SOMO: SIRAHA 5 ZA KUMTEKA MWANAUME

SOMO: SIRAHA 5 ZA KUMTEKA MWANAUME YEYOTE

Tufunue Mithali;14;1-5 ,12:1-3

Karibuni Wanandoa Tuogee Leo Kuhusu ufanye Nini ili mmeo au mchumba umkamate Asirukeruke au Kutangatanga huku MPE haya yatakufanya Mwanaume Yeyote Asiruke au Asikunyanyase Silaha hizi Zitumie wewe mwanamke imara

Naitwa Pastor Richard Mwalimu wa Wanandoa
WhatsApp Number Pastor Richard+255759861768



SILAHA YA KWANZA


Silaha ya kwanza anayopaswa kuwa nayo mwanamke ni kuwa na maisha yake na siyo maisha ya kuiga.


Wapo wanawake ambao hupenda kuiga kile kinachofanywa na wanawake wenzake na kudhani hivyo ndivyo anavyopaswa kuwa. Mwanamke mwenye tabia hii anaonekana ni mtu feki. Mwenye tabia hii huwa hana mvuto kwa mwanaume kwani atakuwa ni mwanamke feki. Ukweli ni kwamba wanaume wanapenda mwanamke anayeishi maisha halisi.


SILAHA YA PILI


Mwanamke anapaswa kuwa mtiifu na mwenye heshima na busara. Mwanamke hapaswi kuwa na kiburi na kutaka kuota mapembe kwenye uhusiano wake. Heshima na utiifu haimaanishi kuwa tayari kunyanyaswa, hapana. Mwanamke anapaswa ampe mpenzi wake au mumewe heshima inayotakiwa kama kichwa cha uhusiano wenu. Linapotokea jambo la kubishana kati yenu hasa mnapokuwa na watu wengine, mwanamke unapaswa kuzungumza kwa hekima na busara. Hii itamfanya mwanaume kuona mwanamke wake ni ‘kichwa’.


SILAHA YA TATU


Mwanamke anapaswa kuwa na uwezo wa kujitegemea. Hapa pana utata kidogo. Wapo wale wanaoamini kuwa mwanamke anapaswa kumtegemea mwanaume kwa kila kitu. Lakini ukweli ni kwamba wanaume wengi wanapenda kuwa na uhusiano na mwanamke ambaye anaweza kusimama kwa miguu yake na kujitegemea pia.


SILAHA YA NNE


Mwanamke lazima awe anajiamini. Naam, hapa haimaanishi kuwa anatakiwa kuwa kiburi na mbishi, hapana. Isipokuwa mwanamke anapaswa aoneshe kujiamini kwa kile anachokisema na anachotenda. Lazima matendo yake yafanane na maneno yake. Asiwe na maneno mengi halafu vitendo ni sifuri.


Kujiamini kwa mwanamke kunamfanya mwanaume ajue kuwa ana mpenzi au mke ambaye anaweza kukabiliana na mikwaruzo mbalimbali inayohitaji hoja na utetezi.


SILAHA YA TANO


Mwisho, silaha nyingine ni kuwa na mvuto wa kipekee. Hapa haimaanishi kuwa mrembo sana, hapana. Ina maana kuwa mwanamke anapaswa kuwa nadhifu kila wakati ili kumfanya mwanaume apende kuwa nawe na avutiwe kuwa na wewe wakati wote.


Silaha hizi tano akiwa nazo mwanamke yeyote, basi mwanaume haruki na atambue fika kuwa mwanaume atavutiwa nawe na uhusiano wenu unaweza kudumu na kudumu na kudumu

TUNAPOMALIZA SOMO LETU TUELEZANE UMTUMIA SIRAHA ZIPI KUMKAMATA MWANAUME

Share kwa Wegine

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.