SOMO:MAZINGIRA YA SHETANI ANAVYOMKAMATA MTU

SOMO: MAZINGIRA ANAYOTUMIA SHETANI KUKAMATA;
🌴🌴🌴🌴🌴🌴🌴🌴🌴🌴🌴🌴🌴🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳
Vitabu Rejea: Waamuzi;16' Matendo:6;8-15, Yeremia:26:👉🏿2Nyakati:22:1-9
__________________________________________________________________
Naitwa Pastor Richard
Nipo Morogoro Veta Dakawa
Kutoka Kanisa la Holy Spirit

Karibu Leo Nataka Nikufungue Akili yako Inawezekana Unateseka Lakini huelewi Shetani huwa Anatumia Njia Zipi ili Akukamate Na Akutumikishe na matatizo Kupitia Hili Somo Utapona Pakubwa Sana Ambapo umeteseka miaka mingi Sana

Karibu🙏🙏

MAZINGIRA maana Yake kila Kitu Kilichokuzunguka wewe.
KUKAMATWA Ni kuwekwa chini ya himaya ya utumwa wa Shetani Kutembea katika Tabia Zake.

1: MAZINGIRA YA KWANZA ANAYOYATUMIA KUKAMATA
Ni MAHUSIANO YAANI UCHUMBA AU MAPENZI.
Waamuzi:16
Delila aliweza Kuingiwa na Roho ya Shetani nakumuuza mchumba wake ili ajipatie Pesa Na Kwa Kutumia maneno mazuri na Vishawishi Mbalimbali vya Mapezi Samsoni Akawa Kipofu Hasikii Wala haabiriki mpaka alipojikuta Yupo kwenye matatizo kwa Sababu ya mapenzi

NINI FUNDISHO Wanaume/Wanawake Walioandaliwa na Shetani hutumia mazingira ya mahusiano na wewe uliyesimama na Mungu ili wakamate nguvu yako ya kuomba ndani yako nguvu ya maono yako nguvu ya Upendo na Mungu Utaanza kumuacha Mungu au kuacha Maombi kwa Sababu ya mahusiano wengine walifikia mpaka kuchukia kanisa na watumishi kwa Sababu ya Mapenzi Wasielewe wamekamatwa na Adui Tayari

Kujiondoa Usifanye haraka Kuoa au Kuolewa jiridhishe na Muombe MUNGU Sana usipate kinadelila.

2: MAZINGIRA YA PILI ANAYOYATUMIA SHETANI NI FAMILIA ZETU AU WATU TUNAOKAA NAO.
2Nyakati:1-9
Ahazia alikuwa mtoto wa Josephat Unapomsoma Huyu Josephat alikuwa mtu aliyempenda Mungu Sana lakini Baada Ya Kufariki alitokea Ahazia Ambaye aliuawa na watu aliokaa nao wakiitaji ule utawala na Uzao wa Josephat usiendelee Kumjua Mungu.

Katika Familia Asipotokea Hata mmoja akasimama Ni lazima Adui atawaua Kiroho Kama Ni Kwa Asitokee Hata mmoja watoto wasimjue Mungu wazazi wasiokoke lazima Shetani ataiua familia hiyo Kiroho Na Ukiamua Kusimama Simama haijarishi Mapito utakayokutana nayo elewa umawabeba Ndugu zako.

3: MAZINGIRA YA TATU: ANAYOYATUMIA SHETANI NI KUKUPA HOFU YA KILA UNACHOKIFANYA

Shetani Siraha Yake Kubwa ni Hofu Hii huwa Hali ya mtu Kukosa kuwa Anajiamini Anakuwa mtu Wa Kujidharau nakujikana mwenyewe

Hii Hali huwatesa watu Wasielewe ndio lango la matatizo Yote

4: MAZINGIRA YA NNE:KUTOKUWA UNAMSIFU MUNGU KUMSIFIA KWA MATENDO YAKE.

