SOMO: FURAHA NDANI YA NDOA

SOMO: JINSI YA KUFANYA UWE NA FURAHA MAISHANI Mwako

Karibuni Wanandoa Tuongee+18 Naitwa Mwalimu Wa Wanandoa (Pastor Richard)

Mithali:15;8-22 Nehemia;12:16-18  Luka:15:7

MAMBO YANAYOKUFANYA UWE NA FURAHA NDANI YA NDOA YAKO.
B
1:SAMEHE.
Kiukweli huwa vitendo vingine ndani ya ndoa kuvi vumilia huwa kazi au tu katika maisha ya Jamii iliyotuzunguka Hali Ambayo huondoa furaha ndani Yetu nakuweka huzuni na chuki Kati yetu lakini ukiwa na moyo wa Kusamehe Utakuwa nafuraha.

2:CHUKUA MADHAIFU YA MWEZAKO UYAFANYE YAKO SIO UMCHUKIE.
Mkeo au Mmeo unapomuona Anakosea kosea elewa kuwa hicho kinachomkoseha huitwa udhaifu sio kweli Kusema Mmeo au Mkeo akakufanyia Kitu hicho milele asibadilike elewa Atabadilika tu na Atakuja kuushinda huo Udhaifu Ukiishi na watu Wachukulie Kama walivyo usipende Kuyaweka moyoni MADHAIFU Ukaona Kama Anafanya kwa Kusundi.Utaishi na Furaha.

3:JIKUBALI WEWE NI PEKEE NDIO MAANA UMEOLEWA  AU UMEOA.
Usipende Kujiliganisha ndoa yako au maisha yako na mtu mwingine Wala usifikirie Ujana wa ndoa utakapoanza ukaanza kuona ndani ya ndoa Mmeo Kama hakuelewi hakusikilizi Anaanza kubadilika ukawa na presha elewa huo ni ujana Kama mkeo Anaanza kukununia kukuchukia ujue wewe Ni mtu special uliyeadaliwa katika maisha Yake usiwaze au Kuaza kuwaeleza watu wa nje Tulia hicho Kipindi kitapita.

4:ISHI LEO ✍🏼UONE YA LEO✍🏼 SIKIA LEO✍🏼 USAMEHE LEO✍🏼 UPENDE LEO.
Wanandoa Wengi hupenda kuishi na kuyabeba Yaliyopita wanaanza kuyaingiza Kwenye maongezi au Kusikia Taarifa zilizopita au Kupenda Na Kuigiza upendo uliopita Wewe Nimesema Ukiitwa Tu Mwanandoa Heshima Kubwa Sana Ambayo wewe Ni Kuelewa Mungu amekupendelea Kwanini akupe Leo mme Akupe Leo MKE asikupe Kesho. Kila Jambo Lione Machoni Pako jipya juu ya mwezako usione limepita. Utapata Furaha daima.

5:SHUKURU
Jiwekee Utaratibu unashukuru kila Anachokufanyia mkeo au Mmeo Wanandoa Wengi wanasema SI Wajibu wake Namshukuru wa Nini Lakini asijue Anaondoa Furaha Kati Yao.

6:UWAZI
Weka wazi na umweleze UKWELI Usije ukalongwa Ukaingia kwenye ndoa halafu ukawa unamficha Mmeo  au Mkeo yaani akija Kujua Furaha inatoweka.

7:Imani
Jiwekee imani ya kuwa ndoa Yako Ni mfano ndoa yako inaupendo ambao Ni wakipekee Jiwekeeni Utaratibu wa Kuomba Pamoja MKE na mme. Kuongozana Katika Misingi Mzuri wa Wokovu ili hata Familia Yenu imjue Mungu.

Basi Naishia hapa ubarikiwe Mwanandoa Tuongee+18

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.