SOMO; MAAJABU YA TENDO LA NDOA
SOMO; MAAJABU MATANO YA TENDO LA NDOA
1;Mwanaume hutoa mbegu hadi milioni 300 kwa tendo moja tu la ndoa, lakini mbegu moja pekee hutumika kuzalisha mtoto inapokutana na yai la mwanamke lililotayari.
2;Kufika kileleni kwa mwanamke ni msaada mkubwa kiafya kwake. Huweza kumsaidia mwanamke kupunguza hatari zaidi ya kupata magonjwa ya moyo, kupooza, kansa ya matiti pamoja na msongo wa mawazo.
3. Mwanamke anapokuwa kileleni hukaa takribani sekunde 20 hadi 14, tofauti na wastani wa mwanamme ambaye hukaa kwa wastani wa sekunde 6 tu. Hata hivyo, tofauti na mwanamke, mwanaume anapokuwa kileleni hupitiwa na giza zito katika ubongo wake kwa sekunde takribani tatu (blackout).
4. Tendo la ndoa hupunguza maumivu ya kichwa.
-Utafiti uliofanywa na wa wataalam wa saikolojia na uhusiano kutoka Chuo Kikuu cha Munster chini Ujerumani umebaini kuwa tendo la ndoa husaidia kupunguza maumivu ya kichwa. Utafiti huo uliochapishwa mwaka 2013, ulibaini kuwa mtu mmoja kati ya watano waliofanya mapenzi wakiwa na maumivu ya kichwa, alimaliza akiwa hana maumivu hayo tena.
Kwenda haja ndogo muda mfupi kabla ya tendo la ndoa ni hatari zaidi kwa afya.
-Ingawa wataalam wengi wa afya wamekuwa wakieleza kuwa kwenda haja ndogo kabla na ya tendo kunasaidia kuepuka ugonjwa wa UTI, huu sasa unatajwa kuwa ‘nusu ukweli’.
UTI hutokea pale kibofu cha mkojo kinapopata bakteria wanaoingia kupitia njia ya mkojo. Na tendo la ndoa linaweza kusaidia maambukizi wa bakteria hao kuwatoa kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
Maoni
Chapisha Maoni