LASIMU YA KANUNI


YALIYOMO
Sura ya Kwanza: Taratibu Za Ibada
Sura ya Pili UBATIZO
Sura ya Tatu MEZA YA BWANA
Sura ya Nne Mashemasi na Wazee wakanisa
Sura ya Tano Sadaka na Taratibu Zake
Sura ya Sita Mipaka na Wajibikaji wa Viongozi
Sura ya Saba Ndoa na Uchumba
Sura ya Nane Umoja na Ushirikiano

Sura ya TisaπŸ‘‰πŸΏMASHARTI YA KUJIUNGA UCHUNGAJI NA SIFA ZA WACHUNGAJI

SURA KUMIπŸ‘‰πŸΏ MAONO YATATIMIZWAJE



1:SURA YA KWANZA
πŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏTARATIBU ZA IBADA πŸ¦πŸ‘‰πŸΏ
Taratibu za ibada Ni miongozo mbalimbali za kanisa zinazohusiana na ibada Zetu ndani Ya Kanisa la Holy Spirit

Ibada Zetu zitaongozwa na Roho Mtakatifu Kufundisha na kuongoza ibada zetu

Ibada Zetu zitakuwa Kama ifatavyo

AπŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏIBADA KUU πŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏ
Jumapili 

ibada inaanza Saa 8:30-12;30(Saa mbili na nusu mpaka Saa Sita na Nusu

Hii ni Ibaada Yote Jumapili itaanza Saa mbili na Nusu katika muda huo Vjpindi vitaanza

Jioni ibada ya marudio itaanza Saa:4:00 mpaka Saa 6:00 Jioni(Saa kumi mpaka Saa kumi na mbili

πŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏ1:SUNDAY SCHOOL πŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏ
Sunday School itaanza Saa 8:30-9:30(Saa Mbili na Nusu mpaka Saa tatu na Nusu
Sunday Hili Ni darasa la Biblia na Kujifunza Biblia Litaunganisha Waumini Wote na Mwalimu wa Sunday School atatoa Nafasi ya maswali kuuliza Na Atashirikisha Darasa lake Kupima uelewa wa kile alichokifundisha.

        πŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏ2:SIFA,KUABUDU NA KWAYAπŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏ
Sifa na Kwaya 9:30-10:30(Saa tatu na Nusu mpaka Saa Nne itakuwa Kipindi Cha Sifa Kuabudu na Kwaya.

Kipengele hiki kitawahusu Wanasifa na Waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili waliotutembelea  na Kwaya Zilizopo ndani ya kanisa
Watapata Nafasi ya kuimba na Kusifu mpaka Saa Nne na Nusu.

           πŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏNENO LA MUNGU πŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏ
Neno la Mungu Kuanzia: Saa 10;45-12;15(Saa nne kasorobo mpaka Saa Sita Na robo muda wa mnenaji wa Neno la Mungu Anayekuwa Ameaandaliwa Siku hiyo Kunena ujumbe we Mungu kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu.

                πŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏMATANGAZO YA IBADAπŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏ
Mtangazo yataanza Saa 12:15 mpaka Saa 12:30(Saa sita Na robo mpaka Sita na Nusu.
MATANGAZO Yote ya Kanisa pamoja na utambulisho wa Wageni utafanyika kwa Mzee wa Kanisa wa Zamu Siku hiyo.
✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️🌏🌏🌏🌏🌏🌏🌏🌏
BπŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏIBADA ZA KATIKATI YA WIKIπŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏ

1:JUMATATU

Jumatatu Ni Kipindi Cha Vijana TU Kuanzia Saa Kumi mpaka Saa kumi na mbili jioni(Saa;4;00-6;00)

Darasa Hili litalenga Kijana mwenye Sifa ya Kujitambua nakujielewa Watapata Nafasi Kujifunza Changamoto  mbalimbali na Jinsi yakutoka kwenye Changamoto hizo za Vijana.

Atasimamia nakuongoza Kipindi Mzee wa Kanisa wa Vijana Anayekuwa Ameteuliwa na mchungaji wa kituo husika.

Watapewa nafasi Vijana Kuuliza maswali nakujifunza Kitu Kupitia maswali
Wataandaa makongamano na Semina mbalimbali

2:JUMANNE
Jumanne Siku ya Wazazi Wote wenye watoto Saa Kumi mpaka Saa Kumi na mbili(4:00-6:00)

Jumanne Wazazi Wote Watajifunza Maadili ya kikristo Kuwalea watoto na Jinsi Yakuwaongoza Kiroho hii Kwaajili yakuadaa watoto wenye hofu ya Mungu watakao enenda katika misingi ya Kiroho nakuwaokoa watoto Wetu kwenye maangamizi ya Dunia na utandawazi.

