SOMO: KARIBU YESU

SOMO👉🏿 KARIBU YESU HIVI VYAKO MWILI WANGU MALI ZANGU
Mathayo:16:8
UFUNUO:3:20

Basi Alikuwepo mtu Mmoja ameokoka anampenda Yesu Sana Siku Moja Yesu Alimtembelea Nyumbani Kwake Akabisha Hodi,,Hodii,,Hodii,,Akasema Karibu wewe Nani Akasema mi Yesu akamkaribisha Akampa chumba Self KILA kitu humo Yesu akasema okay Siku ya pili akasikia hodi akaenda kufungua akakutana nakipondo Cha Shetani akapingwa na Shetani na Yesu Yumo ndani ya NYUMBA Yake Siku Ya Pili Shetani akaja Akabisha hondi Akafungua mlango
Shetani alimpiga nakumtesa Yule mtu Siku 14 Yumo ndani Akakumbuka hivi Kwanini napingwa na Yesu ninaye Humu Humu ndani akamfata Akasema Mimi Yesu shetani ananitesa nawewe humo humu ndani hunisaidii Yesu Akamwambia Umenipa chumba hiki Kimoja nikae nami nalinda hiki ulichonipa Akasema Aah Sasa ukae na Sebuleni usiwe TU chumbani Yesu akawa Yupo na Sebuleni Shetani Tena akaja Siku Hiyo kabisha Hodi Akafungua Shetani Akamvuta nje kampiga Kweli alimtesa magumi akaondoka kwenda Kusema Kwa Yesu Tena naleo kaja kanipiga Mimi nilijua Kwakuwa Yesu upo Sebuleni utanisaidia Yesu akasema umeniambia Mimi nikae Sebuleni na chumbani sio nikae nyumba yote Akasema aaha mumbe nimekosea nimkabidhi Yesu ufunguo Yeye ndio Afungue Kama Kawaida Yake Shetani SI alishazoea kumtesa huyo mtu Siku Hiyo Kaja kampa Yesu uhuru wa kutawala Funguo magari  mashamba Watoto ndoa Afya nk akaja kubisha Hodi Yesu Akafungua Shetani alipomuona Yesu alitetemeka nakuaza kupingwa alipingwa Ikawa Mwanzo na mwisho huyu mtu kuteseka?

Yamkini nawewe Unaye Yesu ndani Yako lakini unapingwa kutokana Yesu umemkaribisha chumba Kimoja umemkaribisha eneo Moja kwingine Adui wanaingia kutokana Funguo za nyumba yako umekaa

Ushuhuda mfupi
Mimi kwangu huwa sifungi mlango au kuogopa mtu ataiba popote Nikienda huwa sifungi Iwe Simu Yangu siweki lock kwa Sababu mlizi wa Mali zangu nyumba Yangu Yupo Yesu Sio Kufuli.

Nikawa nipo katika Vita Watu Hapa nilipo wanatuma Majini uchawi wait kuipinga Huduma ya Moto wa Yesu Mimi nikawa napingwa TU napingwa Siku Hiyo nikamwambia Bwana Karibu umiliki nyumba Yangu Ndoa Yangu mwili wangu akili Yangu kila kitu Shetani saivi na uchawi wao wameshindwa Kwanini uteseke Mkaribishe Yesu

Karibu Katika SOMO .Karibu Yesu

MAANA YAKE: KARIBU YESU sawasawa Kumpa Nafasi ya kuingia kukaa kwenye Chochote unachokifanya uwe unaumwa uwe huzai uwe huolewi Mkaribishe Yesu

LENGO Ni kumponya mlengwa

Maono kuadaa Kizazi chenye nguvu ya kumtumikia Mungu.

SABABU ZINAZOMFANYA MTU ASIMKARIBISHE
1:Kwa Kujua Akiokoka Tayari Yesu anakaa ndani Yake na Mali zake
2:Kukosa Kujishughulisha na Neno la Mungu Kukosa uelewa wa Neno Karibu
3:Mapokeo Watu wanawakuta Wanasema Karibu Yesu moyoni Karibu Yesu maishani nayeye anakalili Asielewe Yeye Yesu Anamuitaji Kwenye Nafasi ngani labda unateswa na magonjwa madeni maroho MACHAFU nk

NJIA ZA KUTOKA  KWENYE TATIZO
1:Kwanza Jua Yesu unamuitaji Sehemu ngani chumba Kimoja au nyumba Yote Kama nyumba Yote mpe ufunguo wa nyumba.

2:Mpe Yesu uhuru akae na nyumba yako Yote Mali zote usimpe mpaka

3:Karibisha Wachungaji unapowakaribisha waambie Karibu muwe huru Baba hapa Ni kwenu. UTAKUWA umemuingiza Yesu kwenye nyumba yako Pasipo kujua.

FAIDA ZA KUMKARIBISHA YESU

1:Hutapingwa na Mateso au magonjwa
2:Hutashindwa Sababu atafanya uliyemkaribisha
3:Hutabaki ulivyo Utabadilishwa
4:Ongeza FAIDA Yako

HASARA UKIWA YESU HUMKARIBISHI.

1:Shetani atakuwa anakupa Kipingo kila Siku
2: Wachawi na Ufalme wa ngiza utakuonea
3:Utabaki na levo Hiyo Hiyo hutabadilika

Hitimisho
Nitaongoza Maombi nyanyuka usimame ulipo

NIFATILISHE
Eeh Yesu Naomba Unisamehe Siku zote nakulalamikia Kuwa Mimi mbona siowi mbona Siolewi Nasema mbona Mtoto sipati mbona huduma Yangu haikui mbona kazi sipati mbona Mimi mwizi wa Fungu la kumi kumbe nashindwa Kusimama au Kupokea kwa Kuwa sijawahi kukaribisha Leo nimejifunza Nasema KARIBU Yesu kwenye mahusiano Yangu KARIBU Yesu Kwenye Uzao Wangu Karibu Yesu...(Taja hitaji) katika jina la Yesu 🙏 Amen 🙏

Tumia Somo Hili kushare magroup matano Tu

Naitwa Bishop Richard
Simu ya Bishop Richard Kwa maombezi piga Jioni saa 12 00
+255759861768
Mwanzilishi wa Makanisa ya Roho Mtakatifu Tanzania
Moto wa Yesu makao makuu Morogoro Veta Dakawa

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.