SOMO: USIRUHUSU MTU ANGUSE MOYO WAKO
SOMO:USIRUHUSU UNGUSWE MOYO WAKO NA MTU
UTUNZE MOYO WAKO
MOYO; huwa ndio Chanzo Cha Furahs Kwako au Huzuni.
Kupitia Moyo Unaweza kuhisi na Kupata Taarifa YOYOTE.
UNATAKIWA HAKIKISHA MOYO WAKO UNAUFANYIA HAYA.
1:LINDA MOYO WAKO KULIKO KIUNGO CHOCHOTE.
Usikubali mtu aunguse moyo wako au akupige kwenye moyo maana utaumizwa na kujeruhiwa usiweze Kupata Matibabu ya haraka.
Mungu Ametupa Tahadhari Kupitia Kitabu Cha
Mithali 4:23
[23]Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;
Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
Zaburi 73:26
[26]Mwili wangu na moyo wangu hupunguka,
Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu
Na sehemu yangu milele.
2; USIRUHUSU MAWAZO MABAYA YA UNGUSE MOYO WAKO
Unaweza Kuupa Mawazo mabaya au Kufikirisha mabaya na Ukajikuta unajiumiza mwenyewe Usiufanye moyo wako uwaze mabaya
MUNGU huchukizwa na Mawazo Mabaya.
Mwanzo 6:5
[5]BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.
ππΌππΌππΌππΌππΌ
Zaburi 66:18
[18]Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu,
Bwana asingesikia.
3:UFANYE MOYO WAKO UFURAHI KILA SAA.
Moyo wako UFANYE uwe na Furaha kila Siku Usiufanye moyo ukose Furaha.
Mwanzo 18:12
[12]Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee?
Zaburi 16:9
[9]Kwa hiyo moyo wangu unafurahi,
Nao utukufu wangu unashangilia,
Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.
4;USIUFANYE MOYO WAKO MGUMU KUTII $AUTI YA MUNGU.
Moyo wako Usiwe Mzito Kutii Sauti Ya Mungu usikiapo Sauti ya Mungu
Kutoka 7:13-14
[13]Moyo wa Farao ukawa ni mgumu asiwasikize; kama BWANA alivyonena.
[14]BWANA akamwambia Musa, Moyo wa Farao ni mzito, anakataa kuwapa watu ruhusa waende zao.
5;UFANYE MOYO WAKO UMPENDE MUNGU.
Mpende Mungu Kuliko Kitu Chochote Muweke Mungu Moyoni Mwako
Kumbukumbu la Torati 6:5
[5]Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.
6:UFANYE MOYO WAKO KAMA ULIKOSANA NA MUNGU UMRUDIE MUNGU
Kumbukumbu la Torati 30:2
[2]nawe utakapomrudia BWANA, Mungu wako, na kuitii sauti yake, mfano wa yote nikuagizayo leo, wewe na wanao, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;
7: USIFANYE MOYO WAKO UWE HONDARI USIONGOPA.
Moyo ulioshujaa usioongopa hofu yoyote au shaka Yoyote.
Yoshua 1:6
[6]Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.
8;UFANYE MOYO UTUNZE NENO LA MUNGU
2 Samweli 7:21
[21]Kwa ajili ya neno lako, na kwa moyo wako mwenyewe, umetenda makuu hayo yote, ili umjulishe mtumwa wako.
9:UFANYE MOYO UWE MVUMILIVU KWA BWANA.
Hakikisha moyo wako Unakuwa na Subira kwa Bwana
Zaburi 27:14
[14]Umngoje BWANA, uwe hodari,
Upige moyo konde, naam, umngoje BWANA.
10: UFANYE MOYO UWE MOTO KATIKA BWANA.
Zaburi 39:3
[3]Moyo wangu ukawa moto ndani yangu,
Na katika kuwaza kwangu moto ukawaka;
Nalisema kwa ulimi wangu,
HITIMISHO
UFANYE MOYO WAKO UWE NA FURAHA ULIZI NA AFYA
Kwa Kuulinda Moyo Wako
WITO
Tumia Namba hizi umfate WhatsApp Pastor Richard Akupe maelekezo ya Kufika Kwenye Huduma hii Ufundishwe+255759861768
Maoni
Chapisha Maoni