Mzee wa Kanisa upande wa   wazazi ataongoza Kipindi nakuwapa Nafasi wazazi Kuuliza maswali

3:JUMATANO
Jumatano itakuwa Ni siku ya Wanamaombi Kukutana Kanisani Muda Saa kumi mpaka Saa kumi na mbili.

Wanamaombi wataongozwa na Mzee wa Kanisa katika Sehemu ya Wanamaombi Wataombea Kanisa na nchi watu mbalimbali na mahitaji mbalimbali

4; ALHAMIS

ALHAMIS Ni siku ya Wanandoa Wote Watakutana Kanisani nakujifunza masuala ya ndoa na Ulezi wa ndoa Changamoto za ndoa

Ataongoza Mzee wa Kanisa aliyekatika Uogozi wa ndoa
Atawapa Nafasi Wanandoa Kuchangia hoja na maswali Kuligana Somo alivyoliandaa.

5:IJUMAA
Ijumaa itakuwa Siku ya Kufunga na Kuomba Kanisa lote masaa 12
Saa mbili usiku mpaka Saa Saba Usiku ibaada ya Maombi na Sifa itafanyika Kanisani kuombea kanisa,Amani ya nchi Yetu Uogozi wa Kanisa.

Maombi haya yataongozwa na Mchungaji itaanza Sifa Baadae Neno la Mungu Baadae Maombi kanisa Nzima litaomba

6:JUMAMOSI
Jumamosi itakuwa Siku ya Sifa na Mazoezi ya Kwaya Kuanzia Saa tisa kamili mpaka Saa kumi na mbili
Wanasifa na Wanakwaya Watakutana Kanisa nakuadaa  Sifa ya Jumapili na Taratibu za Ibada.

7; JUMAPILI
Jumapili ibada ya marudio itaanza Saa kumi Nakumalizika Saa kumi na mbili Jioni

Ibaada hii itaongozwa na Mchungaji 

✔️✔️✔️✔️πŸ‘‰πŸΌπŸ‘‰πŸΌπŸ‘‰πŸΌπŸ‘‰πŸΌπŸ‘‰πŸΌπŸ‘‰πŸΌπŸ‘‰πŸΌSURA YA PILI UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
 

Kwa hiyo kubatizwa ni kuzika utu wa kale "maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo" (Gal 3:27).

JINA:

Jina la Kiswahili na la lugha nyingine nyingi linatokana na kitenzi cha Kigirikiβαπτί΢ω (batiza maana ya Kufunika kuzamisha Kitu

UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU Ni NINI?


Jibu: 
Ubatizo wa Roho mtakatifu Ni nguvu ya mabadiliko anayoipokea mtu Baada ya kumpokea ROHO MTAKATIFU ndani yake

UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU

✔️✔️✔️✔️πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡
MAANA YA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU

