SOMO;Uchumi na Kijana

SOMO;Uchumi na Kijana
Maana ya Uchumi,
Uchumi huweza kuelezewa kama jumla ya shughuli zote za binadamu zinazolenga kutosheleza mahitaji yao, huhusisha uzalishaji, usambazi, na utumiaji wa bidhaa, ikiwa ni pamoja na kutolewa kwa ajili ya huduma mbali mbali, uchumi mara nyingi hutazamwa kwenye ngazi za kijiji, jumuiya, mkoa, taifa au Dunia kwa ujumla.
Uchumi ndio hutafsiri uwezo wa kumudu mahitaji.

Teknolojia pamoja na utandawazi
Teknolojia, ni kukua kwa sayansi ya uzalishaji katika Nyanja mbali mbali ka ma vile, kiuchumi, kisiasa, na kijamii,
na utandawazi ni uongezekaji na muunganiko wa kiutendaji katika Nyanja mbali mbali kama vile kisiasa, kijamii, na kiuchumi, mara nyingi teknolojia ndiyo huzaa na kuieneza utandawazi.

2. MATABAKA YA KIUCHUMI DUNIANI
Ni ukweli uliodhahiri kuwa utofauti wa kiuchumi katika nchi zetu, ndio unaopelekea hata uchumi wa watu wake wanaoishi humo, Kutokana na utofauti wa uchumi na mafanikio ya nchi zilizopo duniani, Dunia imejikuta katika matabaka ambayo yamekuwa ni vigumu kuepukika, ambayo ni kama;

Nchi za daraja la kwanza (First world countries)
Hizi nchi ni za dunia daraja la kwanza, ni nchi zilizokwisha kuendelea ambazo wao ndio wazalishaji wakubwa wa bidhaa na waanzilishi wakubwa wa mambo mbali mbali, ni mataifa yanayomiliki viwanda vikubwa na yanaendesha | yanafadhiri mashirika yenye nguvu Duniani, mataifa haya hujiendesha kwa misimamo na mawazo yao wenyewe na teknolojia zao wanazitengeneza na kuanzisha wao wenyewe, huwa sio wategemezi katika kufanya mambo wala wategemezi kimawazo kutokea nchi ambazo zipo chini kiuchumi, mataifa haya pia ndiyo hulenga kuendelea kuyafanya mataifa yanayoendelea kuwa tegemezi wa kimawazo, misimamo na kiteknolojia kwao. miongoni mwa nchi hizi ni kama Marekani(U.S.A), China, Urusi, Uingereza, Hispania, Ujerumani n.k

Nchi daraja la pili (Second world countries)
Hizi ni nchi ambazo bado znaendelea, hazijafikia maendeleo ya nchi za daraja la kwanza, lakini pia hazilingani na nchi za daraja la mwisho, hizi ni nchi ambazo zenyewe zna uwezo wa kujiongoza zenyewe, kwa sera na mawazo ya watu wake, ni nchi ambazo huwa na viwanda vikubwa vya wastani vyenye uwezo wa kawaida tofauti na vile vya nchi za daraja la kwanza, japo huwa ni tegemezi katika maswala ya kiteknolojia mpya na mawazo kutoka nchi zilizokwisha kuendelea, lakini hizi ni nchi zenye watu(vijana) wanaojaribu kutengeneza mawazo yao ili nchi hizi ziweze kujiendesha bila kuwa tegemezi kutoka mataifa ya daraja la kwanza. Mfano Tanzania, uturuki, Poland, India, nk

Nchi daraja la tatu (Third world countries)
Hizi ni nchi za daraja la mwisho, hizi ni nchi ambazo znaendelea na bado ziko chini katika kila Nyanja, nchi hizi ni tegemezi katika kila kitu, ni nchi zenye viwanda vidogo visivyokidhi mahitaji ya watu wake, na hivyo nchi hii hutegemea bidhaa zakuingizwa kutoka nje katika nchi za daraja la kwanza na la pili, hizi ni nchi ambazo hufuata mawazo na misimamo ya mataifa ya daraja la kwanza na la pili, nchi hizi nyingi hutokea baani Afrika na chache Asia, mara nyingi nchi hizi znakumbwa na madeni kutoka mataifa makubwa, pamoja na taasisi znazofadhiliwa na mataifa makubwa miongoni mwa nchi hizi ni Burundi, Malawi, Uganda n.k

