SOMO:CHANZO CHA MATATIZO YAKO

SOMO: CHANZO CHA MATATIZO YAKO.
Nawakaribisha katika Nakala hii Ambayo itakufanya ujue ukweli wa matatizo yako yanasababishwa na nini nawewe Utaweza Kutengeneza kama utaitaji kupona lakini kama utaitaji kuagamia hutaweza kutengeneza na Mungu. Sasa nakuarika utenge sikio lako ujifunze Neno la Mungu na Pastor Richard  Huyu mtumishi yupo Morogoro Veta Dakawa 
Mfate WhatsApp Yake +255759861768


MAANA YA CHANZO CHA MATATIZO Ni Kitu ngani kinalifanya Tatizo ndani yako lipate nguvu mzizi wake ni nini?

Ukitaka Kupona tatizo lolote lile Tafuta chanzo usitafute tatizo. 

KUNA MAMBO MATATU YAKUZIGATIA NA NDIYO YANASABABISHA UPITIE MATATIZO UKINIELEWA SOMO HILI UMEPONA.

A;MATOKEO YA DHAMBI 
Vitabu rejea: Mwanzo:4:7 Mhubiri.8;12
Yeremia;14:20,Mithali:17;19 Matendo;3;19
Neno linasema hivi;
Mwanzo 13:13
[13]Lakini watu wa Sodoma walikuwa wabaya, wenye kufanya dhambi nyingi sana juu ya BWANA. 

Dhambi utafurahia unapoifanya kama hauna hofu ndani yako ya kiungu Na utajipa moyo hakuna aliyemkamilifu au hakuna asiyetenda dhambi Mimi ni malaika sawa  Je,Unajua matokeo yake baada ya hiyo dhambi.
Nitatolea matokeo ya dhambi tatu tu.

1:Dhambi ya Kuzini au Kuishi maisha ya kuzini 
a)hautaolewa au kuowa kwa sababu unamiuganiko ya wanaume  wengi wanawake wengi ipo roho itazuia ndoa itaruhusu uwe mtu wa maisha ya kuzini.

b)Utaitwa Malaya utaitwa lango la Takayama za kinamna zinazotupwa huko utaitwa majina mabaya na utakuwa usiyeheshimika.

c)Utakosa Baraka za Mungu utapata laana nyingi Sana kupitia tendo la kuzini.

d)Utaishi maisha magumu yaliyokosa ushuhuda mzuri mbele za jamii hata wazazi.

e)Utawaongopa wachungaji utakuwa mtu wa kukwepa wachungaji na kanisani utaanza kupunguza mahudhurio na utaacha.

Haya Yote Unayapitia baada ya kuishi katika dhambi ya kuzini matokeo utakayoyapitia maisha yako kulaaniwa na kuishi maisha ya kutapatapa Hutakuwa mwenye kuheshimiwa.

2 Dhambi Ya Wizi Wa Zaka
Matokeo yanayokupata baada ya kuitwa mwizi au jambazi zoefu la fungu la kumi utapatwa na haya 
a)Uchumi wako utayumba sana kuja kuurejesha itakuwa mpaka usimame kweli na fungu la kumi kutoa Utapata pesa lakini zitaisha bila kufanya la maana utakuwa usiyetumia pesa yako utadhurumiwa nk.

b)AFYA YAKO Itavamiwa na magonjwa,mikosi,kupata ajali nk kwa kuwa ulikuwa mwizi wa zaka
c)FAMILIA Hapa namanisha utaowa mtu siyo sahihi utaolewa na mtu ambaye siyo sahihi utateseka kuowa na kuolewa utateseka na uzazi na mambo yote yanayohusu familia. 

Haya yatakupata unapokuwa mwizi wa fungu la kumi 
Fungu la kumi kama huna kazi unalitoa hivi nenda kanisani unasafisha kanisa kamsaindie mchungaji kupokea wageni kusafisha makazi yake jiwekee kila wiki.
Usitoe kwa kurukaruka kuwa mwaminifu kila mwezi
B;MATOKEO YA UCHANGUZI WETU.
Mwanzo 6:2
[2]wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. 

Pia Jambo la uchanguzi katika kuowa au kuagalia aina ya mwanamke sura yake au mwanaume sura hii huwafanya watu wengi waishi na watu watakaowatesa mioyo yao.

a)uchanguzi katika mahusiano kutakufanya uteseke sana 

b)Uchanguzi katika kazi hutaki kujishughulisha kisa umekosa ulichosomea kitakufanya uteseke sana.

c)Uchanguzi wa Madhabahu Unatazama nebo ya kanisa lako ukikosa nebo hiyo huendi Kanisani kutakufanya uteseke utakuja kwenda sehemu usikute dhehebu lako yapo ya aina hiyo mengine wewe si utakufa kiroho.

d)Uchanguzi wa maisha ukikosea msingi wa maisha yako ukiwa bando kijana uzeeni utasumbua watu wewe.

Sasa Kama unateseka kwa katabia kakuchangua badilika utateseka mpaka lini ondoka kwenye maisha hayo.

C)MATOKEO YA KUPIMA VIWANGO VYA IMANI ZETU.
Tusome
Yakobo 1:12-14
[12]Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao. 

[13]Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. 

[14]Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. 

Mungu huwa amjaribu mtu isipokuwa sisi katika tamaa zetu tunaingia kutamani kufanya mambo yaliyo nje.

Mambo ambayo Mungu Huzingatia Anapokupitisha kwenye wakati mgumu.

1:Kupima kiwango chako chakustahimili vipindi vingumu.
2;Hutupitisha katika kipindi kingumu ili kutupa ushuhuda wa kuwashuhudia wengine.
3.Hujipatia utukufu tunapovumilia na kuvuka katika kipindi kingumu.
4.Huangalia na Kutenganisha kilicho dhaifu na change nguvu kupitia kipimo cha majaribu
5.Huwajua waliowake kwa kuwa huwa hawaachi kutoa zaka kwa sababu ya wakati waoupitia hawaachi ibadani hawaachi kumpenda Mungu.

CHAKUFANYA
Jifunze kutatua matatizo kwa kuliewa somo hili usiweke imani yako kila kitu umelongwa wewe mwenyewe unaweza kuruhusu uponyaji endapo utajua chanzo cha tatizo lako nini.?

         HITIMISHO 
Tafakari ujiulize wewe matatizo yako unayoyapitia ni matokeo ya nini? Je, Unachukua hatua zipi sasa baada ya kuwa umejifunza Chanzo cha matatizo yako?
Unamuahindi nini Mungu kupitia Somo hili?
         WITO
Chukua muda huu kuwashirikisha watu wengi Sana na uwe balonzi unayejali wengine Share Somo hili mara nyigi zaidi.
Huduma hii inalenga kukuponya na kukufungua kupitia Mafundisho ya neno la Mungu kama unateseka mfate WhatsApp Pastor Richard +255759861768 Atakupa maelekezo uende Ukachukue majibu Yako Haombei kwenye Simu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.