  1. Ni tendo la kuzamishwa na kujaa Roho Mtakatifu. Mdo 1:4, 2:4.
  2. Ni tofauti na kuzaliwa mara ya pili. Yn 20:22; Mdo 2:4, 8:12, 1:4.
  3. Ni kipawa cha Nguvu kutoka kwa Mungu. Lk 24:49; Mdo 1:8; Lk 1:35.
  4. Ni ahadi kwa wote waaminio. Mdo 2:4, 39.
II. UMUHIMU WA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU.
  1. Imeagizwa katika maandiko. Ef 5:18, Mdo 1:4-5.
  2. Ni chanzo cha Nguvu za Kiroho:
    • Katika Huduma ya Yesu Kristo. Mdo 10:38; Lk 4:1.
    • Katika Huduma ya Kanisa la kwanza. Mdo 1:8, 2:4, 4:31, 33.
III. JINSI YA KUBATIZWA NA ROHO MTAKATIFU.
A. MASHARTI YA KUBATIZWA NA ROHO MTAKATIFU.
  1. Lazima uzaliwe mara ya pili. Awe Amebatizwa kwa maji mengi Yn 14:17; 3:5-7.
  2. Upende kujazwa na Roho Mtakatifu. Mt 5:6; Rm 15:16; 1Kor 6:11, 7:37.
  3. Mtii Mungu. Mdo 5:32.
B. HATUA TATU ZA KUPOKEA ROHO MTAKATIFU.
  1. Karibia kwa ujasiri katika kiti cha neema.Tubu nakuachana na njia za kale Ebr 4:16.
  2. Mwombe Mungu akujaze Roho Mtakatifu mtamani Roho Mtakatifu. Lk 11:10, 13.
  3. Msifu Mungu kwa Imani. Mk 11:24; Lk 24:53.
C. USHAHIDI WA KUBATIZWA NA ROHO MTAKATIFU.
  1. Kunena kwa lugha. Mdo 2:3, 10:45-47, 19:1-6.
  2. Ishara hizi zitafuata ukitembea katika Roho:
    •  Kuwa na uwezo wa kutenda kazi za Yesu. Yn 14:16-18, 16:14.
    • Kuhisi uwepo wa Mungu. Yn 14:16-18.
    • Kusikia vibaya kuhusiana na dhambi. Yn 16:7-11.
    • Kuwa na uwezo wa kushuhudia. Mdo 1:8.
    • Kuwa na ujasiri. Mdo 2:14-41.
    • Kujisikia kumpenda Mungu na watu. Rm 5:5.
    • Kuwa na uwezo na hamu ya kuomba na kuwaombea wengine. Rm 8:26-27.
    • Madhihirisho ya karama za Roho Mtakatifu. 1Kor 12:1-11.
IV. HITIMISHO - MAMBO MUHIMU KATIKA KUBATIZWA NA ROHO MTAKATIFU.
  1. HAMU: Uwe na hamu ya kubatizwa na Roho Mtakatifu.
  2. IMANI: Amini kuwa unapokea Roho Mtakatifu sasa. Ebr 11:16; Mk 11:24.
  3. MSIFU BWANA: Bwana anaonesha uwepo wake wakati wa sifa. Mdo 4:31.
  4. JIWEKE CHINI YA MUNGU: Jitoe kwa Bwana kila kitu kiakili na kimwili. Rm 6:13, 12:1

 

SURA YA 3:MEZA YA BWANA,

Moja ya maagizo muhimu ambayo Bwana wetu Yesu Kristo aliyatoa kwa wanafunzi wake na kwa kanisa kwa ujumla ni kitendo cha kushiriki meza ya Bwana, 

MEZA YA BWANA:
mathayo 26:26-28" Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu
27 Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki;
28 kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. "
Tukisoma pia...
 Yohana 6:52-56" Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule?
53 Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.
54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
55 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
56 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.
57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi.  "
Tunaona kuwa haya ni maagizo ya Bwana kwa kila mkristo kushiriki meza ya Bwana kikamilifu.

FAIDA ZA KUSHIRIKI MEZA YA BWANA IPASAVYO:
 
1. Kuitangaza mauti ya Bwana hata ajapo; 
1wakoritho 11:26 inaeleza umuhimu wa jambo hili kwamba tunapoumega mkate na kukinywea kile kikombe tunaitangaza mauti ya Bwana katika miili yetu wenyewe, hii inamaana kuwa tunakubaliana na lile jambo la kufa na kufufuka kwa Bwana Yesu pale msalabani vivyo hivyo na sisi tunayachukuwa yale mateso ya Bwana Yesu katika miili yetu( kwamba tunakubali kudharauliwa, kuchukiwa na hata kuuawa kwa ajili ya yake kama yeye alivyouawa).hivyo picha ya Kristo inajengwa ndani yetu wafilipi 1:29"Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake; "2timotheo 2:12" Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi; " Kwahiyo Huko pia ndiko kutangaza mauti ya Kristo.

2. Tunauimarisha uhusiano wetu na Mungu:
 1wakoritho 10:16" Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?
17 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.
18 Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu?
19 Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu?
20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.
21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. "
kwa mistari hii inaonyesha kabisa kuna mahusiano makubwa ya rohoni kati ya mtu na Bwana, pale anaposhiriki meza ya Bwana. Kama tu vile mtu anapokwenda katika madhabahu za mashetani na kula vitu vya mashetani ni dhahiri kabisa nguvu za giza zitamwandama huyo mtu, vivyo hivyo pia na kwa mtu anayeshiriki meza ya Bwana anashiriki pia neema ya Bwana na baraka za Bwana, na roho za unyemelezi za shetani kama roho za magonjwa, hofu, n.k. Mungu anazifukuzia mbali maana Bwana Yesu alisema mtu asipokula mwili wangu na kuinywa damu yangu hana uzima ndani yake.(yohana 6:53). kwahiyo tunapoula mwili wake na kuinywa damu yake tunakuwa na uzima ndani yetu kila siku.