3. MAENDELEO YA TEKNOLOJIA DUNIANI
Hivi sasa ni tupo katika kipindi ambacho dunia inapitia teknolojia kubwa na za kisasa, matumizi ya smu janja(smartphones), matumizi ya roboti viwandani(robotics), kuenea kwa mitandao ya kijamii, internet za kasi kama 3G na 4G, zmerahisha sana dunia katika kusafirisha habari, ikiwa ni pamoja na utendaji kazi katika Nyanja mbali mbali, lakini pia kushirikishana katika fursa mbali mbali ambazo zmeibuka kutokana na teknolojia kukua.
Maendelao ya Teknolojia yameibua mawazo na fursa, pamoja na michezo mbali mbali ambazo, pamoja na changamoto za kibiashara kama zilivobioashara zingine, hizi pia zmeweza kuajiri vijana wengi ulimwenguni, teknolojia hizo ni pamoja na…

Teknolojia ya mifumo ya kubadisha pesa za kimtandao (Block Chain Technology)
Hii ni mifumo ambayo huwawezesha watumiaji wake kuweza kutuma au kutoa hela, na pia kununua na kuuza sarafu(coin) za kimtandao mfano wa coin hizo ni bitcoin na etherium.

Kununua, na kuuza Sarafu za kimtandao (Crypto Currency Trading)
Hii huhusisha ununuji wa sarafu inapokuwa imeshuka kwenye mzunguko, na kisha kuiuza wakati itakapopanda

Biashara za mtandaoni (Online Networking and marketing bussiness)
Hizi ni mifumo ambazo huanzishwa na makampuni na hutumia watu kuwekeza hela zao, ambapo baadae hurudishiwa hela zao walizowekeza pamoja na faida ya uwekezaji, makampuni haya hujihusisha pia utengenezaji wa mtandao wa watu ambapo watu hulipwa kama wakiwaalika na kuwasajili wenzao.

Kubeti (gambling | Sports betting)
Hii ni michezo inayohusisha kubashiri matokeo ya michezo mbali mbali kama mpira wa miguu, mpira wa kikapu, nk, ambapo watu hupata pesa kama matokeo ya michezo yakiwa sawa sawa na bashiri zao.

Televisheni za mtandaoni (online TV)
Hizi ni televisheni(TV) ambazo znaanzishwa mtandaoni, kwa malengo mbali mbali kama kuburudisha, kufundisha, au kuhabarisha, watu huweza kupata pesa kwa mikataba ya kurusha matangazo kupitia televisheni hizo, na pia hulipwa na mitandao kama youtube kwa kuwa na watazamaji na wafuatiliaji wengi.

Ufundishaji kwa njia ya mtandao (online learning)
Hizi pia ni njia za kujiajiri ambapo watu hutengeneza platforms za kujifunzia mtandaoni, na hivyo hulipwa kwa kufundisha watu wahitaji wa elimu au maarifa anayoitoa.

Urushaji wa matangazo ya kibiashara mtandaoni (online branding)
Hii nayo ni njia ambayo vijana wanaweza kujiajiri kwa kufungua blogs au websites, na wakawa wanalipwa kila wanapotuma matangazo ya mashirika mbali mbali ambayo wameingia nayo mikataba ya kuitangaza.

NB: Hizo ni fursa mbali mbali ambazo sasa teknolojia imerahisisha Zaidi, Katika kuchagua fursa na biashara hizi ni vyema mhusika aamue kufuatilia changamoto za kila moja pamoja na risk za kila biashara,

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.