SOMO;MWILI WENYE PUMZI HAI
SOMO: MWILI WENYE PUMZI HAI.
VITABU;Mwanzo;2:7,6:17,7:15-30
Ezekieli;37:5-12
●UTANGULIZI;●
Mwili Wenye Pumzi Hai ndio mwili ulio hai hivyohivyo Katika maisha yako Ya Kiroho na Mungu Unaweza Ukawa Umembeba Yesu Aliye hai ndani yako lakini Wewe ulimbeba ukawa Umekufa kiroho unajikuta hata kuiona Faida Ya Uliye Naye Huwezi Kuiona Unajikuta Umekufa Lakini Unatembea Nafsi Yako Imekufa Tayari.
Karibuni Katika Somo Hili.
TUOMBE;
Baba Naachilia Ufahamu na Uelewa Kwa Watoto wako wakaelewe Ninapofundisha Somo hili Ukaachilie Pumzi Kwa Mtu aliyekufa akawe hai katika jina la Yesu. Amen
PUMZI HAI NINI ?
Ni nguvu inayopewa kitu Kilichokufa au Sanamu iweze kujiendesha nakusimama kuongea nakujitambua.
MAANA YA NENO PUMZI HAI.
Nikufufua kitu kilichokufa.
KUNA VIASHILIA AU DALILI UNATAKIWA UZIJUE ILI KUJIELEWA UNAHAI NDANI YAKO AU ULISHAKUFA ZAMANI.
1:Uhai wa Milango Yako Ya Ufahamu
Ambayo kutokana Na Jinsi Unavyoweza
Kujitambua na Kuelewa Kuchukua maamuzi.
Maana kama milango ya ufahamu umekufa.
Hutojitambua,Hutakuwa na Maamuzi Yoyote.
Marko;13;29 Mwanzo:2:7
UFANYE NINI KAMA MILANGO YA Ufahamu IMEKUFA.
Lazima uchukue hatua Utafute Neno la Mungu ufundishwe Ili milango ya ufahamu ifunguke bila Mafundisho Utaendelea Kutembea na Kuishi ukiwa Huna Pumzi hai kwa hiyo lazima ufanye mambo yanayokufakufa Tu. Ukiwa hai utafanya mambo yaonekane hai.
2:Uhai Wa Mifupa Yako
Unaweza ukawa unatembea mifupa yako umekufa maana mifupa ikiwa hai na mwili hutaona unalalamika matatizo.
Ezekieli aliambiwa Tabiria mifupa
Watu waliokufa mifupa yao ikabaki inatapakaa tu. SOMA;EZEKIEL;37;5-15
3:Uhai wa Mtu mwenyewe.
Hapa ni mienendo na matendo yako yanakujulisha wewe upo hai au umekufa.
Mfano: Unaenda Kanisani na mimba unatoa, Unakaa na mwanaume asiyetambulika, unaenda kwa waganga,Ukiambiwa uombe hutaki,Usafi Kanisani ukipangwa hendo, Umeamua Usiende kanisani eti kisa Mungu amechelewa kujibu,Zaka hutoi,Sadaka ya kawaida hutoi,Yaani Unakuwa mtu huwezi kuomba mwenyewe mtu wa kukata tamaa.
Wewe Ujue Umekufa Mtu mzima unatembea Lakini Nafsi yako haina Pumzi Ya uhai.
Unajua Adamu alipoumbwa kabla hajapuliziwa Pumzi alikuwa Sanamu lakini Baada Ya Kupuliziwa Pumzi akawa hai anaweza kutawala Wanyama,Samaki ,nk
Chochote Kilichokufa hakiwezi Kukitawala kilicho hai. Inaamana Dalili Kuku zinazokujulisha umekufa.
1;Kila utakachofanya Kinakufa
2:Hutasimamisha hata nyumba ya chumba kimoja.
3:Mawazo na Mipango Yako inakufakufa Tu
4;Unakuwa Huombi Hutoi zaka kanisani hupendi Biblia husomi nk.
5;Kila Kitu Kitakutawala Hadi nguo utapewa hadi chumvi hutainunua
Uonapo Dalili Hizi Nenda Kwa Watumishi Wenye Karama ya ualimu wakufundishe Neno ujue wewe huhitaji uombewe.
Ulemavu wa Kanisa la Leo Linapenda Kuombewa ombewa kataa roho ya kuwa mtu uliyekufa Tamani uwe mtu uliye hai.
HITIMISHO
Tunatakiwa Tulitafute Neno la Mungu kwa Wingi ili Tupate Mwangaza na Nuru katika maisha Yetu.
WITO
Hebu Sambaza Somo hili Kwa Magroup Yako.
Kwa Msaada Unayetamani Uokoke Nipigie +255759861768 Jioni Saa 12;00 nakuendelea
Naitwa Pastor Richard
NIPO MOROGORO VETA DAKAWA
Maoni
Chapisha Maoni