SOMO: NGUVU YA UPENDO

SOMO: NGUVU YA UPENDO

Waamuzi:16:15
1Samweli:18:22
Zaburi:18;1
YOHANA:21:15:18

UPENDO Ni kujitoa maisha Yako Kwa Ajili Ya Kitu unachokipenda.

KUPENDA Ni Kukichukua Kitu Kilivyo Na Kukiweka moyoni Pasipo Kuona Mawaaa

NAKUPENDA Ni Kuutoa uthamani wako maisha yako kwa Ajili Yake

KWANINI TUNAPENDA
1:Ni Tabia Asili ya Kimungu ndani Yetu iliyoumbika
2:Ni Kwa Sababu Kile Tulichokipenda Kisipotee Tukilee mpaka Kufikia Ndoto Zake
3:Kwa Sababu Sisi ni Daraja La Wengine

KWANINI TUKIPENDA TUMEPENDA

1:Ni Kwa Sababu Tumekikabidhi Kile Kitu Kitumiliki
2:Ni Kwa Sababu Ya UKweli na Uwazi Wetu
3:Kwa Sababu Ya Upekee wa hicho kitu

KUTOTOFAUTI KATI YA UPENDO WETU NA MUNGU ANAVYOTUPENDA

NDIO TOFAUTI ZAKE NI HIZI

1:Mungu Huvumilia madhaifu nakutusamehe bila kuchoka lakini Sisi huchoka
2:Upendo wa Mungu huaza Kwa Uwazi Lakini Sisi huaza kwa Kujificha.
3:Upendo wa Mungu Ni wakudumu Lakini Sisi ni Wamuda TU
4:Upendo wa Mungu hauoni Mabaya Lakini Sisi Tunaona mabaya
5:Upendo wa Mungu NI Wote Lakini Sisi Ni wa mmoja TU
Wengine hutawapenda Kama mkeo au mama yako.

FAIDA ZA UPENDO


1] Ni kwasababu ya Upendo tumeokolewa dhambini.


“Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa;” Tito 3 :4


2] Ni kwasababu ya Upendo tumemjua Mungu.


“Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.” 1 Yohana 4:7-8


3] Upendo umetusitiri wingi wa dhambi.


“Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.” 1 Petro 4 :8


4] Ni kwasababu ya Upendo tuna ujasiri hata siku ya hukumu.


“Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu.” 1 Yohana 4 :17


5] Upendo hufadhili.


“Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?” 1 Yohana 3 :17


6] Upendo husamehe.


“Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.” Wakolosai 3 :13


7] Kwasababu ya Upemdo tunaweza kuvumiliana.


“Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;… huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.” 1 Wakorintho 13 :4, 7


8] Upendo una nguvu ya kuvuta watu kwa Mungu.


“katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu, na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.” Tito 2:7-8


9] Upendo hutupilia mbali hofu na woga.


“Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.” 1 Yohana 4 :18


10] Upendo ni tunda la kwanza la roho.


“Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,” Wagalatia 5: 22


MAMBO YANAYOPIMA UPENDO WAKO
1:Uadilifu wako na Utakatifu
2:UKweli na Uwazi wa unachokipenda
3:Msamaha na Masahihisho wa Makosa mbalimbali
4: Uvumilivu na Unavyojitoa kwenye hicho kitu
5;Kukitii na Kukifata hicho ulichokipenda

MAMBO YANAYOJENGA UPENDO
1:Kutumia Neno kuwa Kiini Cha Mazungumzo Nakupenda Sana Kila unapongea au kuwa Karibu nacho hicho kitu

2:Kutumia Kiini Cha Neno Nisamehe Kila Unapokiona Umekikwaza au Kukikosea hicho kitu

3:Kutumia Kiini Cha Neno ANSATE kila Kinapokupatia kitu Chochote

4:Kutumia Kiini Cha Neno Uvumilivu Kinapokupatia madhaifu


@2021

Pastor Richard

WhatsApp number+255759861768


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.