SOMO: NGUVU YA AKILI

🥦🥦SOMO; NGUVU YA AKILI🥦🥦
Tufunue;Mathayo:22:37 Zaburi;119;66,1wakoritho:1:19

Luka : Mlango 24:45 Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko

             ;UTAGULIZI:

Akili Ni kiungo chenye nguvu ya kumponya mtu au Kumwagamiza mtu Akili huenda sawa sawa naunavyoiendesha wewe mwenyewe Ukiendesha Akili YAKO uwe Mpumbavu kila Kitu utakuwa Mpumbavu Ukiendesha Akili YAKO uwe na Maarifa utakuwa na Maarifa. Akili inasehemu Kubwa Sana Ya Kufanya Maamuzi na Hatima ya Maisha YAKO na Imani YAKO ikaamini Kama Akili ilivyoongoza. Sasa Kwa Kuwa Mungu Anatupenda Ameamua Azifunue Akili Zetu Kwa Kutuletea Somo Hili Karibu ujifunze nguvu ya akili YAKO inavyoweza kukuponya Mimi Naitwa Pastor Richard Ninaishi MOROGORO VETA DAKAWA.Simu zakuongea nami piga Jioni SAA 12;00 Namba+255759861768


MAANA YA AKILI : Ni uwezo wa Kupambanua Vitu unavyoviona na Kuvisikia  Kisha kuruhusu Maamuzi yaliyosahihi ndani YAKO yaamue. Matokeo ya uamuzi wako huwa tunaita Akili.

Kwa Hiyo Akili inaweza Kukubali uteseke Au Usiteseke inaweza Kukubali uwe masikini au Usiwe masikini.


MAMBO YANAYOWEZA KUKUJULISHA AKILI YAKO INANGUVU.

1:Unachokifanya au Kazi Unayoifanya inakutambulisha Akili yako.

2:Watu au Kundi Ulilonalo au Marafiki zako inakutambulisha Akili yako

3:Mazungumzo yako na Matamshi Yako Unapoongea Yanakutambulisha

4:Mazingira Unavyoweza Kukabiliana nayo Yanakutambulisha Akili.

5;Familia na Wewe mwenyewe Unavyoweza Kujiongoza mwenyewe.


HAYA MAMBO MATANO YATAKUFANYA UELEWE AKILI YAKO INANGUVU AU INAMADHAIFU.

Huwezi Ukashindwa Kujiongoza Mwenyewe au Kufanya Kazi au Kujisimamia mwenyewe Katika maisha halafu wezako wakaweza Kufanya Kazi Wakaweza  Kujisimamia ukajiliganisha nao. Ikiwa wewe Unatembea na WALEVI wa pombe halafu unatengemea uache pombe Ni ngumu au Unatembea na Kundi la watu ambao hawajaolewa au wameachika wewe nae ukawa unatengemea uolewe huwa Ni ngumu Akili ya mtu aliyeoa inaenda sawa na aliyeoa akili ya kijana aliyesingo inaenda Sawa na Usingo wake..

Kwa hiyo Akili hukutambulisha wewe unauwezo ngani na mchango ngani kwa Jamii iliyokuzunguka.


FAIDA YA NGUVU YA AKILI

1:Akili Huweza Kukuvusha vipindi vingumu.

2:Akili Huweza Kukupa Maarifa ya Kutatua Tatizo.

3:Akili Huweza Kukutenganisha Kati Ya mtu Mpumbavu na mwenyehekima

4:Akili Huwa Utambadilisho tosha kwa Watu na Jamii.

5;Akili hukabili Mazingira Yote na haina hofu.


HASARA YA KUKOSA NGUVU YA AKILI.

1:Huwezi kuvuka

2:Huwezi Kukabiliana na mazingira.

3:Utaitwa Majina mabaya Sifa mbaya ndio utapewa wewe.

4:Utaishi Kwa Mateso na utashindwa kuamua

5:Hutatawala Chochote hata baskeli tu.


WITO 

Tumia kiungo Cha Akili Ili uvuke 

HITIMISHO

Kaa na watu wenye nguvu ya Akili Ambao unaona wanakabiliana na mazingira ili ukue

By Pastor Richard


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.