SOMO; MADHABAHU 👉🏿 Part 3

SOMO: UNAPOJENGA MADHABAHU LAZIMA UBOMOE MADHABAHU YAKO YA KALEE
Kutoka 34:10-15
[10]Akasema, Tazama, nafanya agano; mbele ya watu wangu wote nitatenda miujiza, ya namna isiyotendeka katika dunia yote, wala katika taifa lo lote; na watu wote ambao unakaa kati yao wataona kazi ya BWANA, kwa maana ni neno la kutisha nikutendalo.
[11]Liangalie neno hili ninalokuamuru leo; tazama, mbele yako namtoa Mwamori, na Mkanaani, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.
[12]Ujihadhari nafsi yako, usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea, lisiwe mtego katikati yako.
[13]Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao, na kuyakata-kata maashera yao.
[14]Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa BWANA, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu.
[15]Usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi, watu wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, na kuitolea sadaka miungu yao; mtu mmoja akakuita, ukaila sadaka yake.

MADHABAHU ZA KALE👉🏿Hii huwa Ni Tabia Ambazo Mkristo Anakuwa nazo kabla ya Kuokoka Kukubali Kuziacha nakujenga Madhabahu yako upya.

KUJENGA MADHABAHU 👉🏿Hii Huwa Ni Tabia mpya za Kiungu ndani yako kuumbika Hii hatua huwezekana ukiamua Kumpa Yesu maisha yako

HATUA UTAKAZOZIFATA UNAPOMBOMOA
1:Kuwa na mahusiano Na Mungu Katika utoaji wa Sadaka
Unapotoa Sadaka unabomoa mahusiano ya kale unajenga kwa Mungu Uhusiano Kupitia Sadaka Zako.

Hakuna Ujezi wa Madhabahu Ambao hautahusisha Sadaka Ukiona huwezi Kutembea na Mungu Katika uaminifu wa Sadaka ujue unazipa uhalali Madhabahu za kale zikutese.

2:Kuwa na Utaratibu wa Ibada na Mafundisho Ya Neno la Mungu
Unapokuwa na Utaratibu wa Ibada na Mafundisho Ya Neno la Mungu unaharibu elimu za Madhabahu ya Kale na ibada zao.

3:Kuwa na Msimamo wako Binafsi wewe na Mungu Katika mahusiano Yenye nguvu.
Hapa utaitajika Usimame mwenyewe Usipende Kushikwa shikwa unaombewa na kila Madhabahu Unakuwa Tayari unayomadhabahu yako

4:Kuwa Na Baba wa Kiroho Atakayekuongoza na Hakikisha unatoa Zaka Hapo kwa Baba yako Ili Kuifanya Madhabahu Uliyoinjega Itoe majibu yako kwa wakati.
Hapa Unapokuwa na Baba kuwa na mlezi mmoja wa Kiroho Usipende kuwa na Madhabahu Nyigi Utazuia majibu yako na ili Madhabahu hiyo ikutambue Ujue Unafatilia uaminifu
*Mafundisho ya Neno la Mungu kwa Baba yako wa Kiroho
*Kutoa Zaka Kila Mwezi na Kushiriki ujezi wa kanisa

5; Madhabahu Huwa ndio Kiuganishi Cha majibu yako kwa hiyo Ni lazima ujue kile KILICHOKUWA ndani kimeshika maisha yako ujue kiliwekwa na Madhabahu (Tabia) ya kale Huzuia majibu usipokubali Gharama huwezi Kupokea majibu yako.

Madhabahu Yaitaji Ukubali Gharama na Jinsi Ya Kujenga Ni ROHO MTAKATIFU ndiye Hujenga unapookoka.

MADHABAHU UNAPOJENGA HATUA ZA KUFANYA
1:Roho Mtakatifu Ndiye Mjezi wa Madhabahu
Lazima hatua ya kwanza katika ujenzi mkubali Yesu kuwa mwokozi.

2: SADAKA YAKO Ndiyo hulipa Gharama za Ujezi wa Madhabahu yako.
Lazima ujue kila Tatizo unaloliona Linasadaka ndani yako ndio Maana linakutesa.

3:BABA WA KIROHO Ndiye Atakayekuongoza Kumjua Mungu.
Lazima ushikwe ulelewe Kiroho na uwe na mtu anayekuongoza Kufika hatua nyigine

4: MADHABAHU YAKO MPYA Ndiyo Tabia mpya Za Kiungu ndani yako.
Lazima Ukubali Kuacha Tabia zako za nyuma na  Kufata Tabia za Mungu

MADHABAHU ZA SHETANI.
1:Hasira
2:Hofu
3:Kukata Tamaa
4:Kuwaza mabaya
5;Elimu za Shetani
6; Wasiwasi
7:Chuki
8:Kutokusamehe
9;Manug,uniko
10:Uzizi
11:Wizi wa Sadaka
12:Kuchukia habari Za Maombi
13:Kuwa na Baba wengi yaani Madhabahu Nyigi.
14:Dhambi za kujirudia rudia

MADHABAHU ZA MUNGU.
1:Upendo
2:Uvumilivu
3:Imani
4;Kuwaza mazuri
5:Elimu ya Mungu Mafundisho ya Neno la Mungu
6:Ujasiri
7;Samehe
8;Kuondoa Manug,uniko
9;Usizini
10: Uaminifu wa Sadaka
11:Kupenda Maombi na Mafundisho
12:Kuwa na Baba Wa Kiroho mmoja
13:Utubu.
14:Moyo wa Kuchukia Dhambi

Ujenzi wa Madhabahu Unatakiwa uwe hivi

Hitimisho
Kumbuka Lazima Ukubali Gharama kulipa Kama roho Mtakatifu atakavyokuuongoza unapoanza ujenzi wa Madhabahu yako

Wito
piga Simu za Pastor Richard Jioni saa 12 00 +255759861768

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.