPOTEZA, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usio kawia. Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa. Na katika kutamani WATAJIPATIA FAIDA KWENU KWA MANENO YALIYOTUNGWA TU; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii*”
Ubatizo wa maji machache umetungwa tu wanadamu na sio elekezo sahihi la Mungu kwenye Biblia. Na watu wanaotetea au kufundisha ubatizo maji machache kwamba hakuna shida, ni sahihi tu.

*HAO NI WAPOTOSHAJI TU WA KWELI YA MAANDIKO. AMBAO WANALAZIMISHA KUINGIZA VYA KWAO, AMBAVYO WALA HATA HAVIKO KIBIBLIA* 
Kwa sababu Neno lenye tu ubatizo linamainisha kuwa ni maji mengi na sio machache.
Lugha za asili za biblia kabla ya tafsiri mbalambali ni kiebrania na kiyunani. Agano la kala iliandikwa kwa lugha ya kiebrania na agano jipya iliandikwa kwa kiyunani. Katika kuifasiri biblia kwa lugha zetu kuna baadhi ya maneno machache ambayo misamiati yake ilipoteza maana halisi iliyopo katika biblia. Kwasababu lugha zingine zunakuwa na mapungufu.
Katika biblia ya lugha ya kiebrania kuna neno *“BAPTIZO”* lenye maana ya UBATIZO kwa Kiswahili na kwa kiingereza BAPTIZM,
Katika biblia ya lugha ya kiyunani kuna neno *“BAPTO” lenye maana ‘kuzamisha au kuchovya”*.
Mifano katika biblia kuhusiana na neno” *BAPTO’ kuzamisha au kuchovya*.
 ( 1 ). Tonge la ugali linavyotowelewa katika ugali kisha linazamishwa lote. Tendo hilo la kuzamishwa ni kubapto *“bapto”*(kubatiza) katika kiyunani (YOHANA 13:26).

 ( 2 ). Kuchovya ncha ya kidole. Neno kuchovya hapo (LUKA 16:24) lina katika lugha ya kiyunani ni *‘BAPTO” bapto likiwa na maana kuchovya au kuzamisha*.

 ( 3 ) Tendo la kuchovya vazi katika damu lina maana ya kubapto *“ BAPTO”* kubatiza katika biblia ya ya lugha ya asili kwa kiyunani.
Kwahiyo biblia inapozungumzia juu ya ubatizo inazungumzia ubatizo wa maji tele na sio machache.
*WATU WOTE WALIOBATIZWA KATIKA BIBLIA, ILIKUWA NI MAJI MENGI TU*
(1) Nabii Yohana aliwabatiza watu wa Ainoni kwa sababu huko nako kulikuwa na maji tele (YOHANA 3:23). 

(2)Pia tunamuona mtumishi wa Mungu Filipo na towashi *wakitelemkia majini* ili abatizwe katika maji tele (MATENDO 8:34-39). Walitelemka majini akambatiza kisha wakapanda kutoka majini (MATENDO 8:36-39).

(3) Wana wa Israeli katika Agano la kale, waliotoka utumwani misri wanatajwa kuwa walibatizwa ili wawe wa musa . Na ubatizo huo ulikuwa ni wa maji mengi.
Biblia inasema katika *1WAKORINTO 10:1-2:-Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufaham ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; WOTE WAKABATIZWA wawe wa Musa KATIKA WINGU NA KATIKA BAHARI*”.
 

(4) MAJI YA UBATIZO NI KABURI. Kimsingi kubatizwa ni kuzikwa na kufufuliwa pamoja na Kristo katika ulimwengu wa roho.
*WARUMI 6:4-5:-“Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama tulivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika tutaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake*.”

*WAKOLOSAI 2:12:-“MKAZIKWA PAMOJA NAYE KATIKA UBATIZO; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu*.
Sasa basi mtu anapozikwa, maana yake anafunikizwa na udongo pande zote, anazazimishwa na kufukiwa chini ya udongo. Hakuna mtu anayezikwa kwa kunyunyuziwa udongo. 
Na kwa msingi huo, ubatizo kama tendo la ishara ya kuzikwa pamoja na Kristo, ndiomana ni *LAZIMA UFANYIKE KWA MAJI MENGI, ILI MTU AZAMISHWE kama ishara ya kuzikwa kiroho*. Na sio vinginevyo. 
Lakini Nje na hapo kwa ubatizo maji machache , tutakuwa tumedanganywa na kudanyika kwa kujifariji bure eti tumebatizwa, kumbe hamna kitu !!