3. Kupokea ufahamu wa kulielewa NENO la Mungu zaidi:
luka 24:13"
13 Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili.
14 Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia.
15 Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao.
16 Macho yao yakafumbwa wasimtambue.
17 Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao.
18 Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi?
19 Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote;
20 tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha.
21 Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo;
22 tena, wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi na mapema,
23 wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai.
24 Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona.
25 Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!
26 Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake?
27 Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.
28 Wakakikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, naye alifanya kama anataka kuendelea mbele.
29 Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao.
30 Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa.
31 Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao.
32 Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko? "
tunaona hapa umuhimu wa jambo lingine tena kuwa  watu hawa wasingemtambua Bwana kama wasingeumega mkate, vivyo hivyo na sisi kwa kufanya hivyo Mungu anaachilia Roho ya kumjua yeye na Neno lake vizuri siku baada ya siku pale ambapo tulikuwa hatumuelewi vizuri tunapata ufahamu mpya wa kumwelewa vizuri, hivyo ni muhimu kwa kila mkristo kushiriki meza ya Bwana.

JINSI YA KUANDAA:

Vitu vinavyohitajika ni  mkate usiotiwa chachu( yaani usiotiwa hamira), na uwe ni unga wa ngano, Ni vizuri kutumia ngano ambayo haijakobolewa iliyosagwa japo kwa mazingira ya sasa hivi ni ngumu kupata ngano ambayo haijakobolewa isiyochanganywa na chochote hivyo unaweza ukaenda tu masokoni kununua ngano na kwenda kuisaga mwenyewe mashineni kama wanavyosaga unga wa mahindi nusu kilo/kilo moja inatosha kwa matumizi ya muda mrefu, kwahiyo wakati unaanza kuandaa chukua unga mkono mmoja(sasa inategemea na idadi mnaokutanika kushiriki) idadi inapaswa iwe ni watu wawili na kuendelea haiwezekani kushiriki peke yako, kanisa ni kuanzia watu wawili na kuendelea.
ukishapima unga mkono mmoja, tia mafuta yoyote mazuri ya kupikia kama kijiko kimoja (wengi wanapenda kutumia mafuta ya mizeituni), lakini kwa huku kwetu yanayopatikana sana ni ya alizeti, kisha tia chumvi kidogo, kisha weka maji kidogo halafu kanda kama vile unavyokanda chapati, (angalizo : usitie hamira wala vyombo unavyotumia visiwe na hamira vioshe kabla haujatumia). 

ukishamaliza kukanda sukuma kama unavyosukuma chapati, usipoteze muda mwingi katika kukanda na kutengeneza umbo, maana unavyozidi kukawia unga utaumuka kutokana na hamira ya asili hivyo jitahidi kuwa haraka kidogo. ukishamaliza tia jikono usiweke chochote tena baada ya kuuweka jikoni, acha kama dakika mbili tatu, ili uwe mgumu wa kuvunjika ukishaiva toa. Na mkate wako utakuwa upo tayari.

Divai inayohitajika ni ile ya mzabibu, na sio fruto au juisi ya zabibu hapana, kilichotumika kushiriki kwa mitume na kanisa la kwanza ni divai(yenye kiwango fulani cha kileo ndani yake). Kama utahitaji divai hizi zinapatikana kila mahali hapa nchini kwetu, zinaitwa "Alter wine". zimetengenezwa maalumu kwa ajili ya kushiriki meza ya Bwana, ukinunua utaona zimechorwa alama ya msalaba na zimeandikwa "Alter wine". 
Kwahiyo baada ya kuandaa mkate wako na divai mkishakwisha kushukuru 

WATAKAO SHIRIKI MEZA YA BWANA

1:Watu Waliokoka na kusimama

2:Watu waliotubu 

3:Watu Ambao Wamejiandaa

4:Watu Ambao Wasafi moyoni

WATAKAOHUDUMIA MEZA YA BWANA

 1:Wazee wa kanisa

2:Wachungaji Wote waliowekewa Mkono na Askofu

3:Wataombea Mzabimbu na mkate kabla ya kuumenga Ni Wachungaji TU mzee wakanisa hataomhea

