SOMO; NGUVU YA MAMLAKA

SOMO; NGUVU YA MAMLAKA ILIYOMO NDANI YAKO INAVYOAMUA HATIMA YA MAISHA YAKO


Naitwa Pastor Richard
Nipo Morogoro veta Dakawa
WhatsApp Number+255759861768
Jumapili Tar 9/1/2022


USHUHUDA


Kasemwa alikuwa mtu anayeteseka na Maisha ya magonjwa magonjwa akawa amefika Kanisani H.i.v inamtesa nikamuuliza H.i.v uliipataje akasema Babs Mimi sijui nikamwuliza Nini Tena kinachokusumbua akasema mahusiano Yangu Yanashinda kila mwanaume naye mpata anakuwa Tayari kwenda Kutoa mahari lakini Mimi naongopa kwenda kupima Ndipo nilipoiona MAMLAKA YA UKIMWI Inavyomuendesha


 
1;Ameipa nafasi mamla ya h.i.v ikae ndani Yake


2:Anataka mamlaka ya Afya iondoke ndani Yake lakini hajui aliipaje
Mamlaka hayo nayo inangoma kuondoka


3;Inaanza Kumpangia Wewe hutaolewa Sababu Mimi H.i.v nipo nawe nimekuoa


4;Anaikumbalia Kasemwa anakaa Singo kisa ile mamlaka ya ukimwi IPO

Afsnye Nini Sasa Lazima Ajue aliipaje nguvu Kubwa H.i.v Iwe na mamlaka Makubwa ndani Yake Kisha aseme nitaolewa na sitameza dawa au kuisikiliza Mimi ninayomamlaka ya Afya.


NGUVU YA MAMLAKA.  Ni uwezo na nguvu iliyomo ndani mwaka Yenye mamlaka ya Kufanya Chochote kwenye ulimwengu want roho na ikasimama hivyo hiyo nguvu ilivyoamua ikuendedhe.

Chochote Unachokiona Unakiishi Kinamamlaka kimeamua uishi hivyo Nani wakuja kukiamuru kiondoke Ni Yule mtu mwenye mamlaka
.
MAMBO AMBAYO HUKUJULISHA IPO MAMLAKA NDANI YAKO

1:MAMLAKA HUWA NI KITU CHENYE NGUVU NA MAAMUZI YOTE NDANI YA KUTENDA INAVYOJISIKIA


Danieli 11:3
[3]Na mfalme hodari atasimama, atakayetawala kwa mamlaka kubwa, na kutenda apendavyo.

Chochote ukiona ndani yako kinakutawala Mfano magonjwa wewe Ni mtu unaumwaumwa TU magonjwa yanayo mamlaka Na Mwili wako. Ukiona Huolewi nguvu ya kutokuolewa inayonguvu ndani yako.

2:MAMLAKA INAYONGUVU YA KUENDESHA KIZAZI CHAKO KIKAWA NA MAISHA YA KUFANANA AU TATIZO LA KUFANANA


Zaburi 145:13
[13]Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote,
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.

Mamlaka inaweza kuwashika Wazazi mpaka watoto na mpaka Wajukuu inayonguvu yakuwapeleka waishi inavyotaka Yenyewe Mfano mamlaka ya umaskini au mamla ya magonjwa Unaweza kukuta familia Nzima inateswa na magonjwa ujue hiyo Ni mamlaka.

3:MAMLAKA INAWEZA KUINGIA NDANI YA MTU NA IKAMTAWALA KUPITIA BARUA AU MAANDISHI .

Unaweza kuletewa Taarifa ukaisoma na ile mamlaka ikaingia ndani ya mwili wako kukutumikisha Kama ilivyoandikwa ukaanza kuitii
Mfano; Umepokea ujumbe Mimi nawewe Kuazia Leo Basi usinitafute Wala kupiga Usipoelewa Kweli mtaachana.
Au UMEENDA Kupima Daktari akaandika Una.U.T.I Taiford Na Malaria Ukirudi nyumbani lazima uitii hiyo mamla uliyoisoma

 
Esta 9:29
[29]Ndipo malkia Esta, binti Abihaili, pamoja na Mordekai Myahudi, alipoandika kwa mamlaka yote kuithibitisha barua hii ya pili ya Purimu.

4:MAMLAKA HUPEWA NGUVU KUPITIA JINA LA HICHO UNACHOTAKA KIKUTAWALE.

Mfano ukitaka uwe mgonjwa lazima uiruhusu Jina la ugonjwa huo litamkwe ndani yako ulisikie Mfano wewe unah.i.v Postive
Wewe unakansa wewe unakisukari .
Usipe nafasi kusikiliza mamlaka inayokuharibu SomaπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌ


Marko 11:28-31
[28]wakamwambia, Ni kwa mamlaka gani unatenda mambo haya? Naye ni nani aliyekupa mamlaka hii uyatende haya?
[29]Yesu akawaambia, Nitawauliza neno moja, nanyi mnijibu, kisha nitawaambia ni kwa mamlaka gani nayatenda haya.
[30]Ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni, au kwa wanadamu? Nijibuni.
[31]Wakasemezana wao kwa wao, wakisema, Kama tukisema, Ulitoka mbinguni, atasema, Mbona, basi, hamkumwamini?

5; MAMLAKA INANGUVU YA KUKUPONYA MATATIZO YOTE

Mamla inayonguvu ya kukuponya Tatizo lako na Kukataa magonjwa ndani yako ikiwa ile mamlaka utaitamka kwa kuponya au afya


Luka 9:1
[1]Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi.

6;MAMLAKA INANGUVU YA KUKUPA UZIMA WA MILELE USITESEKE.

Mamla inaweza ikasema USITESEKE na huwezi kuteseka inaweza Kusema Uwe mzima wa Afya unakuwa


Yohana 17:2
[2]kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.

7; MAMLAKA HUWA INAENDA KWA LEVO ILE YA JUU INAAMRISHA WA CHINI
Unaweza kukuta Tatizo ndogo ndani yako linapata nguvu kukusumbua au kukutesa kwa Sababu limeamrishwa likutese na usipojua litakutesa.


Warumi 13:1
[1]Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.

8; MAMLAKA YOYOTE HUDHIBITISHWA NA MUNGU


Warumi 13:2
[2]Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu.

Kila Mamlaka inayotenda Kazi ndani Yako ujue Mungu Ndiyo Ameiweka ifanye kazi ndani Yako na Yeye ndiye mwenyekuiondoa.

9:USIIDHARAU MAMLAKA ILIYOPO.


2 Petro 2:10
[10]na hasa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu. na kudharau mamlaka.
Kila Mamla inanguvu ndani yako usidharau inaweza kukutesa au usiteke

10;TUMIA MAMLAKA KUKEMEA MAMLAKA ZINGINE ZOTE


Tito 2:15
[15]Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote.

Unapotaka kuitoa mamlaka nyigine Tumia mamlaka kuiambia huitaji itoke itatoka.

RUHUSU ikutawale mamlaka ya Kimungu ndani Yako Ikatae mamlaka ya shetani.

HITIMISHO


Jiulize IPO mamlaka ngani inakutawala na Kwanini imepata nguvu

WITO


Chukua hatua Fika Kanisani Morogoro Veta Dakawa 2022 Ni Mwaka Wa Masahihisho
MFATE WhatsApp number Pastor Richard Akupe maelekezo ya Kufika Kwenye Huduma hii+255759861768

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.