SOMO:NINI MAANA YA SADAKA
SOMO: NINI MAANA YA SADAKA NDANI YA KANISA
Mathayo:5:22-25 Waebrania:13:16 Hesabu:7:23-50 Kutoka:10;12
Zaburi:119:108.15:8 Yohana:3;16
Soma hivi vitabu
KARIBU UJIFUNZE NINI MAANA ya SADAKA NA KUNA AINA GAPI NA Umhimu wa Kuwa nasadaka.
Naitwa ✍🏼 Moto wa Yesu au Pastor Richard wa Morogoro veta Dakawa
Inawezekana huwa Unajua sadaka Ni kumtolea Bwana au nikitu unachokitoa Kwa Kanisa wagonjwa nk.
Tutaanza Kuona Sadaka Ni Nini?
Sadaka Ni Nini?
Sadaka huwa Ni kitu chochote unachoweza kukitoa au Kukifanya Kwa Ajili kitu Fulani : Pia Sadaka Ni Ibada Kamili inayokufanya kile unachokiamini kijibu kwako .Sadaka hutolewa Kulingana na maelekezo na utaratibu wa eneo husika unapotolea sadaka.
Mfano Sadaka ambazo huhitaji muongozo na maelekezo
1:Zaka;(Fungu la Kumi na Ukombozi,Kuteketezwa)HIZI huwa hazitolewi bila muongozo wa Mchungaji au anayekulea Kiroho.
SADAKA HUTOLEWAJE.
Sadaka Ni Siri yako na Madhabahu unayoitolea
Sadaka hutolewa Kwa mrezi wako wa kiroho au Kanisani.
Hizi huwa Sadaka Zote unazozitoa Kwa Ajili ya Mungu.
UNAPOTOA SADAKA HIZO KWA MCHUNGAJI NA KANISA ZINAENDA WAPI;
Matumizi ya Sadaka husimamiwa na Baraza au Halmashauri ya Uundaji wa Kanisa husika kuazia ngazi ya Taifa inakuwa na Katiba Ambayo inagawanyisha
1:Lipo Fungu Hufanya kuendesha Kanisa
2:Lipo Fungu la Kusafirisha Huduma na kuwasaindia watumishi wanaoanza kazi
3:Lipo Fungu linalomhudumia Mchungaji na Familia Yake
4;Lipo Fungu linalofanya Kuendesha nakufungua miradi Mbalimbali mfano: RC.KKKT. FPCT. T.A.G nk Ambayo yameshasimamisha miradi.
5:Lipo Fungu huwasaidia wahitaji wagonjwa yatima na wagane na wajane.
USIPOTOA SADAKA TAFSIRI YAKE.
Hutaki kanisa la Bwana Liendelee Unataka life au libaki hivyohivyo wasijenge au kununua viti au vyombo
UNAPOTOA SADAKA HIZO
Unafanya Kazi Kubwa nakuendesha Huduma na Mchungaji mwenyewe Azidi kula Kukuombea na kuifanya kazi ya Bwana bila Kuwaza atakula Nini?
KWANI NI LAZIMA NITOE KANiSANI AU NIMPE KUHANI.
Hesabu;3;49
KWA UPANDE MUNGU SADAKA=Hutolewa Kanisani au Mchungaji wako. ukiipeleka nje ya maeneo hayo Unafanya Makosa na Unajiungamanisha na Ibada za Majini au mashetani.
MFANO WATU WALIOPATA MALI KWA SHETANI
Pesa zao au sherehe zao hutoa kwa Yatima wajane wagonjwa Sadaka ya Shetani hutolewa nje ya Madhabahu ya Mungu Kanisani au Mchungaji.
HUWA TUNAWAJIBU WAKUTOA KUWASAIDIA YATIMA WAJANE.
Lakini ukae utambue chochote unachokitoa kwa Watu wenye shida Yatima wajane huwa Ni SHUKURANI au Kusaidia kitu ambacho hicho huwa tofauti na Sadaka
Maana Sadaka inatolewa kwa unachokiamini kiwe ufunguo wa Kupokea
MAJIBU yako.
MAANA YA SADAKA ✍🏼Ni Madhabahu ya Mungu(Mahusiano Yako na Mungu)
Ukikosa hapa ujue huna mahusiano na Mungu.
AINA YA SADAKA
Kwa Mungu Maangano Yote mawili yanafanya Kazi Lakini Kuna Sadaka Zilizo za mhimu wewe MKRISTO Uzijue.
Kuna Sehemu Tatu za Sadaka
1:ZAKA(Sheria Lazima Utembee hivyo Kama Mungu alivyoangiza)
Hizi Sadaka huwa Ni
a) Fungu la Kumi
b)Sadaka ya Ukombozi
c)Sadaka ya Kutekezwa
d)Sadaka ya Kibali
Sadaka hizi tunasoma(Malaki;3;9-10,Yohana;3;16 Hesabu:3;
2:AHADI(Huwa Kifungo Kikubwa usipotimiza)
Hizi huwa Sadaka zinazofuta ulichoahidi mbele za Mungu
1:Sadaka ya Nadhiri
2:Sadaka ya SHUKURANI
3:Sadaka ya Amani
4:Malimbuko
Sadaka hizi tunasoma Nehemia; Malimbuko;10:37 Mathayo:6:3 Hesabu;30:9-11
Luka : Mlango 11
41 Lakini, toeni sadaka vile vya ndani, na tazama, vyote huwa safi kwenu
3:HIARI(Huwa hazimfungi mtu Wala Hakuna Sheria ya Utoaji)
Hizi huwa zinatolewa Kila Ibada mnapokutana nyumbani kwa Bwana
1:Sadaka inayotolewa Jumapili
2:Sadaka Kujitoa Kutumika Kwa Mungu.
3:Sadaka ya Kujitoa kulisha wachungaji na Kupamba kanisa
4:Sadaka ya Unayonguswa utoe bila kuambiwa
Maoni
Chapisha Maoni