*WAGALATIA 6:3:-“Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake*”.
*ACHANA NA UBATIZO WAKO HUO FAKE WA KUNYUNYUZIWA MAJI, sijui uliobatizwa nao tangu utoto*. Lakini Kubali hivi sasa, nenda kabatizwe upya kwenye maji mengi. Huu ndio ubatizo wa kweli kibiblia, utokao kwa Mungu. Amina.

*⛪ WATU WANAOFUNDISHA JUU YA UBATIZO WA KUNYUNYIZIA MAJI KICHWANI AU USONI NAO PIA WANA MAANDIKO. Ambayo watayatumia maandiko haya kwa maana isiyo kweli halisi, kwa kuyapotosha kitafsiri*.
Hoja potofu za wapotoshaji wanaojaribu kuhalalisha ubatizo wa maji machache. Watatumia maandiko yafuatayo yafuatayo:-
*EZEKIELI 36:25:- “Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafuwenu wote, na vinyago vyenu vyote”*.
*HESABU 8:5-7:- “Kisha Bwana akanena na Musa. Na kumwambia, watwae walawi na kuwaondoa kati ya wana wa Israeli, kasha uwatakase. Nawe utawafanyia mambo haya ili kuwatakasa, nyunyiza juu yao maji yatakasayo dhambi, nao wajinyoe kwa wembe mwili wote, kasha wazifue nguo zao na kujitakasa”*.    
Upotofu ni rahisi kuingia kama tutayatafsiri maandiko isivyo kama tupendavyo. (2 PETRO 1:20; 2TIMOTHEO 2;15).
Maana ya maandiko hayo yanayotumiwa kimakosa kuharalisha ubatizo wa kunyunyiza maji kichwani au usoni. *KWA SABABU WAKATI WA TORATI YA MUSA KULIKUWA HAKUNA SUALA LA UBATIZO. Desturi ya Ubatizo umeanzia rasmi wakati wa Agano jipya*.
Kwa maana hiyo hatuwezi kuyahusianisha Maandiko hayo na suala la nzima la ubatizo. kunyunyuziwa maji hapo , yana maana nyingine iliyo mbali na suala suala la ubatizo.

*TUSICHANGANYE TAFSRI YA MANDIKO, Bali tulitafsiri andiko kwa tafsiri yake iliyo halali*.
*HESABU 19:13 “Mtuawaye yote agusaye maiti ya mtualiyekufa, asijitakase, yuatia unajisi maskani ya Bwana; na mtu huyo atakatiliwa mbali na Israeli; maana, hayo MAJI YA FARAKANO hayakunyunyizwa juu yake, atakuwa najisi, unajisi wake ungali juu yake bado”*. 
Kwahiyo tunaona kuwa wakati wa agano la kale mtu aliyekuwa akiigusa maiti ya mtu aliyekufa, alihesabika kuwa amenajisika kwa kuigusa tu. Alihesabika kuwa ni mwenye dhambi (unajisi) na angeweza kulinajisi hekalu la Bwana (maskani ya Mungu). Mtu aliyenajisika alihesabika kuwa safi baada ya kunyunyiziwa kichwani maji ya utakaso yaitwayo *FARAKANO*. 
WAEBRANIA 9:10 “kwa kuwa ni sharia za jinsi ya mwili tu……..

*ZILIZOAMRIWA HATA WAKATI WA MATENGENEZO MAPYA*”
Hayo maandiko wakati wake ulishapita, maana sisi Leo tunaongozwa na Agano jipya, Agano la rohoni; Agano la kale lilikuwa na mapungufu (WAEBRANIA 8:7-9).
*LEO KATIKA AGANO JIPYA HATUITAJI TENA KUNYUZIWA HAYO MAJI ILI TUTAKASIKE*. Badala yake dhambi au uchafu unaondoka kwa damu ya Yesu kwa njia ya imani ( WAEBRANIA 12:24 ;1PETRO 1:2). Hatunyunyuziwa maji kichwani Leo kama wakati wa Agano la kale, bali *damu ya Yesu Kristo Leo ndiyo inayonyunyizwa juu yetu na kuondoa dhambi*
Tendo la kunyunyuziwa damu ya Yesu ndilo linaitwa kuzaliwa kwa kwa roho au kuzaliwa Mara ya pili ( YOHANA 3:3-10). Mtu asipozaliwa Mara ya pili, hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu ( YOHANA 3:5; 1:12). Maji yanayotajwa katika Yohana 3:-3-10, *Ni neno la Mungu*, siyo ubatizo wa maji kama waalimu wengine wanavyopotosha. Neno la Mungu linamsafisha mtu kama vile maji yasafishavyo (YOHANA 15: 3; 1PETRO 1:23).