4:Itafanyika Mara mbili kwa mwezi mwazo wa mwezi na mwisho wa mwezi

🍈🍈🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳


 SURA YA 4:MASHEMASI NA WAZEE WAKANISA

MASHEMASI NI Wahudumu ndani ya Kanisa

Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Ufunuo wa Yohana 22:12 

Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia. Waebrania 6:10 

KAZI ZA MASHEMASI

1:Kuhakikisha Utaratibu unasimama vizuri 

2:Kupanga ratiba za ibada na usafi

3:Kuwaelekeza Wageni nakuwakaribisha

4: Kuwahudumia watu Kiroho na Kimwili kanisani

5:Kuielezea Taratibu nakusimamia utekelezaji wa Taratibu


SIFA ZA MASHEMASI

1;Awe mtu mwenye hekima

2:Awe anayejitambua Mwenyewe

3:Awe Tayari kufanya kazi mwenyewe bila kusukumwa

4:Awe na Ushuhuda mzuri ndani ya kanisa

1 Timotheo 3:10

[10]Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia.

πŸ₯¦πŸ₯¦πŸ₯¦πŸ₯¦πŸ₯¦πŸ₯¦πŸ₯¦πŸ₯¦πŸ₯¦✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️

WAZEE WA KANISA Ni Watu ngani?

Wazee wa kanisa Ni washauri na walezi wa kanisa Kristo

Huwa Wanapatikanaje✔️πŸ‘‰πŸΏHuteuliwa na Mchungaji Baada ya kuomba nakupewa Majina yanayopendekezwa na Waumini ROHO MTAKATIFU ndio huchangua Mzee wa Kanisa.

Matendo ya Mitume 20:17

[17]Toka Mileto Paulo akatuma watu kwenda Efeso, akawaita wazee wa kanisa.

SIFA ZA WAZEE WA KANISA

1:Awe na MKE/Mme mmoja

2:Asiwe mtu wa Tamaa ya madaraka

3:Awe mtu mwenye maamuzi Yakujenga kanisa

4:Awe mtu mwenye Ushuhuda mzuri

5:Awe mtu anayejua Kukaribisha nakushauri.

6:Awe amewekewa Mkono na Mchungaji

7:Awe mtu mtu anayependwa na Waumini

8;Awe mtu anayeongoza nakusimamia familia zake.


KAZI ZA MZEE WA KANISA

1:KUMSHAURI mchungaji katika Huduma

2:Kupokea migogoro nakutatua migogoro ndani ya kanisa

3:Kuhakikisha Misingi ya Imani inasimamiwa Kikamilifu

4:Kuijua Imani na Kuelezea Katiba ya Kanisa

5:Kufanya majukumu ya mchungaji endapo Kama hayupo

6:Kukemea na Kulinda Katiba ya Holy Spirit

7:Mzee wa Kanisa Ni Mtumishi wa Mungu anayefanya kazi zote za uchungaji

Yakobo 5:13-14

[13]Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.

[14]Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.


MASHEMASI NA WAZEE WA KANISA WATAPATIKANA KWA.

1:Kupendekezwa na Waumini Kisha Mchungaji kiogozi atamchangua Kuligana na ROHO MTAKATIFU atakavyomuongoza

2:Kila Baada Ya mwaka mmoja au Nusu mwaka watateuliwa Wegine na waliomaliza wataruhusiwa Majina Yao Kutuma ofisi ya mchungaji Kisha yatatangazwa kanisani 1/3 ya kula itahidhinisha kupitishwa


SURA YA SITAπŸ‘‰πŸΏSADAKA Na TARATIBU

SADAKA na ZAKA(Fungu la kumi)

Ni kitu Chochote unachotoa Kwa Ajili ya Mungu 


SIFA ZA SADAKA

1: Sadaka Isiyo ya Uovu

2:Sadaka Isiyo ya dhuruma

3:Sadaka itokanayo na jasho lako

4: Sadaka itokanayo na Shughuli zako

5: Sadaka Isiyo ya mikataba 

Usitoe Sadaka Yenye Ulemavu au Yenye Uovu.

6; Sadaka Kuutoa muda wako

7: Sadaka Yako itokayo moyoni usiladhimishwe

KAZI ZA SADAKA

1:Kujenga Huduma ya Holy Spirit na Kuendeleza maono ya Kanisa

2:Kuhubiri injiri nakuifanya ifike mbali

3:Kujiunganisha na Madhabahu hii

4: Kupokea Majibu na Kuifanya Kazi ya Mungu.

5:Zinabadili maisha yako nakukufungua.

6:Itaendesha Kanisa nakuanzisha miradi mbalimbali

7:Itaendesha maisha ya Wachungaji na familia za

Zaburi 20:2-3

[2]Akupelekee msaada toka patakatifu pake, 

Na kukutegemeza toka Sayuni.

