SOMO: USHUHUDA
SOMO: USHUHUDA
Zaburi:19:7,81:5
Isaya:8;16-20
Isaya:30:8
Marko:14;56
Luka;21:13
Yohana:1:7-19
Kuna Mtu mmoja Alikuwa Anateseka na Tatizo la Uzazi tokea ubint wake mpaka miaka 53 alipofika Kanisani Kwangu Kuonana nami Baada ya Kusoma Shuhuda Kwa Akili yangu ya kibinadamu niliona Kama kitu hakiwezekani Sababu hata blid ilikuwa imekata Kiukweli mama alikuwa na imani alichokiongea Kupitia wewe Mtumishi nashuhudiwa nitapokea Ushuhuda Nilimfundisha Neno nikamuombea Baada ya miaka 2 akaanza kuona Kaja Kupokea mapacha watatu akiwa na umri wa miaka 63 Huu ndio huitwa Ushuhuda Mtu anaona Mabadiliko ya Kimwili Alikuwa hivi Anakuwa hivi.
USHUHUDA NI NINI?
Ushuhuda Ni mabadiliko anayoyaona mtu Baada ya Kuomba au Kuombewa.
Unapoona TU Hali ya mabadiliko Ulivyokuwa Mara ya kwanza na Utakavyokuwa Baada ya Maombi.
MAANA YA USHUHUDA: Matendo Makuu Yenye mabadiliko ndani yako.
KUNA AINA MBILI YA USHUHUDA
1: USHUHUDA WA KUDUMU
2: USHUHUDA WA MUDA MFUPI.
USHUHUDA WA KUDUMU
Huu Ni Ushuhuda Anaoupokea mtu nakuutuza Ushuhuda huo kwa Kuweka mahusiano mazuri mtu na Mungu Kupitia Mafundisho ya Neno la Mungu na Sadaka.
USHUHUDA WA MFUPI
Huu Ni Ushuhuda wa Mtu anaebokea Mabadiliko halafu asiendeleze mahusiano Yake na Mungu kwa Mafundisho ya Neno la Mungu Pamoja na Sadaka.
KWANINI TUNASEMA LAZIMA USHUHUDIE ULICHOFANYIWA.
1:Unaufanya Ushuhuda Wako udumu.
2:Unamuaibisha Shetani na Kazi zake
3:Unamuinua Mungu na Kazi Zake
4:Unaponya wengine Kupitia Shuhuda
5;Unaokoa roho Nyigi Zilizokamatwa na Shetani Kupitia Ushuhuda utazikomboa.
KUNA TOFAUTI KATI YA KUFUNGULIWA NA USHUHUDA
1: KUFUNGULIWA:-ni hatua ya kwanza kabisa unapoombewa unaona Hali ya tofauti ndani ya mwili wako inayoabatana na uchomvu au ishara Ambazo za kulengea mwili.
2: USHUHUDA:- Ni Hatua ya Pili Baada ya Kufunguliwa Unaanza kuona matokeo ya maisha yako vitu vinaanza Kufunguka Kuponywa kubadilika Tabia yako.
NANI ANAPASWA ASHUHUDIE ALIYEKUOMBEA AU ALIYEOMBEWA
Mwenye Tatizo ndio Anapaswa Ashuhudie mabadiliko aliyoyaona Baada ya Maombi
NITAJUAJE HUU USHUHUDA WA MUNGU NA HUU USHUHUDA WA SHETANI.
Huhitaji uwe na Roho wa Ufahamu akujulishe ishara Kubwa ushuhuda wa Mungu na wa Shetani haupatani.
1:Hauna Ushahidi wa Kile kinachoongelewa.
2:Unapishana na Kutokuoana kabisa
Marko:14:56
3:Huwa inaonesha mtu anavyofunguliwa sio matokeo Baada ya Kufunguliwa.
USHUHUDA WA MUNGU WA KWELI.
1:Utaonesha Ushahidi au picha ya tukio
2:Huoneshwa Baada ya Kufunguliwa Amekuaje
3: Ushuhuda wa Mungu haulengi unapoondoa mapepo unalenga Baada ya kuyaondoa huyo mtu anaendeleaje.
Luka;21:13
HITIMISHO
Usikubali Kukaa na Ushuhuda Shuhudia kila Unachokiona Mungu Ametenda
Wito
Mpigie Pastor Richard Akupe muogozo wa Kufika Kwenye Huduma hii+255759861768
Maoni
Chapisha Maoni