*ITAENDELEA SEHEMU YA PILI…..

*INAENDELEA SEHEMU YA PILI……..*

Wapotoshaji hawa watalitumia tena hili andiko kujaribu kuhalalisha ubatizo wao wa maji machache.
Watanukuu katika *MATENDO 9:17-18:-” Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia ulioijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu. Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, AKASIMAMA, AKABATIZWA*”.

Watasema Paulo mtume alikuwa ndani ya nyumba hapo, akasimama akabatizwa. Kwahiyo watafikiri hapo kulikuwa na ubatizo wa maji machache. Jambo ambalo siyo sahihi.
MATENDO 9:18, Biblia zetu za kiswahili zinasemama akasimama , akabatizwa lakini hazielewei vzuri kitafsiri.
Tafsiri nzuri ya mstari huo tunaipata katika Biblia ya kingereza ya King James vision, *ACTS 9:18;-“Immediately there fell from his eyes something like scales, and he received his sight at once; And HE AROSE AND WAS BAPTIZED**.
MATENDO 10:20:-” Basi ondoka ushuke ufuatene nao….. *( Arise therefore, go down and go with them….)*
Kwahiyo hapo Paulo mtume alioondoka (mahali hapo ndani ya nyumbani) na kwenda kubatizwa. Na ubatizo alibatizwa nao huko, ulikuwa ni maji mengi.

*🔷JE, ASKARI WA GEREZANI NA WATU WA NYUMBANI MWAKE WALIBATIZWA KWA MAJI MENGI ?*
[ MATENDO 16:30-34] 
 *Jibu ni Ndiyo*.
Bila shaka watumishi hawa waliwapeleka mahali penye maji mengi kwa wakati huo na kuwabatiza kwa kuwazamisha ili washiriki mauti ya Yesu kwa kuzikwa na kufufuka kwake

( WAKOLOSAI 2:12; WARUMI 6:4).

*🔷 JE UBATIZO , WA NYUMBA YOTE UNAOTAJWA KATIKA BIBLIA SI PAMOJA NA WATOTO WADOGO ?*
[ MATENDO 18:8; MATENDO 16:31-33].
*Jibu ni Hapana*.
Ni muhimu kufaham katika tamuduni za wakati wa Biblia, watoto wadogo hawakuruhusiwa kuwepo eneo lenye watu wazima, ndiyo maana wanafunzi wa Yesu waliwafukuza (KUMBUKUMBU 3:5-6). Hata katika hesabu za watu watoto hawakuhusishwa katika hesabu ( 1SANWELI 22:19; EZRA 10:1; YEREMIA 40:7). Watoto hawakubatizwa katika familia zao (1 KORINTO 1:10-11; MATENDO 10:1-2), mtoto Mdogo/mchanga hawezi kumcha Mungu, hivyo Biblia inaposema nyumba nzima wakabatizwa, *ina maana ya watu wazima*.

*⛪ UBATIZO HAUFANYWI KWA WATOTO WADOGO/ WACHANGA*
Kwa kawaida katika makanisa hayo, watoto wadogo wanapobatizwa eti huwa anakuwepo mtu mzima anayempakata na kujibu maswali badala ya mtoto huyo. *Hiyo siyo sahihi kibiblia*
*EZEKILI 18:20:-” Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; MWANA HATAUCHUKUA UOVU WA BABAYE, WALA BABA HATAUCHUKUA UOVU WA MWANAWE; haki ya mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake*”.
Tena Biblia inasema

*Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe ( WAGALATIA 6:5)*.
Kwa. Msingi huo , mtu hawezi kutubu dhambi kwa niaba ya mtu mwingine.
Ni muhimu kufaham kuwa watoto wadogo ufalme wa mbingu ni wao hata bila ya kutubu dhambi (MARKO 10:13-14). Sisi sote tumezaliwa tukiwa na asili ya dhambi. Tumezaliwa kwa mfano wa Adamu na si kwa mfano wa Mungu ( ZABURI 51:5; 58:3). Pasipo sheria hakuna dhambi, dhambi inahesabiwa kwa sheria (WARUMI 4:15; 5:12-13).
Mtoto Mdogo anaweza kutenda dhambi kama vile kusema uongo, kucheza dansi, kuzira, uchoyo n.k. Lakini watoto wadogo hawahesabiwi dhambi, kwa kuwa hawajui vizuri mema na mabaya. Watoto wadogo hawana uwezo wa Kujua kupambanua au kutofautisha mema na mabaya. Wanafanya bila Kujua ni dhambi, ndiomaana Yesu alisema ufalme wa mbinguni ni wao.

