SOMO:FOMULA YA KUPATA MKE/MME WA KWA MUNGU

SOMO: JINSI YA KUPATA UBAVU WAKO.

Naitwa Pastor Richard Mwalimu wa Wanandoa
Karibuni Tuponyane Kwenye Kipengele hiki
Jifunze Somo Hili Unaetaka Kupata mke/mme mfikie ndoa.

Kila kitu huwa kinafomula Hakuna Jambo unaloweza kulisimamimisha  bila kuliwekea Fomula Ndoa ya Kutoka kwa MUNGU inafomula Ni tofsuti na MKE/mme unayempata kwa Akili Zako.

MAMBO HAYA YAFANYE UKIWA KWENYE UTAFUTAJI WA MKE/MME

1:ANZA KWA KUMPENDE MUNGU KWA AKILI ZAKO ZOTE NA MOYO WAKO WOTE.
Mathayo 22:37
[37]Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.

UKIMPENDA MUNGU MAMBO HAYA YATAJIDHIHIRISHA


1;Utampata mtu Sahihi kwa muda Sahihi
2;Utampata mtu mwenye Sifa unazotaka
3;Hatua Zenu kwenye mahusiano hazitaishia Njiani
4;Utakuwa Ushuhuda kwa Wegine

  2:USIZINI NA MTU AMBAYE  HAJAKUTOLEA MAHALI WALA KUJIRAHISISHA BINT UNATAKIWA UKIMBIE DHAMBI YA UZINIFU.


Mathayo 5:27
[27]Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;


πŸ‘‰πŸΏπŸ™ MAANA UKIZINI NA MTU AMBAYE HAJAKUTOLEA MAHALI
1:Utakwamisha hatua zisiendelee Milango Yake itafunga
2:Mtachokakana haraka mtaachana
3;Mtapoteza Ushuhuda wa Kristo.
4:Utapatwa na mikosi Mbalimbali.

KIJANA USIZINI NAWEWE BINT USIJIRAHISHE KISA UNAKIMBILIA KUOLEWA mwanaume atakayekuambia mzini huyo SI muoaji Ni mharibifu wa mwili wako.

3:UNAPOMUOMBA MUNGU AKUPE MKE/MME USIMUOMBE UKIWA TAYARI UNAMCHUMBA AU RAFIKI UNAEMTAZAMIA.

Mathayo 5:37
[37]Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.

MAANA UKIJA MBELE ZA MUNGU KUMUOMBA NA UNAMTU KICHWANI MAMBO HAYA YATATOKEA.



1;Utakapopewa mke/mme wa Kwa Mungu utakataa utasema Pastor Richard niombee huyohuyo arudi Nampenda Sana.
2;Utafanya ucheleweshe kujibiwa kwa Kuwa Tayari Unamtu KICHWANI mwako.
3;Utafanya Mungu akuache uendelee na huyo uliyempata kwa Akili zako.

HAYA YAZINGATIE SANA KWA KIJANA UNAETAKA KUPATA HARAKA MKE AU MME.

Simu ya Pastor Richard kwa maoni na msaada mfate WhatsApp Akupe maelekezo ya Kufika Kwenye Huduma hii+255759861768

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.