SOMO: SEHEMU YA PILI YA KAZI ZA MALAIKA
ISOMO: KAZI ZA MALAIKA ✔️✔️Part 2
Karibuni Sehemu ya pili mwendelezo wa Somo Hili Uzidi Kujifunza Kwa Habari ya MALAIKA Kule mbiguni Tuliishia Kuwaona WAPELELEZI Kazi wanaoifanya Kule mbiguni.Naitwa Bishop Richard Naekuletea Somo Hili Kwa muongozo wa Roho Mtakatifu katika ufunuo wa juu Kaa Katika Uwepo ili unielewe.
1: MALAIKA WA MOTO
Hawa Nia malaika wanaohusika TU na Tanuru la Motoni na SAA nyigine huwatokea WANADAMU kwa muonekano wa moto mfano;Kutoka:3:2
Kutoka 3:2
[2]Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea.
Hesabu 16:35-36
[35]Kisha moto ukatoka kwa BWANA, ukawateketeza hao watu mia mbili hamsini waliofukiza uvumba.
[36]Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
Unapoona watu wa agano la kale walikuwa wakiomba Moto unashuka unateketeza Sadaka au mwali wa Moto hao walikuwa Ni Malaika wa Moto waliokuwa wakishuka nakuteketeza Sadaka.
Malaika wa Moto hushuka kwa misili ya Moto na huwaka nakushughulikia Kumfanya Mungu watu wamjue huwatokea watu katika nguvu ya kuwadhihirishia wamepata kibali kwa Mungu. Malaika Hawa hutenda kazi mbiguni na duniani kwa Watu walio na Mungu.
KAZI ZAO HAWA MALAIKA
1:Kazi Yao ya Kwanza Kuhakikisha Mtu Akipewa hukumu ya Motoni hutokea Kule mbiguni na kumchukua Yule mtu mpaka kwenye Tanuru la Moto.
2:Kazi Yao Ya Pili Huhakikisha ulizi unaimarika pale kwenye Tanuru la Moto kila roho inayotaka Kutoka wanapigwa wanarudi Motoni.
3:Kazi Ya Tatu Mungu huwatuma kwa Watu wake hapa na huja Kama Moto ili kuwasaidia katika mapambano ya Kiroho.
4:Kazi Ya Nne Malaika wa Moto Hushughulikia Kuzibeba Sadaka Kumbwakumbwa nakuzipeleka kwa Mungu kwa Ajili ya kupiga wakuu wa Anga wasizuie Sadaka hizo Zenye nguvu yaani kitu unachomtolea Mungu Kama nyumba kiwanja Gari mshahara maisha yako kwa Ajili ya mwingine Malaika Hawa lazima washuke wawe nawewe na kuibeba Sadaka wao huwa wananguvu na ni Moto kwelikweli hawana MCHEZO
MUONEKANO WAO
1:Hawa huonekana Moto na chechee Kali za Moto
2:Huwa wanabawa moja Kubwa kulia na jigine kushoto
3:Wanaonekana katika mapambano ya Kiroho ya Vita Waite utawaona
Hili Jeshi la Malaika wa Moto Ni Hatari kwa Shetani na Anga lilozuia majibu yako. Waite watayachukua haraka nakukuletea.
2: MALAIKA WA ZAMU
Hawa Ni Malaika wanaopangwa Kuongoza Ibada Kule mbiguni na Kuhudumu Kujifunza vitu mbalimbali za Ibada za Kule mbiguni mfano muogaza Sifa
KAZI ZAO HAWA MALAIKA
1: Kuhakikisha Ibada zinaenda Katika mtiririko uliomzuri mbiguni na duniani wanapokaribishwa ibada za duniani.
2:Hupanga Ibada ya duniani iwe na uwepo na Usikivu mzuri mtu aielewe ile ibada .
3:Hufurahi na Kuhudumu pamoja na Wachungaji wanaompa Nafasi roho Mtakatifu
4:Hawakai na watumishi wanaomnyima Uhuru roho Mtakatifu wanaofata miongozo ya kibinadamu Kama liturunjia pale Pasipo na roho Hawakai.
MUONEKANO WAO
1:Huonekana Katika Malaika kawaida lakini pia Huonekana Kupitia mahubiri Kama mtu Yupo na Roho Mtakatifu
3;MALAIKA WA WATOTO WACHANGA.
Hawa Ni Malaika wanaowalinda watoto wachanga na mama anaemnyonyesha Hawa Malaika ndio Huhakikisha Usalama wa mchanga mpaka anakua anakuja MALAIKA mwingine Ambaye huitwa mlizi.
KAZI ZAO HAWA MALAIKA WA WATOTO
1:Kumlinda mtoto mpaka akue
2:Kumtetea mtoto mdogo na hatari
3:Kumfanya mtoto aelewe Adui nakutoa ishara ya Julia
4:MALAIKA WA AFYA
Hawa ni malaika wanaoshughulikia Wagonjwa na Kuwafariji Kuwaponya
Kazi zao Hawa malaika
1:Kutibu watu nakufanya operation kwenye madonda mipasuko
2:Kubadilisha Tumaini la Mgonjwa nakumpa imani atapona
3:Hawa huongoza kushughulikia na Afya TU
MUONEKANO WAO
Huonekana Kama nguvu na imani imemwingia Mgonjwa nakuponywa
5:MALAIKA WA WAJUMBE
Hawa Ni malaika Wanaowapasha watu Habari mbalimbali
KAZI ZAO
1:Hawa malaika humjulisha mtu ujumbe wa Mungu
2:Hawa malaika humwinjia mtu mwenye kibali kwa Mungu
3: Hawa malaika husema na mtu Kupitia Maombi Neno Mtumishi wa Mungu nk
6: MALAIKA WA ULIZI.👉🏿
Hawa Ni malaika wanaosimamia mbiguni kuratibu shughuli za ulizi na hushuka duniani kwa mtu mwenye Kutembea na Mungu
KAZI ZAO WANAZOFANYA
1:Kuhakikisha ulizi wa maeneo Yote Kule mbiguni Shetani haingilii.
2: Kuhakikisha Mtu Anakuwa Salama Anapowaita waje
3:Kuharibu mitengo na Vikao vya Adui zako wanaotaka kukudhuru.
4:Ni walizi wa Maisha ya wokovu wako ukiokoka pepo watapingwa
7: MALAIKA WA UJEZI
Hawa Ni malaika wanaoratibu shughuli za ujezi Kule mbiguni na utuzaji wa mazingira Kule mbiguni.
KAZI ZAO WANAZOFANYA
1: Kuhakikisha mazingira ya yapo vizuri
2:Kila Siku Kudizain muonekano wa mbiguni
3:Hushuka chini wakiitwa na mtu aliyeokoka vizuri
8: MALAIKA WA KIFO
Hawa hudiri Kuchukua roho ambazo Mungu anaziitaji mbiguni
KAZI ZAO WANAZOFANYA
1:Huchukua roho za watu
2:Husimamia mtu anayekufa nakubeba roho Yake
3:Hawatendi Kazi nyigine Zaidi ya Kifo
4:Wao hawaui Wala hawaamuliwi na mtu isipokuwa Mungu.
MUONEKANO WAO
Huwa wanakuwa na Vazi Jeusi mabawa meusi
Ansateni Mungu AWABARIKI Kujifunza Kitu
Kaa Subiri Kitabu Cha Kazi ya Malaika
Naitwa Bishop Richard
Simu+255759861768
@2021 April 10
Maoni
Chapisha Maoni