*WAEBRANIA 5:13-13-14*. Mwenye uwezo wa kupambanua mema na mabaya ni mtu mzima *ndiyo mwenye sifa ya kubatizwa*; lakini mtoto Mdogo hata kama akifa anakwenda mbinguni moja kwa moja bila kizuizi chochote.

*🔷 Kabla ya kubatizwa sharti mtu huyo atubu dhambi zake zote kwa kumwamini Yesu baada ya kuhubiriwa au kufundishwa*
Ili mtu awe na sifa ya kubatizwa kibiblia lazima atubu dhambi zake kwanza kwa kumwamini kwa moyo wake, Mwana wa Mungu Yesu Kristo.
BIBLIA INASEMA katika
*MATENDO 2:37-38, 41:-Waliposikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akamwambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA kwa jina la Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu*
*Nao waliolipokea lile neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu elfu tatu*”.

*MATENDO 8:12-13;-” Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, WAKABATIZWA, WANAUME NA WANAWAKE. Na yeye simoni mwenyewe ALIAMINI AKABATIZWA, akashikamana na filipo: akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa iliyotendeka*”.

*MARKO 16:15-16:-” Akawaambia, Enendeni ulimwenguni kote, mkahubiri injili kwa kila kiumbe. AAMINIYE NA KUBATIZWA ATAOKOKA; asiyeamini atahukumiwa*”.
Pia katika MATENDO 8:35-38, Towashi aliamini kwanza kabla ya kubatizwa na Filipo. Mtu baada ya kujifunza neno la Mungu na kuliamini kwa moyo wake wote na kusafishwa kwa damu ya Yesu kwa njia ya imani, baada ya kutubu kwake; ndipo aweza kubatizwa.

( MATENDO 16:31-33; MATENDO 18:8).
Sasa basi kwa mtu ambaye ni mtoto sana Mdogo/mchanga hawezi akahubiriwa, akaamini na kutubu, kisha akaokolewa. Kwa maana hiyo mtoto mdogo asiyejua kupambanua mema na mabaya, HANA SIFA YA KUBATIZWA KI-BIBLIA.

*⛪ WATOTO WADOGO WANABARIKIWA TU, HAWABATIZWI*.
Biblia inasema katika MARKO 10:13-16;-” Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea. Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. Amin, nawaambieni, Ye yoyote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa. *AKAWAKUMBATIA, AKAWEKA MIKONO JUU YAO , AKAWABARIKIA*”.
Yesu mwenyewe alilokuwa mtoto mdogo, alibarikiwa tu, hakubatizwa. *Simeoni akawabariki*(LUKA 2:27-34).
Yesu alibatizwa katika maji tele alipokuwa mtu mzima (LUKA 3:21-23; MATHAYO 3:13-17). Ametuachia kielelezo; tufuate nyayo zake ili MUNGU apendezwe nasi. 
Ubatizo wa kweli kibiblia ni wa maji mengi tena kwa watu wazima, na sio watoto wadogo.
Biblia inasema katika
*WAEBRANIA 12:2:-” TUKIMTAZAMA YESU, mwenye kuanzisha na mwenye kuitimiza imani yetu……..*”.

*1 YOHANA 2:6*:-” Yeye asemaje ya kuwa anakaa ndani yake,

*IMEMPASA MWENYEWE KUENENDA VILE VILE KAMA YEYE (YESU) ALIVYOENENDA*”.
(1) Je, Yesu alibatizwa kwenye maji mengj au machache ❓

(2) Yesu alibatizwa akiwamtoto mdogo au mtu mzima ❓
Kama kweli tunataka kwenda mbinguni ni muhimu tumtazme Yesu na kuenenda sisi wenyewe vilevile kama Yesu alivyoenenda. *TUBATIZWE NA SISI KWENYE MAJI MENGIIIII*!! Maana Yesu alituachia kielelezo ili tufuate nyayo zake (1 PETRO 2:21).

 MUNGU AWABARIKI wote kwa ujumbe wa neno hili.

🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺
Mtumishi wa Mungu aliye hai,
*MWL:- ODRICK BRYSON* 
(0759 386 988; 0717 591 466).
Whatsap.

*KWELI YOTE YA NENO LA MUNGU ISIYOGOSHIWA*

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.