[3]Azikumbuke sadaka zako zote, 

Na kuzitakabali dhabihu zako.


UTARATIBU WA matumizi itagawanyika Mara mbili 

__________________________________________________

MAKAO MAKUU NA KANISANI (TAWI)

1:Kutunza watumishi na waasisi 30%

2:Kujenga Kanisa na maendeleo 70%

30% itaenda kwa watumishi na waasisi  wa Kanisa 

70% itagawanyika 20% Itabaki kanisani 50% itatumwa makao makuu

3:Makao makuu watapangilia Kuendesha makanisa na kuendeleza makanisa .machanga

4:Makao makuu itasimamia mapato na matumizi Kuendesha kanisa

5;Kutaweka Taratibu za Uongozi wa kanisa kuwalipa waweka hazina kiasi kuligana na mapato ya kanisa

6:Makao Makuu Itakusanya 50% Kila Baada Ya Mwenzi Kutoka Matawi Yote 50% Itabaki Kanisani

7: Mafungu ya Kumi na Sadaka Zingine Zitabaki Kanisani Zitakazotumika Kujenga Kanisa nakuanzisha Matawi mengine Sadaka za Hiari ndio zitatengwa Zingine Zitatumwa makao makuu Zingine Zitabaki kanisani.

8;Kanisa linapofikisha watu 50 litaanza Kutuma makao makuu 50%

9:Muweka Hazina Kutoka makao makuu atazungukia makanisa kukangua matumizi na Udhibiti Taarifa na Utoaji wa Pesa  Yeye ataunda Tume ndogo Na Taarifa Zitafikishwa Kwenye Kikao Cha Viongozi makao makuu 

10: Kanisa litajiendesha Kupitia Sadaka na miradi mbalimbali

11:SADAKA Zote zitasimamiwa na mhasibu atakayeteuliwa na zitatengwa kwenye Account ya kanisa

AINA ZA SADAKA ZITAKAZOTOLEWA KANISANI

✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✨✨✨πŸŽ„πŸŒ³πŸŒ³πŸŒ³πŸŒ³

1:Sadaka Ya Shukuran: Imeandikwa Zaburi:116:17 Zaburi:50:14 1Wakoritho:14:16

Hutol

2:Fungu la Kumi (Zaka) Imeandikwa Mwanzo;14:20 1Samweli:8;17 Luka:18;12

Hutolewa katika Madhabahu Yako hii Kila Mwezi Asilumia 10%

Kila atakayetoa Fungu la Kumi ataombea mahitaji matatu

1:Mungu Kupitia Fungu la kumi hili lifungue..(Atataja mahitaji matatu yaliyomsumbua)

3:Sadaka Ya Ukombozi: Imeandikwa Kutoka:3:49_51 Yohana:3:16

(Hii Sadaka hutolewa na mtu mwenye matatizo Au Amefungwa Anaitaji kukomboa kilichofungwa atatoa Sadaka hii kwa mchungaji atamuombea

Ataomba mahitaji Yake akiwa Ameishika Sadaka na Amepinga magoti Kabla hajaito πŸ‘‰πŸΏπŸ‘‰πŸΏBaba Naitoa Sadaka hi katika Madhabahu yako ikaongee kwa Habari ya Ukombozi wa,,,,,(Atatamka matatizo yake)

Mchungaji Ataomba Hivi

Baba Nadhibitisha Maombi ya mwanao Kama alivyoomba Sadaka hii ikaongee kwa Habari ya matatizo Yake katika Jina la Yesu πŸ™ Amen πŸ™


4: SADAKA YA HIARI(Hesabu:15:3 Kumb;16:10 

Sadaka hii itatolewa kila Ibada zote Katika na ibada kuu mtu anatoa Chochote alichokuwa nacho kwa Ajili ya Bwana

5: SADAKA YA KUTEKETEZWA(Zaburi:51:16 Ayubu;42:8 Mwanzo:22:2-4

Hii huwa Sadaka ya Kutoa kitu Kikubwa Kama vile kiwanja nyumba gari nk unapeleka kanisani au mshahara wako 

Hii hutokea kwa kusikia Msukumo au Sauti au mchungaji Apewe Sauti na Mungu haitakiwi uitoe bila kuona hizo dalili. Unapoitoa utaongea Neno moja TU na Mungu atatenda

6:MALIMBUKO(Kutoka:22:10 Nehemia;12:44 Walawi:23:10

Kila utakapovuna au mavuno ya KWANZA mtolee Mungu Kama MALIMBUKO ya mavuno yako yatatolewa kanisani

7:SADAKA YA NADHIRI(Hesabu:30:3-10 Zaburi:116:14,18 Muhubiri;5;4-5

Hii hulenga mtu anayenena kuweka kiapo au ahadi atafanya Jambo na Asifanye kwa Mungu utatakiwa utimize ulichokinens nakukiongea


SURA YA 7 UCHUMBA NA NDOA

Luka 1:27

[27]kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu.

