SOMO: KANUNi ZA KUENDESHA UHUSIANO

SOMO: KANUNI 7 ZA KUENDESHA UCHUMBA WAKO.

👉🏿👉🏿Karibu Katika Darasa la Wanandoa Na Mahusiano Leo hii Nataka nifundishe Jinsi Ya Kuendesha Uchumba Wako Kwa Wale mliopo Kwenye Uchumba mlio na malengo ya Uchumba wenu Kufika Mbali Basi SOMO Hili linawalenga Mtulie msome Kwa Umakini Kwa UTULIVU.
UCHUMBA NI NINI? nipatano la watu wawili Jinsia ya Kiume na Kike linalowapeleka Kuanza Maisha ndoa na Uchumba huwa umeshatambulika kwa wazazi Kama haujulikani huo uitwa Urafiki..
MNAPOFIKIAGA Kwenye Uwe umeamua mwenyewe na usiingie kwa kuiga Shuhuda kwa Kuwa unaona wezako wanaolewa hapana Tulia kabla hujaingia ili Kuepuka maumivu na majeraha kwenye moyo wako Sababu ukikosea utaumizwa nakusalitiwa.
Naitwa Bishop Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa
Karibu UJIFUNZE mbinu za Kuendesha Uchumba Wako mpaka ukafikia ndoa.

👉🏿👉🏿MAMBO YAKUZINGATIA KUENDESHA UCHUMBA WAKO ILI USIVUNJIKE AU KUISHIA NJIANI  FANYA HAYA.

A:Ruhusu Mungu Akupe MKE/MME Usiruhusu Akili Zako Zikupe MKE/MME.👉🏿👉🏿👉🏿🥦🥦🥦🥦🥦🥦🥦🥦🥦🥦🥦

Mwanzo:2:21 BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,

Watu wengi Leo Hawataki Mungu awape wachumba au mke/mme wanataka wapate watu Kwa Akili zao Mapenzi ya Mungu Ndani Yao yamefutika Adamu au Eva hawakutengemea Kama Watakuwa MKE na Mme Kwa Kuwa Adamu aliangalia Mtu wa Kufanana nae hakuona wote walikuwa na Tabia moja Akili zake ziliona Bora zikae bila ndoa kwa Kuwa wanawake wote Adamu Aliona Tabia moja na Eva nae hivyohivyo Lakini Mungu Yeye aliwaona wanaweza kukaa Pamoja na Mungu akamfata Eva na kumkutanisha Adamu  Sasa hapa ili uitimize hii Njia
1:mpende Mungu na kuwa Mwaminifu katika Madhabahu Yako kutoa na Kuitunza Madhabahu Yako.
2:Usiweke mtu kichwani na Usipende Pesa penda Utu.
Kadiri utakavyopatia kupata mchumba ndivyo hivyohivyo utaweza Kuendesha Uchumba Wako mpaka kwenye ndoa.

B:WEKENI MISINGI YENU INAYOTUNZA USHUHUDA WENU KWA MUNGU NA KWA JAMII
Mwanzo:2:25 Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya.
Isaya : 8:16 Ufunge huo ushuhuda,

Wewe Kama Kweli Umekusundia Mahusiano Yenu Yafike Mbali hutaharakisha kuujua Ubint wa mweza wako na ujana wa mweza wako mtajenga Msingi Wa Kutokuzini  na mtafata hatua zinazowataka mfike nyumbani Pande Zote mbili ili wawatambue wazazi na waelewe Uchumba wenu nakufata mtakavyopangiwa.

Bint ukikosea hii step ya Pili utakuja kuolewa na Mwanamme ambaye hajatulia Mwanamme mzinifu Wala hutakiwi ukimbie au uwe na haraka maana ndoa huhitaji utulie na Upate kitu Sahihi
Hapa unatakiwa uweke wazi kwa mwezako
1:Hatutazini mpaka ukatambulike nyumbani utoe mahali.
2:Mimi Nataka Uchumba wetu tuujenge kwenye Hofu ya Mungu wote mpatane mnahofu ya Mungu.

C:MHESHIMIANE KATIKA MAZUNGUMZO YENU

Mithali :14;31 Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake;Bali yeye awahurumiaye wahitaji humheshimu

Kwa Kuwa Uchumba huwakutanisha watu wanzima wawili wànaojitambua huwa panakuwa na shida Sana endapo Hawa wakaleta Pesa Kazi cheo Elimu zao kwenye Uchumba wao heshima na mwendelezo wa Uchumba wao huwa unaishia njiani kwa Kuwa kila mmoja anajivunia kitu na anaona Amependwa Kwa anjili Ya Pesa Kazi Elimu Yake kumbe Hupaswi uchanganye Uchumba na Pesa au Kazi Tunza muda wa Kazini Ajibika Ukija Kwenye Uchumba Ajibika Kama mchumba.

D:MTANGULIZE MANENO YA MAHABA MNAPONZUGUMZA AU KUCHAT 

 Wimbo;4;1:Tazama, u mzuri, mpenzi wangu,U mzuri, macho yako ni kama ya hua,

Unapoongea na Mchumba Wako Anza Na Neno Baby Wangu Mme wangu Nakupenda Sana Kisha Endelea Sasa

Usiongee Neno Bila Kutamka wewe Nakupenda Sana wewe Mzuri Msifie Katika Hata hatua anayoifanya Hata Kama Ni ndogo Kama Amekupa Chochote SEMA Ansate Tengenezeni Uchumba wenye Upendo Sio mnachati Kama Sio wachumba au mnaongea Unaanza vipi niaje umeenda kwa Bi mkubwa hapana. ongeeni Kama watu mnaojiandaa Kujenga Ndoa


E:MTANGULIZE IBADA MBELE SIO KAZI AU PESA MBELE.

Wafilipi : 2;17 Naam, hata nikimiminwa juu ya dhabihu na ibada ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote

Muweke Msingi wenu msikose ibada na muombee Uchumba wenu mkae mkijua Shetani hapendi ndoa kwa hiyo Kipindi Cha Uchumba ndio Cha kuomba msikae mnaangalia Wachungaji wawaombee.ombeeni Uchumba wenu.

F:MSIKOSE BABA WA KIROHO NA HUYO ANATAKIWA HATUA ZOTE AJUE.
Hapa hutakiwi uwe na mababa wengi uwe na baba mmoja TU utakayemweleza nakukusaindia Kuongoza Uchumba Wako ufike Mbali hapo ndipo utatoa Fungu lako la Kumi kwa Baba Yako huyo na utatunza Nakupenda Madhabahu hiyo usitoe Fungu lako nje ya Baba Yako wa Kiroho huyo ndiye kashika Baraka zako.



G:TENGENI MUDA WA KUKUTANA NA KUPANGA MIKAKATI YA NDOA

Msikae muda mrefu mpo kwenye Uchumba mwaka mmoja TU au miezi Fugeni ndoa msiruhusu Shetani akapitia Lango Hilo la kukaa muda mrefu bila ndoa mkaingia KUZINI na kuchokana
Tumieni Somo Hili muelimishane nakuongozana Vyema

Naitwa Mwalimu Wa Wanandoa Pastor Richard
Simu piga Jioni Saa 12:00 Kwa +255759861768

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.