SOMO:MAMBO YAKUONGEA WACHUMBA
SOMO:DARASA LA WACHUMBA WANAOENDA KUFUNGA NDOA SI MUDA MREFU
UTANGULIZI
Mabinti wengi huwa Wanafurahia Sherehe ya harusi na Akili Zao Kuzielekeza Kuhakikisha Siku Yao ya Harusi na Kujiandaa Kwa gharama nyigi Juu Ya Sherehe. Hali ya Upokeaji wa Bint na Kijana huwa tofauti Bint Huona Tukio la Sherehe Ni Kubwa Kuliko ndoa anayoenda Kuijenga.
Nipo Hapa Leo Kwa Ajili yakuwaponya wachumba Ambao Wanaenda Kufunga Pingu za Maisha Hakuna Kitu Ambacho Kitaharibu Ndoa Yenu Endapo Unaingia Kuolewa au Kuoa Hamjawekana wazi
1;Historia Zenu
2:Familia Zenu Zilivyo
3:Imani zenu
4:;Kazi Zenu na Upatikani wa Uchumi wenu.
5:Mipaka na Usiyopenda
6:Malengo Yenu ya Kuishi Pamoja
Usioe au ukaolewa na Mali au Kazi au Pesa Olewa na mtu olewa na utu utaifanya ndoa Yako iendelee mbele na mfanikiwe
HAYA MAMBO HAKIKISHA HUJARUKA HATA KIPENGELE KIMOJA YAONGEENI NA MUWAKANE WAZI KABLA YA TUKIO LA NDOA.
1:HISTORIA ZENU.
Vijana Wetu wengi Huwa hiki Kipengele wanakipuuza wakikutana huko mjini kila mmoja anakazi Yake Hawana muda wakupeana historia zao.
Kabla hujaolewa au Kuoa Mchumba wako lazima aweke wazi historia ya maisha Yake kwa Kuwa mmeamua Kwenda kuanza maisha Yenu itawasaidia Kudumu Katika Nguvu ya Upendo.
2: FAMILIA ZENU.
Vijana wengi huficha mazingira Yao ya Nyumbani kwao hasa wanapopata mabinti wenye Kipato hushindwa Kuwapeleka mabint au wachumba wao kwa Wazazi huishia hewani na Bint Kwakuwa hujataka kujua ukiingia kwenye ndoa kumbe umeingia familia ya kichawi au inayoandamwa na uganga nk lakini mkipeana historia za Hali halisi ya wazazi Wenu mtafanyika mabadiliko kwa Familia Zenu Mbili.
Usifiche wazazi wako hata Kama Ni chizi au mlemavu mpeleke mchumba wako amjue mama Yako Baba Yako Usiolewe au Kuoa mwanamke anayekuficha wazazi wake.
3:IMANI ZENU
Hakikisha kabla hamjafunga ndoa mnaulizana nakuwekana sawa katika IMANI Kwakuwa mmekuwa Kitu KIMOJA haipendezi wewe unasali kanisa Jigine na mmeo kanisa pegine hii huwa mbaya Sana Katika kuharibu maisha Yenu kwa Kuwa Shetani hutumia mafarakano Yenu na Makosa kukazia kuharibu milango Yenu ya Baraka.
Wanandoa nisheria ya ndoa za kikristo lazima Iwe Imani moja MUNGU mmoja mme mmoja MKE mmoja Kabla hamjafunga ndoa mpatane mtasali sehemu moja.
Ni lazima Narudia Lazima msiingie kwenye ndoa mnaabudu sehemu tofauti tofauti
4; KAZI ZENU
Wekeni Sawa Ratiba ya Kazi Zenu mpaka wa Kurudi Nyumbani muda sahihi unaotoka Kazini Kazi ngani unayoifanya Weka wazi kwa Mchumba wako Mambo yahusuyo kazi Yako Kaeni muogelee mpage ratiba sahihi Ambayo haitaleta maswali au maumivu Kipindi mtakapokuwa mmeingia maisha ya ndoa
Wekaneni wazi mshahara wenu Matumizi ya Pesa Zenu mpage Pesa Zenu zote zijenge maendeleo ya familia Yenu mnaoenda Kuanzisha.
5;KIPATO CHENU NA UPATIKANAJI WA PESA
Mimi Ni Pastor Richard Nimekuwa nikikutana na mabint wengi wameolewa wasielewe Kipato na Mali Zote mmewe alizipataje Kumbe Ni Jambazi lakini mwanamke hajui Ni Vyema Mnapofunga ndoa weka wazi Kipato Chako na Kazi inayokuingizia Pesa Uchumi
Ukificha Ukaona Nachoongea hakina Maana ndoa Yako haiwezi kudumu MWEZAKO akijua hukuwa mkweli
6: Mipaka Yenu
Mmekutana Wote Wa Wakubwa Na Sasa mnaenda Kuwa Kitu KIMOJA Tabia ulizokuwa nazo na MWEZAKO yanayomkwaza uache Kila ulichokuwa unakifanya utamshirikisha MWEZAKO Mtapeana mipaka ya unayopenda na Usiyopenda
7:Malengo Yenu Kwa Pamoja
Tayari mmeshaanza Kuishi Pamoja mmeoana ili iweje mikakati Yenu ya Kufikia Lengo na HATUA Zipi mnazipanga muaze nazo ili Kufanya Lengo lifikie Kusudi.
Haya Ndio wachumba muogee Kabla hamjafunga ndoa Ili ndoa isije Ikawa na Tatizo Ndoa huhitaji Mwanzo mzuri kwenye Uchumba ili Kujenga ndoa ya Kuigwa
Naitwa Mchungaji Richard
Nipo Morogoro ✍️ Veta Dakawa
Maoni
Chapisha Maoni