SOMO: KIBURI NI CHUKIZO KWA MUNGU
SOMO;;KIBURI NI CHUKIZO KWA MUNGU PIA HUKUTENGA NA MUNGU KIACHE KIBURI HICHO.
Tufunue Biblia Tusome Wote kwa Sauti Mithali;16;18๐๐ฟZaburi:73;6๐๐ฟ1Samwel;17;28๐๐ฟLawi:25:19๐๐ฟLuka:1:51๐๐ฟ1Timoth:3;2
MUHUBIRI na Mwalimu Bishop Richard
Yupo mtu Alikuwa Anateseka Kila mchumba akimpata akikaa nae mwaka tu anamuacha kwa Sababu ya kiburi Yupo Mtu mmoja alikuwa Anapesa akawa Amekuja Kuombewa Kanisani Kutokana na Mazingira Kanikuta naanza nasali kwenye mti Akasema Kanisa lako Pastor Richard liko wapi nikamuonesha Nasali hapa kwenye mti alikuwa Akiitaji mme Kutokana na Mtazamo aliokuwa nao hakuukuta akaishia Kutembea mbure Kutokana na Dharau au kiburi Wapo watu wengi Sana wanateswa na viburi vya chinichini Wazazi wameongea wewe Wachungaji wameongea Kutokana na Kuinuliwa Kidongo au Kupata Nafasi Kidongo imewafanya wamekuwa na Kiburi mpaka Kanisani Acha nikuambie Kiburi ni Kibaya Ndani mwako Hupaswi Ufunge Kiburi
๐๐ฟ๐๐ฟ
Mithali 16:5
[5]Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA;
Hakika, hatakosa adhabu.
MAANA YA NENO KIBURI๐๐ฟNi Kitendo Cha Kujiinua na Kutaka Ukuu kuliko wengine
LENGO LA KUFUNDISHA Kumponya mmoja Yupo na ugonjwa huu
MTAZAMO WA SOMO watu wataponywa nakubadilika kwa kujua
Kweli
SIFA SABA ZA MTU MWENYE KIBURI
✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️
1. Hajui kujishusha hata kama amekosea.
''Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.-Mithali 13;10''
2. Maongezi yake mengi yamejaa kujisifia yeye.
'' Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa BWANA ni MUNGU wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani.-1 Samweli 2:3''
3. Hana utii pote panapohitaji utii.
''Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa-Luka 14:11''
4. Analofanya yeye tu ndilo sahihi lakini ya wengine yote hayafai.
''Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya KRISTO YESU ; -Wafilipi 2:3-5''
5. Halekebishiki.
''Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA; Hakika, hatakosa adhabu.-Mithali 16:5''
6. Anajifanya anajua yote.
'' Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti.-Mithali 16:25''
7. Hutaka kusikilizwa yeye tu huku yeye hayuko tayari kusikiliza wengine.
''Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.-Mithali 18:12
MAMBO AMBAYO UTAYAONA YANATANGULIA KUKUPA TAARIFA UMEVAMIWA NA TATIZO LA KIBURI
1;Utaanza Kuwa na Dharau Tofauti na ulivyokuwa
Ujue roho ya kiburi inakuja
2:Utaanza Kuwa Jeuri Chinichini Ukitumwa huendi ukiambiwa Hufanyi
Dalili hii ukiona mchungaji au wazazi wanakuelekeza ufanye uje Kanisani upambe wewe hupambi utoe viti hutoi ujue kiburi hicho
3:Kujiona unafaa kumbe hufai mbele za MUNGU
Utaanza Kujiona wewe unauwezo kuliko mwingine
4:Utaanza Kuwa Unawatukana watu
Utaanza Kuwa na Lugha ya matusi
5:Dhambi Utazifanya zote
Hutakuwa na Ujasiri wa Kuishinda Dhambi itakuendesha
6;UTAKUWA Ukifanya Kitu huku unatukana moyoni
๐ฅฆ๐KWA SABABU NGANI NAFUNDISHA KIBURI
NAFUNDISHA KIBURI Sababu Ni ulemavu wa Kiroho wa wakristo wengi Kwa Kanisa la Leo Kiburi kimezuia majibu ya wengi na Baraka zao Naamini watapona wanaoteswa nakiburi
NJIA YA KUTATUA
1;Ishi Maisha yenye upendo na wengine usiwaone wait Kama SI kitu
2:Kubali Kurekebishwa na ubadilike
3:Mtii MUNGU na Anaekuongoza Kiroho
4:Jifunze Kuipenda MAFUNDISHO Ya Neno la MUNGU
5:Jiombee rehema na kujiombea mwenyewe
USHAURI WA KIROHO
Kama hujaokoka Tumia namba Hizi nipigie +255759861768
HITIMISHO
Kiburi ni chazo Cha kumuasi MUNGU na Kumilikiwa na Shetani na mapepo
WITO
TUOMBE WOTE
Eeh Bwana Yesu Naomba ufute kiburi ndani Yangu Kwa Jina la Yesu ๐ Amen ๐
Share katika magroup
@2021 Pastor Richard
Nipo Morogoro Veta Dakawa
Maoni
Chapisha Maoni