MOYO ULIOKOSA UJASIRI WA MAOMBI
SOMO:MOYO ULIOKOSA UJASIRI WA MAOMBI.
Mathayo:5:8 Mathayo:6;21 Matendo:8:21 Mithali:23:17
Naitwa Bishop Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa.
Muda wa Kuongea Na Bishop Richard jioni Saa 12:00 Simu+255759861768
MOYO ULIOKOSA UJASIRI WA KUOMBA: huwa Ni moyo uliozungukwa na majukumu mbalimbali ya Kimwili moyo ulioelemewa na Dhambi .
Watu wanaoteswa na huu moyo huwa Ni ngumu wao kusema moyo wao uwaongoze kuomba hauna hiyo tabia au UJASIRI utamkuta mtu Huyu akitaka kuomba TU huu moyo utamkumbusha majukumu ya Kimwili Ambayo anapaswa ayafanye kwa hiyo nguvu ya uwepo inatoweka UJASIRI unatoka Moyo huu humkosesha mtu MAJIBU yake.
MOYO HUU HUWA MTU UNAMFANYA HIVI FATILIA UJUE HUU MOYO ULIOKOSA UJASIRI WA KUOMBA.
1:Huu Moyo Humkumbusha mtu Dhambi au Kumhamasisha Afikirie Dhambi.
Utamkuta mtu Yupo katika Maombi Unafikiri anaomba kumbe Anadaiwa au Kuna Mchumba wake kanisani baadala Aelekeze akili yake Maombi atawaza wale anaowadai au Mchumba wake Yupo Kanisani na Kama ameingia Kanisani Jana alizini akatubu moyo huu huendelea kumuelekezea yule mtu nakuona Dhambi Sio kuona mguso wa Bwana au Mkono wa Bwana.
Yohana:13:21-22 Mithali:23:17
2:Huwa Moyo Umejawa Upizani na Vikwazo vingi vya Kufanikiwa.
1Thelonike;2;17-18 Mithali;23:33
Hujawahi kuona Mambo Yao kila afanyalo linakizuizi halifanikiwi shida huwa moyo huu ULIOKOSA UJASIRI.
3:Moyo huu Hutawaliwa na Tamaa za Mwili;
Galatia:5:16-17 Rumi;8;5-7
Watu wenye moyo huu huandamwa na Tamaa za Mwili Kuzini ulevi nk hawawezi kuzuia moyo huu huwa na nguvu kwao.
4:Huwa na Moyo uliokata Tamaa na Maisha
Mithali;13:12
Huu moyo huwaongoza watu kukata Tamaa
5:Nafsi Kuumizwa
Zaburi:77:1-4
Huwa wanasalitiwa huwa wanaumizwa na Kutapeliwa haki zao Hupitia misukosuko kami hii niliyoitaja moyo huu ndio huwafanya.
6;Huwa Hawana Muda Wa Kuomba
Luka:21:34-36
Kutokana na Moyo huu kuwaweka bize na utafutaji hawana Muda wa Kuomba au kusali wakirudi huko wamechoka.
7:Hawajui Umhimu wa Kuomba.
Hawawezi Kuwa na UJASIRI wa Kukaa katika Maombi.
Maoni
Chapisha Maoni