Shetani Amewakamata wengi watu huwa kazi kumsifia Mungu lakini Kuyasifia Matatizo na Mapito au Kusikia ujinga na Upuuzi Wanakuwa wa KWANZA mfano; mtu utakuta anasifia Tamthilia Mcheza mpira movie Mchumba wake Anasifia Mapito Lakini Kusema Amsifie Mungu Aseme Mungu Kweli Mimi kanibadilisha Mungu kanifungua Mungu Amenipa kazi Watu hawawezi kumbe Ni mazingira Ambayo Shetani alishawashika watu

Watu kumchezea Mungu tu kazi au Watoe vitu vyao wapeleke Madhabahuni kazi lakini kupeleka kwenye bar mpira mchumba na Mambo yasiyompa Utukufu Mungu  ndio kwanza wanapeleka unamfanya Mungu asijibu kwako kwa kutomsifia Mungu anapenda umsifie Msifie TU Mungu.

Pia cheza msifu Mungu kwa kucheza uone

5:KUTOKUSHUHUDIA NA KUWAVUNA WATU.
Shetani huaadaa moyo wako usione hata moja ulilotendewa na Mungu kila Siku ukilala Ukiamka unawaza Mapito yako TU hufikirii hata moja Alilokutendea Mungu kila Kitu  umefanya kwa Akili zako

Tambua unapomshuhudia Mungu na Kumtukuza Unafungulia Mungu Atende Kwako Unapoendelea Kubeza Ushuhuda Nakuona huoni mabadiliko toka umjue Mungu au uombewe Unakuwa Unamfanya Mungu Asitende Kwako akatende Kwa Wegine.

MTUKUZE MUNGU KUZA SHUHUDA ZAKE UNAPOFANYA HIVYO UNAMUAIMBISHA SHETANI NA UNAMSHINDA NA MATATIZO YAKE
______________________________________________________________________
______________________________________________________________________
______________________________________________________________________
SHETANI ANAVYOKUADAA NA KUKUPIGA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO

STEJI YA 1: ANAANDAA MAZINGIRA YA VITA
Kwa Kutumia watu kuwaingia ndani Yao (SHETANI Ni roho inayotenda kazi ndani ya watu

STEJI 2:ANAKUHAMISHA MAZINGIRA ULIYOYAZOEA ANAKUPA MAZINGIRA YAKE
Mfano ulikuwa mwaminifu wa zàka anakufanya usitoe yaani kila ukipata Pesa anakuelekezea matatizo uyatatue kwaza. Ambayo hayo matatizo mwenyewe ndio anayainua Ukimaliza Pesa unasema sitamuimbia Mungu. Usipoelewa Ndio Anakuwa Ameshakudhibiti.

Kama unammeo/mkeo mlikuwa mnapenda litaandaa chuki  na hasira ukikumbali kuyafata hayo mazingira Tayari Anakupinga

Kama ulikuwa na Afya Utaanza Kama MCHEZO naumwa Nahisi vitu vinatembea Ukishaingia TU kukubaliana nae anaanza kukutesa na magonjwa mpaka utoke lazima ukutane na Mafundisho Ya Neno la Mungu.

STEJI YA 3: HUMSHAMBULIA MTU KWA MATATIZO MATESO MBALIMBALI MPAKA ATOKE LAZIMA APATE MTU AMRUDISHE KWENYE MAZINGIRA SALAMA.

Hapa Sasa mtu hutakiwa atafute Neno la Mungu Arudi kanisani Ampende Mungu na Kuaza Kusali Mawazo Yake Yananjegeka kwenye nguvu za Mungu.

Kama ulikuwa huombi Anza Kuomba
Kama Zaka hutoagi Aza Kutoa
Kama ulikiri Mgonjwa Kiri uzima ndani yako
Kama ulisema hutaolewa SEMA nitaoa/Nitaolewa
Kama ulikuwa Umesema mme/MKE wangu Malaya SEMA mme/MKE wangu Ni mwaminifu.

Yaumbe maneno yako yawe na Baraka

HITIMISHO
Mnaofika Kupokea majibu Yenu Kupitia Mafundisho ya Neno la Mungu mkumbuke Biblia Notbook Pen mtakaa siku tatu kula utajigharamia pakulala papo Unapokuja njoo na Imani ya kuponywa

WITO
Share kwenye magroup mbalimbali watu Uwaponye

Kwa Kuongea na Pastor Richard
Piga +255759861768
Muda mpigie Jioni saa 12 00 mpaka8;00 usiku

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.