Uchumba Ni Hatua inayompeleka. Mtu kwenye ndoa

HATUA ZIFATAZO ZITAFANYIKA KUWASAINDIA WACHUMBA NDANI YA KANISA

1:Watafundishwa Masomo ya Uchumba Methali:12;1

2;Watahudhuria Darasa litakalofundishwa na Mwalimu wa Wanandoa

3:Watapewa Nafasi ya kuuliza maswali na Kuchangia Maoni

4:Mchungaji atatakiwa Aweke Kipindi Cha Wanandoa na Uchumba

5:Mwalimu wa Wanandoa Atatakiwa kuwa na Vitabu na Kusoma Nakala mbalimbali

6:Watafundishwa hatua na Taratibu zitakazowafikisha kwenye ndoa


HATUA ZA UCHUMBA

1:AGANO LA UCHUMBA

Hii huwataka Walengwa Wazini Wala kukaa mazingira tatanishi yanayoharibu Ushuhuda

WATAPITIA HATUA ZIFATAZO

a)Urafiki 

Katika Kipindi hiki  Watafanya yafatayo

πŸ‘‰πŸΏkuwekana wazi malengo Yao

πŸ‘‰πŸΏKutambulishana Kwa Wazazi na Viongozi wa Din

πŸ‘‰πŸΏKuelekezana Vitu wanavyovipenda na Wasivyopenda(Uwazi msifichane)

Kipindi hiki Unatakiwa uwe msiri TU

B) UTAMBULISHO KWA MCHUNGAJI

Hiki kipengele mtaenda office ya Mchungaji na Kumweleza mchungaji Urafiki wenu atawapa Taratibu na atakaa nalo kuwa Siri

C)UCHUMBA KUKAMILIKA.

Kijana wa Kiume ataenda Kutoa mahari nyumbani kwa Bint na mahari hutengemeana na familia na Utaratibu wao 

Mahari Ni utaratibu wa kibiblia

Mwanzo 34:12

[12]Mjapoongeza sana mahari na zawadi, nitatoa kadiri ya mtakavyoniambia, lakini mnipe huyu msichana, awe mke wangu.

Kutoka 22:17

[17]Ikiwa baba yake huyo mwanamwali akataa kabisa kumpa, atalipa fedha kama hesabu ya mahari ya mwanamwali ilivyo.

USIKAE NA BINT BILA KUFATA TARATIBU ZA KWAO


     )NDOA 

Ndoa Ni Muunganiko wa Watu wawili Wanapofanya Tendo la ndoa Jinsia KIKE na MME

HATUA ZA MASOMO YA WANANDOA

1: Watafundishwa Waliomo Kwenye ndoa TU na Wanaoingia

2:Mwalimu atakayefundisha Awe Ameoa na Anaushuhuda mzuri

3:Wanafunzi Watajifunza Jinsi yakuishi maisha ya Ndoa Yenye amani

4;Kipindi kitapangwa na kanisa

5: Mchungaji atateua Mwalimu wa Wanandoa kufundisha Masomo ya Ndoa TU 

πŸŒ²πŸŒ²πŸŒ²πŸ‘ŠπŸΌπŸŒ²πŸŒ²πŸŒ²πŸŒ²πŸŒ²πŸŒ²πŸŒ²

SURA YA NANEπŸ‘‰πŸΏUMOJA NA USHIRIKIANO

Yohana 17:21

[21]Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.

Waefeso 4:3

[3]na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.

WAUMINI WATAKUWA NA UMOJA NA USHIRIKIANO KWENYE JAMII

MAMBO AMBAYO WATAYOSHIRIKI NA UMOJA

1:Waumini WATAKUWA na umoja na wataunda vikundi mbalimbali vya maendeleo

2:Waumini na Jamii watashirikiana kwenye Mambo yote ya kijamii

3:Waumini WATAKUWA na umoja na mshikamano kushiriki Mambo yote ya Kanisa

4:MUUMINI Asiyeshiriki Kuwa pamoja na wezake kanisa halitamjua Wala kumsaidia

5:Waumini watatakiwa kuitikia na kushirikiana kwenye Shinda na Raha

6:Patakuwepo na Taratibu ndogondogo Zitakazoundwa kukizi mahitaji na Utekelezaji.


