SOMO; MAFANIKIO KUPITIA PESA ZETU

SOMO;MAFANIKIO KUPITIA PESA ZETU KIBIBLIA

Kutumia vyema fedha ambazo Mungu ametupa ni changamoto kubwa katika maisha. Kumbuka kuwa tutatoa hesabu ya vile ambavyo Mungu ameviweka mikononi mwetu. Ni jukumu letu kufanikisha maisha yetu kwa zile fedha ambazo Mungu ametupa, kila mkristo ni lazima ahakikishe anafanikiwa katika suala la uchumi kwa utukufu wa Mungu.

Kuna mambo matatu inabidi tuelewe

  1. Fedha ni muhimu katika maisha yetu
  2. Mipango ya matumizi ya fedha ni muhimu kuliko fedha zenyewe
  3. Dhamira na nia yako ya kutumia vizuri fedha zako ni muhimu zaidi katika uwakili wako Sahihi 

Mafanikio yanakuja unapokuwa na mtazamo sahihi

1.Jitoe kikamilifu kwa Mungu

Mungu alimbariki Abraham kwa sababu alijitoa kikamilifu kwa Mungu, akaacha nchi  yake na kwenda kule Mungu alipomwambia aende bila kujua aendako. Mwanzo 13:12-18.

Ebrania 11:8-10  8Kwa imani Abrahamu alimtii Mungu alipoitwa aende kwenye nchi ambayo Mungu angempa kama urithi. Naye aliondoka akaenda ingawa hakujua aendako. 9Kwa imani aliishi kama mgeni katika nchi ya ahadi. Aliishi katika nchi ya ugenini katika mahema pamoja na Isaki na Yakobo ambao pia walikuwa warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. 10Maana alikuwa akitazamia mji wenye misingi ya kudumu ambao umebuniwa na kujengwa na Mungu mwenyewe

Mafanikio yanapatikana katika kujitoa miili na nafsi zetu kwa Mungu, pale tunapotambua kuwa tunaishi kwa ajili yake na yatupasa kwanza kuyafuata mapenzi ya Mungu katika kila sehemu ya maisha yetu.

Warumi 6:13 13Msikubali kutoa sehemu yoyote ya miili yenu itumike kama vyombo vya uovu kutenda dhambi. Bali jitoeni kwa Mungu kama watu waliotolewa kutoka katika kifo wakaingizwa uzimani. Pia toeni sehemu zote za miili yenu zitumike kama vyombo vya haki.

2. Kabili majukumu yako na wajibu wako

Fanya kazi yako kwa uaminifu na kwa kuijali. Mungu amekupatia kazi / biashara ili uweze kujipatia kipato, yakupasa kuifanya kwa moyo wako wote na uwezo wako wote.

1Kor 10:31-32 31Basi, lolote mfanyalo, kama ni kula au ni kunywa, fanyeni mambo yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu. 32Msiwe ki wazo kwa Wayahudi au kwa Wagiriki, au kwa kanisa la Mungu

Vile vile lazima uwe makini katika matumizi yako ya fedha. Huwezi kufanikiwa kama kile kidogo ulichionacho hukitumii kwa busara na kwa kuwajibika..

Mithali 10:4

Mithali 22:29

Mafanikio huja unapofunguka toka kwenye makosa ya kiuchumi

1.Kutokuwa na maana sahihi ya kuweka akiba

Huwezi kuiita akiba kama fedha hizo ni kwa ajili ya matumizi ya wakati huu. Fedha iliyohifadhiwa ni fedha inayowekwa kwa ajili ya mahitaji ya baadaye nay a dharura na sio kwa ajili ya mahitaji ya kila siku. Fedha iliyohifadhiwa hukuelekea wakati fedha inayotumika huelekea mbali na wewe.Lazima utofautishe hela unayoiweka akiba na hela unayoitumia, kuweka hela kwa ajili ya harusi au manunuzi fulani sio akiba.Akiba ni hela ambayo hauitumii wala kuipangia mipango kwa sasa, unaweka kwa ajili ya yatakayotukia maana hatujui ya kesho.

2.Kushindana na wengine

Watu hutumia fedha sio kwa sababu wanamahitaji muhimu bali ni ili wawe sawa na wengine, waende na wakati wasije wakaonekana wabahili au washamba. Unaweza ukawa na uhitaji wa gari au simu, jiulize je unayoinunua ni kweli ndio hitaji latko au unataka uonekane nawe umo japo uwezo wako haufikii hapo? Watu wako tayari kuingia kwenye madeni ili mradi washindane na wengine katika kumiliki vitu vya gaharma.

3. Kuahirisha mipango yako mara kwa mara

Adui mkubwa wa mafanikio ni kusitasita na kuchelewa. Tunapanga mambo mengi sana kwa ajili ya maisha yetu ila tunakwamishwa na kusitasita na kuchelewa kuyatekeleza. Kila unapotaka kuchukua hatua unaona ngoja ufikirie ena na uangalie hali inakwendaje, hatimaye siku, miezi, miaka inakatika wewe upo pale pale. Unapoona tayari umeshaazimia moyoni mwako usikubali kuahirisha kila mara, chukua hatua ili iweze kufanikisha maisha yako.


HITIMISHO 

Kanuni ya kukuza Uchumi wako Itaendana Sawasawa na Unavyojitoa Kwa Mungu.

Ni Jukumu la Kila Mkristo Kujitoa kwa Mungu nakuwa na matumizi Mazuri Ya Pesa.


Wito

Sambaza kwa Group zako

WhatsApp Pastor Richard +255759861768

Nipo Morogoro Veta Dakawa 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

MAOMBI YA USIKU WA MANANE 2025

KITABU IJUE NDOTO YAKO