SOMO; ULIMWENGU WA ROHO
SOMO: ULIMWENGU WA ROHO
🍉Mathayo:5:14 👉🏿24:14👉🏿Luka;20;34👉🏿Warumi;11;12-15
UTANGULIZI
______________
1 Wafalme 2:2-4
[2]Mimi naenda njia ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, ujionyeshe kuwa mwanamume;
[3]uyashike mausia ya BWANA, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako;
[4]ili BWANA afanye imara neno lake alilonena kwa habari yangu, akisema, Ikiwa watoto wako wataiangalia njia yao, wakienda mbele zangu kwa kweli, kwa moyo wao wote, na kwa roho yao yote, (akasema), hutakosa mtu katika kiti cha enzi cha Israeli.
👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👉🏿👉🏿👉🏿👉🏿
1 Wafalme 8:57-61
[57]BWANA, Mungu wetu, na akae nasi, kama alivyokaa na baba zetu; asituache, wala asitutupe;
[58]aielekeze mioyo yetu kwake, ili tuende katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na sheria zake, na hukumu zake, alizowaamuru baba zetu.
[59]Na maneno yangu haya, niliyoyaomba mbele za BWANA, na yawe karibu na BWANA, Mungu wetu, mchana na usiku, ili aitetee haki ya mtumishi wake, na haki ya watu wake Israeli, kwa kadiri ya haja zao za kila siku.
[60]Watu wote wa ulimwengu wajue ya kuwa BWANA ndiye Mungu; hakuna mwingine.
[61]Mioyo yenu na iwe kamili kwa BWANA, Mungu wetu, kuenenda katika sheria zake, na kuzishika amri zake, kama ilivyo leo.
👉🏿👉🏿👉🏿👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼
Yohana 18:36
[36]Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa.
MAANA YA ULIMWENGU WA ROHO ;- Ni Ulimwengu usionekana katika macho ya Damu na Nyama lakini ukiendesha maisha Kama ya Ulimwengu wa Damu na Nyama.
KWANINI UPO ULIMWENGU WA ROHO 👉🏿Upo kwa kuwa Upo Ulimwengu wa Damu na Nyama.
VITA VYETU HUPAMBANA NA ULIMWENGU WA ROHO
Chochote unachoona Unafanya hakisimami Ni kwa Sababu umezibitiwa katika Ulimwengu wa roho.
MUUNDO WA UONGOZI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO
1: UONGOZI WA JUU
a:Shetani Ambaye ndio Baba wa Ulimwengu huo
b:Wakuu Anga Hawa ndio Wasaindizi wake Kama mwana
c:Majeshi na Sekta Zote Husimama Kama majeshi
2: UONGOZI WA KATI
Huu uongozi wa utendaji kazi
a)Ufalme wa Wachawi na Waganga
b)Ufalme wa Majini
c) Ufalme wa Mapepo
d)Ufalme wa Mizimu
3: UONGOZI WA MWISHO
Ni Uongozi Wa Utendaji
a)Uongozi wa utendaji katika Ngazi ya Juu huwa wakuu Anga.
b)Uongozi wa Utendaji katika Ngazi ya Kati huwa Viongozi wakuu wa kila falme.
FAIDA YA KUUJUA ULIMWENGU WA ROHO
1:inakusaindia uweze kupambana nao vizuri
2;Uudhibiti Ulimwengu wa roho usikutese
3:Uumiliki Ulimwengu wa roho
Kinyume Cha FAIDA Ni HASARA
Hitimisho
Ujue Ulimwengu wa Roho kwa kina ndipo uanze kupambana nao usikimbilie kupambana nao wakati huujui.
Wito
Fika Kanisani Morogoro Veta Dakawa Upate Elimu Zaidi UPONYWE Nifate WhatsApp number+255759861768
Maoni
Chapisha Maoni