SURA YA TISAπŸ‘‰πŸΏ:MASHARITI YA WACHUNGAJI WANAOJIUNGA NA HOLYS SPIRIT


Mchungaji anaetaka Kujiunga na Kanisa hili atatakiwa Afate haya-:

SIFA ZINAZOITAJI

1:Awe na wito Ndani yake

2:Awe na Nia ya Kumtumikia MUNGU na Kujitoa

3:Awe Amesoma Thiolonjia

4:Afike makao makuu awekewe mikono na Askofu

5:Atapewa Masomo na Atakuja Makao makuu


SIFA ZA WACHUNGAJI WATAKAOSIMIKWA NA WACHUNGAJI KUSIMAMIA MATAWI

1: Mchungaji Awe na Wito 

2: Mchungaji Awe na MKE mmoja na mme mmoja

3:Awe Amekomaa Kiroho

4:Awe Ameisoma Katiba na Amelelewa kwa Karibuni huyo mchungaj

5:Asimikwe na Mchungaji aliyesimikwa nakuwekewa mikono na Askofu mkuu


AGALIZO :Hairusiwi mtu alazimishwe kazi ya Mungu Au Apewe tawi hajalelewa Kwanza.

KWA ATAKAETAKAE KUJIUNGA KUWA MCHUNGAJI KUTOKA MAKANISA MENGINE ATAFIKA MAKAO MAKUU MOROGORO VETA DAKAWA


SURA YA 10:🌲🌴✔️MAONO YA KANISA NA MBEMBA MAONO{2WAKORITHO:3:6)

Maono haya ya Kuanzisha Kanisa yalianza 2008 na Askofu mkuu Richard Julius Kushoka Mwaka 15/11/2016 Alifika Morogoro Veta Dakawa Kama Angizo la Mungu nakuanza Kusimamisha maono.Akiwa na mwanae wa Kwanza Wa Kiroho Felix Patrick mbena na mkewe Monica Michel mgute mwaka 2017 wakaanza Kusajili Kanisa la Holy Spirit wakiwa na  Vicent David Mihayo ili kufanikisha maono haya yasimame Mwaka 2018 RICHARD JULIUS KUSHOKA Alienda Kusoma Thiolonjia 2019 Alirudi nakuanza Kazi Akiwa na watu 15 Mwaka 2020 Kanisa liliongezeka nakufanya idadi ya waliopokea Huduma kuwa 30 Kwa hiyo Kuwepo Kwa Kipengele hiki kitaendeleza maono nakuyasimamisha zaidi

MOTTO πŸ‘‰πŸΏ✔️Moto wa Yesu ukawake kila Kona Zaidi Jana.

MAONO YANALENGA MAMBO MAKUU MATATU

1: Kuwa fundisha watu katika nguvu ya Roho mtakatifu ili watu wafunguliwe katika fikira zao na Ufahamu wao

2: Ukombozi wa Kiroho na MwiliπŸ‘‰πŸΏHii tutafanikisha watu tukiwafundisha Neno la Mungu Ambalo Hujenga fikira za watu nakuwakuza Kiroho.

3:KUONGOZWA NA KUFANYA KAZI NA ROHO MTAKATIFU πŸ‘‰πŸΏ✔️ Hii itawezekana mean watu kujitoa na kumtii Mungu Kuishi maisha yanayochukia Dhambi maisha yanayompenda Mungu 

MAONO YATATIMIZWAJE NA WATAKAOPOKEA HUDUMA{Isaya:11:2-6)

1:Kutambua Umhimu wa Kuongozwa na Roho mtakatifu

2:Kupenda Neno la Mungu nakumsifu Mungu mchezee Mungu TU

3:Kumtii Mungu nakuchukia Kukosana nae Kupitia Mambo yanayoonekana

4:Kuwa na SHAUKU ya Kuwaomba Roho Saba 

1; Roho wa Bwana :Warumi:8;11

2:Roho wa Kumcha Bwana:Luka,2:14

3:Roho wa Ushauri:1wakoritho:3:9

4: Roho wa Maarifa:Zaburi:112:1-2

5:Roho wa Ufahamu: Yohana:16:7-8

6:Roho wa Hekima:Muhubiri:7:12

7: Roho wa Uweza:Zaburi:50:15

5: Wachungaji wote wawe na Wito Na nguvu ya Kiroho


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.