SOMO:MAMBO YANAYOLETA NDOA YENYE AMANI NA FURAHA
MAMBO 5 YANAYOWEZA KULETA NDOA YENYE AMANI.
Habarini Wadau na Wasomaji wa nakala za Wanandoa Tuongee+18 Ninataka niongelee Jambo la mhimu kwako wewe ambaye upo kwenye mahusiano au ndoa inawezekana unapitia machozi kwenye mahusiano kwa kuwa hukuwahi kusikia Mahusiano au uchumba ndio hujenga msingi mwema wa ndoa njema ukikosea ni kazi kurekebisha ukiwa kwenye ndoa
Naitwa Mwalimu wa Wanandoa Pastor Richard nakualika.
MAMBO HAYA UYAFANYE KABLA YA KUINGIA NDOA.
👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆
1:MAHUSIANO YASIYOELEWEKA NI BORA UYAVUNJE KULIKO KUINGIA KWENYE NDOA ITAKAYOKULIZA MILELE.
Ukiona unatumia nguvu nyigi kulazimisha upendo au unaumizwa na kusalitiwa mara kwa mara halafu unamurudia yule yule anayekuumiza mkiwa kwenye steji ya uchumba ujue unajulishwa huyo mtu kwenye ndoa mtasumbuana tu.
●●●●●●●●●●●●●●
2.UTAKAVYOPATIA KUCHANGUA NDIVYO UTAKAVYOPATIA KUJENGA NDOA YENYE AMANI NA FURAHA.
Unajua kuna mahusiano watu wanaanzisha wakiwa hawana malengo yoyote ghafla wanapeana mimba wanachukuana wanaanza kukaa wote mara nyigi watu walioingia ndoa za mfumo huu huwa watu waliokosea walioana kwa sababu ya kitu sio watengeneze maisha ya ndoa. JIFUNZE KUKOSEA KUOA AU KUOLEWA NI KUKOSEA MAISHA YAKO YOTE.
👉👉👉👉👉👉👉👉👉👉
3.MBADILISHE TABIA MWENZA WAKO NA KUMFUNDISHA UNAVYOTAKA AWE KABLA HUJAINGIA NAYE KWENYE NDOA.
Ukiona mtu upo naye kwenye ndoa anaendelea kufanya aliyokuwa anayafanya kabla ya hamujaoana Ujue ulishindwa kumwambia na kumrekebisha mkiwa bado hamjaoana kwa hiyo tabia hiyo hawezi kuiacha akiwa tayari amekuowa kwa hiyo anza kumtengeneza mmeo au mkeo Awe mke mwema kabla ya ndoa.
👉👉👉👉👉👉👉👉👉👉👉
4.USIJIRAHISISHE KWENYE MAHUSIANO AU KULAZIMISHA PALE USIPOPENDWA.
Kuna wakati mtu anaweza kupenda pale usipopendwa na ukajikuta unakuwa Mtu wa kulazimisha mtu ambaye hakupendi hii huwa mbaya kwako utajikuta unaamua ufanye vitu kwa ajili yake kuifurahisha nafsi yake mfano utamzalia, utazini nae ,utamsomesha, lakini mwisho wa siku atakuacha tu kwa kuwa umejirahisisha kwake.
●●●●●●●
5.NDOA NZURI HUONEKANA KWENYE UCHUMBA NA NDOA MBAYA HUONEKANA KWENYE UCHUMBA WENU.
Uchumba wenu ulivyo kama ni wakuvutana hamshirikishani hakumbukani au mnafanya kila mmoja anavyojisikia ujue ndivyo ilivyo hata ndoa yenu.
Anza sasa kutengeneza ulipongudua umekosea siyo kuendelea Kukosea
Kwa ushauri wa kiroho na mwili
Mfate WhatsApp Pastor Richard +255759861768
Yupo Morogoro Veta Dakawa
HITIMISHO
Tumalize kwa kusema mwenye kuyajenga mahusiano yakawa manzuri ni wewe mwenye kuyambomoa mahusiano yako yakawa mabaya ni wewe pia.
Ni heri kujifunza kosa nakulitatua kosa.
Wito
Nisaindie kushare kwenye magroup mbalimbali
Tusome. Mithali;12;1_5 :13;1-5
Maoni
Chapisha Maoni