SOMO: USALITI

                       SOMO; USÀLITI
Mwal; Pastor Richard
Yupo Morogoro veta Dakawa
YouTube; Kanisa la Moto wa Yesu
             UTANGULIZI
Tusome Vitabu hivi
👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼
1 Mambo ya Nyakati 12:17
[17]Naye Daudi akatoka ili kuwalaki, akajibu, akawaambia, Kama mmenijia kwa amani ili kunisaidia, basi moyo wangu utaambatana nanyi; lakini kama mmekuja ili kunisaliti kwa adui zangu, kwa kuwa hamna udhalimu mikononi mwangu, Mungu wa baba zetu na alitazame neno hili, na kulikemea.
👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼
Mathayo 26:14-16
[14]Wakati huo mmoja wa wale Thenashara, jina lake Yuda Iskariote, aliwaendea wakuu wa makuhani,
[15]akasema, Ni nini mtakachonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vipande thelathini vya fedha.
[16]Tokea wakati huo akawa akitafuta nafasi apate kumsaliti.
👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼
2 Timotheo 3:1-4
[1]Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
[2]Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
[3]wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
[4]wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;

MAANA YA USALITI.
Usaliti Maana Yake Kuondoa Uaminifu au kuvunja Patano.

USALITI NI NINI?
Usaliti Ni nguvu inayokuwa imo ndani ya mtu Yenye mamlaka ya kuasi makubaliano waliokubaliana watu wa wili au Zaidi.

KUNA MAKUNDI MAWILI YA USALITI.
1: USALITI WA MWANADAMU KWA MUNGU.

2: USALITI WA MWANADAMU KWA MWANADAMU

1: USALITI WA MWANADAMU KWA MUNGU
Huu Ni uasi unaofanywa na mwanadamu kwa Mungu wake kuamua Kutembea Kinyume na sheria zake au Utaratibu wake.

Mfano
Mungu Amekukataza Usizini unapozini umemsaliti Mungu
Mungu Anasema Usiabudu miungu wewe unaenda kwa Waganga au unaloga au ulevi Unafanya Unakuwa msaliti hapo ndipo Mungu Anakuacha.

MAMBO GANI HUMFANYA MTU AMSALITI MUNGU
1:Kukosa Mlezi wa Kiroho na Kutokujifunza Mambo ya ROHONI.
2;Kutokutii Neno la Mungu
3: Dhambi Ya Kurundiarundia
4:Kutokufundishwa Neno la Mungu
5;Kukosa moyo wa Toba ndani ya mtu

HASARA ZIPI UNAZOPATA
1;Kutengwa na Neema ya Mungu
2;Kuruhusiwa shetani akutese
3;Kuwa mlango wa adui kukutesa
4:Milango yako Ya Ufahamu Kufunguliwa.
5;Kutokusamehewa Dhambi.

TUFANYE HAYA ILI TUSIMSALITI MUNGU.
1:Tuwe na Mlezi wa Kiroho Yaani Baba Wa Kiroho.
2:Tulitii Neno la Mungu nakuliishi
3;Tuwe na Moyo wa Toba
4:Tubomoe Madhabahu za wenyeji Tujenge Madhabahu ndani yetu.
__________________________________________________________________
_______------------------------------_________________------------------____________

2;USALITI WA MWANADAMU KWA MWANADAMU
Huu Usaliti huwa Ni uasi wa mwanadamu kwa mwanadamu Yaani
Kuvunja uaminifu kwa Wanadamu Wegine.

Mfano; Unasema unampenda mtu hutamuumiza unakuja kumuumiza.
Au kwenda nje ya makubaliano Yenu Wawili Mfano muwe mmepatana Kufanya Jambo mwengine Gafla akabadilika.

MAMBO HAYA HUFANYA UMSALITI MWIGINE
1;Kupenda Pesa Kuliko utu.
2:Kuagalia Thamani Ya nje sio thamani ya utu.
3:Kukosa Uaminifu
4;Upendo wa maagizo
5:Kujipenda mwenyewe na ubinafsi.

HASARA UNAZOPATA UKIMSALITI MWEZAKO
1:Hutampenda
2:Hutotunza Siri zake
3:HUTAKUWA na Utu
4:Maisha yanaharibika
5;Kujenga Uadui na Msaliti
6;Kukosa hofu ya kabisa.

MAMBO HAYA YAFANYE UKIWA HUTAKI UWE MSALITI.
1:MPENDE MWEZAKO toka moyoni mweleze hisia zako unampenda.
2:Kuwa na Utu ukimuona Hana raha kuwa faraja kwake
3:Kuwa mwaminifu na mkweli kwake
4;Kuwa mtu wa ibada na Mungu.

HITIMISHO
Tunatakiwa Tuepuke Usaliti na huku tukielewa Usaliti unatutenga na Mungu Tuwe na utu Tusiwapende Wezetu kwa Sababu ya Kitu.

WITO
Fika Kanisani Morogoro Veta Dakawa Mfate WhatsApp number Pastor Richard+255759861768 Akupe Maelekezo Ya Kufika

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.