SOMO:FAIDA ZA UTOAJI

SOMO: FAIDA 8 ZA UTOAJI KWA BWANA

Sadaka ni sehemu ya utoaji unaoacha pengo Katika Mali zako, yaani baada ya kutoa unaona mahali ulikotoa Mali hiyo pameachwa wazi.Hata hivyo Biblia inasema utoaji Wa kweli ni kujitoa nafsi yako kwanza kwa Mungu kama dhabihu mtakatifu ya kumpemdeza Mungu.


“Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.”
(rom 12: 1)


Mungu anatengemea tutoe nafsi, roho na miili yetu kama sehemu ya sadaka kwa Mungu. Itakusaidia nini kama utajitoa kwa ulimwengu na KUFANYA viungo vyako kuwa silaha za dhuluma kwa ulimwengu Bali tujitoe kwa Mungu kuwa sadaka kwa Mungu.(1Kor 6:13-16 )
————
13 Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili.


14 Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake.


15 Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!


16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.


Mwili wako, nafsi yako na roho yako utoe kwa BWANA kama dhabihu takatifu kwa BWANA. Yafutayo ni mambo saba unayopaswa kujua KUHUSU sadaka yako, kama ifuatavyo;


1. SADAKA INANENA MBELE ZA BWANA


Sadaka yako unaweza kunena vena Mbele za Mungu ikawa UKUMBUSHO Wa Yale uliyomba kwa Mungu, Sadaka haiwezi kunyamaza hata kidogo.


Mfano:1. KORNELIO


1 Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,
Matendo ya Mitume 10 :1


2 mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima.
Matendo ya Mitume 10 :2


3 Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio!
Matendo ya Mitume 10 :3


4 Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
Matendo ya Mitume 10 :4


MFANO:2 DORKASI


(Mat 9 )
————
36 Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa.


37 Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani.


38 Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja kwetu.


39 Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao.


40 Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.


41 Akampa mkono, akamwinua; hata akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, hali yu hai.


2.TOA SADAKA YAKO KWA IMANI.


Katika utoaji wako iwe fungu LA kumi,limbuko, sadaka ya nadhiri,au changizo lolote. Toa kwa IMANI. Toa kwa matarajio fulani kuwa MUNGU atakusaidia katika jambo Fulani. Hiyo nfiuo tafsiri ya IMANI. IMANI ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, hivyo tarajia kitu kwa BWANA YESU.


4 Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena.
Waebrania 11 :4


Unapotoa sadaka yako uwe unatarajia kitu kwa Mungu, unaona waliotoa hata kama wamekufa Mungu aliwafufua, wengine wananena sadaka yako inasema za Mungu.


3.USITOE KWA MANUNGUNIKO AU KUJISIFU.


Unapotoa sadaka yako unapaswa kukumbuka usitoe kwa kunungunika au majivuno au kwa huzuni maana Mungu anataka MTU anayetoa kwa moyo mkunjufu.


(2Kor 9 )
————
6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.


7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.


(Gal 6 )
————
6 Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote.


7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.


8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.


9 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.


4. USIWE NA NENO NA MTU.


Moja ya kikwazo mbele za Mungu kuhusu sadaka ni kama hujapatana na uliyekosana naye. Hakikisha umepatana na mtu, maana kuna uhusiano kati ya sadaka na moyo wako hivyo MUNGU ana taka moyo wako. Patana na mtu uliyemkwaza.


(Mat 5 )
————
23 Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,


24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.


25 Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.


5.KILA AINA YA SADAKA KUNA BARAKA ZAKE/AHADI ZA MUNGU KUTUBARIKI.


Fungu LA kumi au zaka. Mungu ameahidi kufungua mbingu zako au vyanzo vipya vya mafanikio. Ukipata mapato mapya unatoa aslimia kumi kwa mfano 10% ya 100=10. Ukitoa fedha hapa usitarajie kupewa pesa Bali utapewa vyanzo vipya vya kipatia kipato(Mal 3 :8_11 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.


9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.


Malimbuko…Mungu ameahidi Baraka za malimbuko au uzao Wa kwanza.
(Met 3:
9 Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.


10 Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya..


NADHIRI

Nadhiri ni ahadi tunazomwekea MUNGU kuwa akitufanya jambo sisi tutatimiza jambo Fulani kwa moyo wetu Washukrani mbele zake “Akaweka nadhiri, akasema, Ee Bwana wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe.(“1Samwel 1:11)


SADAKA ZINGINE Mungu anaangalia moyo wako maana haina kiwango lakini haimaanishi utoe kidogo. (2Kor 9 )
6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.


7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.

8 Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;

9 kama ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele.

10 Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu;

11 mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.

12 Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu.


6.USITOE SADAKA YAKO KWENYE MADHABAHU YA MUNGU MWINGINE.


Sadaka ni Ibada usije ukatoa ibada kwenye madhabahu ya sanamu au kwa makuhani baali. Nakumbuka siku moja wa ukoo wangu waliomba nichangie sehemu ya fedha kwa ajili ya kutimiza tambiko. Nilikataa kabisa.Nakumbuka kabla ya kuokoka tulikuwa tunatoa nia ya misa kwa ajili ya wafu, nakuomba waliokufa lakini nilipookoka macho yangu yalifunguliwa. Mpendwa usije ukafanya jambo ambalo litakuunganisha na madhabuhu ya Giza.


(Kuto 20 )


23 Msifanye miungu mingine pamoja nami; miungu ya fedha, wala miungu ya dhahabu, msijifanyie.


24 Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo zako, na ng’ombe zako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia.



“Mtu atakayemchinjia sadaka mungu ye yote, isipokuwa ni yeye Bwana peke yake, na angamizwe kabisa.”
(Kuto 22: 20)


7. TOA SADAKA YAKO KWA TARATIBU ZA BIBLIA.


Biblia natoa taratibu kwa kila aina ya sadaka unatoa hivyo tenda vema utapata kibali na sadaka yako itasema mbele za MUNGU kama tulivyojifunza KATIKA namba moja.


Ukitoa vibaya MUNGU hapokei.(Mwa 4 )
————
1 Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana.

2 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi.

3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.

4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;

5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.

6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?

7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishnde.


8;MKUMBUSHE MUNGU KUHUSU AHADI ZAKE / DAI HAKI ZAKO NAWE UTAPEWA.


Mungu mwenyewe katuruhusu tumkumbushe ahadi zake. Mpendwa jipange usiwe na mpengo KATIKA UTOAJI wako.


(Is 43 )
————
25 Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.


26 Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako


By
Pastor Richard

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.