MISINGI 10 YA UCHUMBA

SOMO: SHERIA KUMI ZA MAHUSIANO (UCHUMBA/NDOA)

Mithali;9;9 ,12:1

Kuna Dada mmoja Alifika Hapa Kanisani Akiwa Amejikatia Tamaa Hawezi Kuolewa Kwa Kuwa Umri Umefika Miaka 52 Anakaa TU na Mwanaume Miezi au miaka 2 Wanamuacha Akasema Anatamani Afunguliwe awe na mme wake maisha hayo amechoka nikamuuliza Ulishawahi kuwa na Angano la uchumba Akasema Mimi siijui Kama huwa Kuna Agano la uchumba nikamuuliza Tena huwa unawezaje Kujua Huyu Ni mme na huyu Anataka anipotezee muda Kumbuka Dada miaka 52 hajaolewa Kwa Kukosa kujua Agano la uchumba Baada ya Kufundishwa Sasa hivi Ameolewa na Alishatoa Ushuhuda hapa Lengo Ni kukutazamisha unaweza Ukawa Unateseka kwa Kukosa Kujua Umhimu wa kitu.Naitwa Mwalimu wa Wanandoa Pastor Richard
WhatsApp Number Pastor Richard+255759861768
Nipo Morogoro Veta Dakawa

HIZI NDIO SHERI ZA KUJENGA UCHUMBA MZURI WEKA SHERIA HIZI MOYONI.

1.       MUNGU
Katika Mwanzo Tu mahusiano yako Tafuta mwanamme/Mwanamke Anayemjua Mungu Na Anahofu Ya MUNGU
Ndani Yake mpime
a)Anaenda Kanisani na Anampenda Mungu
b)Hajihusishi Na Waganga wakienyeji na makundi mabaya Kama Walevi Vijana wasiojishughulisha.
c)Kumbuka Kitu Sahihi Cha Toka Kwa Mungu

Hii Amri Ya Kwanza Katika mahusiano Yenye Tija.


2.    UPENDO

Upendo tafsiri Yake kujitoa maisha yako kwa Ajili ya umpendae
Hapa utamjua mtu ukimweleza Kama wewe Mgonjwa Au Unatatizo Anavyokukumbuka Kama Utaona wewe hukumbukwi Hata mtu kukuonyeshea hisia zake Kwa Matendo Viashiria mbalimbali Ukawa huvioni.
Ukiendelea na mahusiano hayo unavunja Amri ya Pili na ndoa yako. Ukija Kuolewa nae utabaki unajuta kumbe ulivunja sheria


  3.      ROHO YA MUNGU
Unatakiwa Uwe na Roho wa Mungu Anaekupa Moyo was huruma sio moyo wa kumjeruhi mwezako hii Inawezekana mtu utakayempata Kama Ni mtu mwenye hofu ya Mungu
Utaona TU mkiwa marafiki hapendi Akukwaze wa kukuweka Kipindi kigumu Yupo wa hivi ukimpenda Mungu Ukawa mwaminifu wa zàka na Kumwabudu.


4.       KUJITAMBUA
Hapa namanisha mtu awe mwenyewe Ameweza Kujitengemea nakuyaendesha Maisha Yake mwenye Kutatua Changamoto zake mwenyewe hii Hata ukisema unaoa au Unaolewa Tayari utaweza Kujenga ndoa Bora na Yenye nguvu ya Upendo



5.       AGANO LA UCHUMBA/NDOA

AGANO la uchumba huwa Ni Kuweka Patano Kwa Bint Kutokuzini na mwanaume mpaka afate Taratibu hata Kama Unampenda Ufundishe moyo wako kuwa na Agano Kutokuzini na mwanaume na mwanaume Kutokuzini mpaka mmefata Taratibu za Nyumbani Kutoa mahari


Na Usiende Kukaa na mwanaume wewe Bint au Mwanaume kukaa na Bint Ambaye hajakutolea mahari


6.       MALENGO YA KUWA WACHUMBA NINI.

Hapa mnatakiwa mkubaliane na Kuwekana wazi mnavyopenda na Usivyopenda

Pia Muwekeane Mikakati na muda wa kukaa kwenye mahusiano TU maana mkikaa muda mrefu mtaanza Kuzini na mtachokana Mawazo yakuoana yataishia njiani mtaachana au mtaamua mkae hivyo hivyo bill ndoa nakujipa moyo au matumaini Pasipo kujua Shetani Ameshawapiga Kiroho.

Mara Nyigi watu wanaoanza mahusiano kwa Kuzini hata wakiingia kwenye ndoa mmoja Wapo ataendelea kuchepuka


7.       MAWASILIANO NA MAZUNGUMZO

Tafuteni muda wa Kuwasiliana na Kuzungumzia mahusiano yenu na mipango Yenu iliyobaki msikae TU mnaenda mawasiliano Hakuna Mazungumzo Hakuna

Hii Huwa Hatari Kwa Wanaotarajia kuingia Kwenye ndoa 



8.       KUSAMEHE NA KUTIANA MOYO

Kwakuwa mmependana muelewe Hakuna upendo Pasipo na Msahamaha na Hakuna msamaha Pasipo Na Upendo

Mnatakiwa mtiane moyo nyinyi Kwa nyinyi sio Msubiri wengine ndio wawatie moyo, .Ni wajibu wa wawili Kuishi na kutawaliwa na Msahamaha.


9.       KUJITAWALA HISIA ZENU

Mtu asipoweza kujitawala mwenyewe madhaifu Yake Ni kazi Kubwa kuingia wewe kwenye uchumba nae Uaze Kumfanya ajitawale hisia zake

Kama wewe ulikuwa ulishazoea Kuzini Kabla ya Kuwa WACHUMBA unatakiwa uitawale Kama Ulikuwa na hasira itawale hasira Kama  wewe  ulikuwa na Tabia Fulani Jitaidi kuikontro ili usimkwaze mwezako


10.   KUSAIDIANA

Kila mmoja anatakiwa awe msaada na ajitoe kwa mweza wake Kwa Kuwa Mmependana Basi mnatakiwa msaidiziane kwenye Changamoto mbalimbali


Na MUNGU WA MBIGUNI AWABARIKI


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.