MAOMBI YA UTIISHO
MAOMBI YA UTIISHO WENYE NGUVU MBELE YAKO
1;Maombi haya Yaombe Kila Siku unapotoka nyumbani
2:Maombi haya Ni Maombi ya Mamlaka Ya Kifalme
3:Unapoomba Tamka Kwa Kukanzia maneno
Ninalidhibitisha Neno la Mungu mbele Yangu Leo Ninapotoka hapa Kwenda____Ninatuma nguvu ya UTIISHO ikaharibu kila mitengo ya Adui Zangu kila maneno ya Adui Zangu kila vikao vya uharibifu kila aliyesimama kuzuia mbele Yangu Kila Nguvu inayoandaliwa ya Rushwa Kila roho ya kucheleweshwa kila roho ya kupangiwa siku ya kurudi kila namna ya uharibifu hautasimama kwa Jina la Yesu Ni Neno linasimama Kutoka Kama Navyolikirii kwa Kusoma linasema(👉Kutoka 23:27
[27]Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao.)Nasema Leo hii Hakuna Adui atakaye Simama mbele Yangu Katika Jina la Yesu 🙏 Amen
Rudia Mara 5
Kisha ndio nenda kwenye kazi zako
@Pastor RICHARD Nipo Morogoro Veta Dakawa
WhatsApp Number+255759861768
Share kwa magroup
🌴🌴🌴🌴🌴🌴🌴🌴✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️♿
MAOMBI YA KUFUTA ALAMA ZA CHALE NA MAANGANO YALIYOFANYIKA KATIKA MWILI WAKO.
1:Uwe una Alama za chale au ulishachanjwa Kichawi.
2:Omba Kwa Kufata maelekezo yalivyoandikwa.
JINSI YA KUOMBA
🚰🚰🚰🚰🚰🚰🚰
Mambo ya Walawi 21:5
[5]Wasijifanyie upaa kichwani, wala wasinyoe pembe za ndevu zao, wala wasichanje chale katika miili yao.
Neno Hili Limetimia ndani yangu Sitachanjwa Chale Tena nafuta kila Aina Ya Alama za chale Zilivyouganishwa nakutumika ndani ya mwili wangu navua ngozi ya chale navaa ngozi isiyochanjwa Chale Katika ulimwengu wa roho Uelewe Mimi RICHARD Nimekombolewa Katika Mwili kwa damu ya Yesu Katika Jina la Yesu 🙏 Amen
Rudia Mara 4
______________________________________________________
________________________________________________________
MAOMBI YA KUKIRI WAKATI UPO KATIKA MAPITO
1:Soma mistari hii kwa kumanisha wewe ndiye mwenye Tatizo
2:Rudia Mara Tatu Kusoma maandiko haya
3:Kisha Omba Maombi kwa imani.
JINSI YA KUOMBA
👉🏿👉🏿👉🏿👉🏿👉🏿👉🏿👉🏿👉🏿
Kutoka 6:3-8
[3]nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.
[4]Tena nimelithibitisha agano langu nao, la kuwapa nchi ya Kanaani; nchi ya kukaa kwao hali ya ugeni.
[5]Na zaidi ya hayo, nimesikia kuugua kwao wana wa Israeli, ambao Wamisri wanawatumikisha, nami nimelikumbuka agano langu.
[6]Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa;
[7]nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri.
[8]Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo naliinua mkono wangu, niwape Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni YEHOVA.(Rudia Mara 3 Kusoma)
Baba Mimi Ni mtu niliyekatika mikono ya farao wa magonjwa farao ameshika uzao wangu Ameshika Uchumi wangu nk(Taja Yanayokutesa)
Kuanzia Leo Ninaomba Utume msaada wa malaika wako waje wanjvushe sawasawa na Neno lako nilivyolisoma Kutoka 6;3-8 Katika Jina la Yesu 🙏 Amen
Rudia Mara 5 maombi
Naitwa Pastor Richard
WhatsApp Number+255759861768
Maoni
Chapisha Maoni