SOMO:KUKUA KATIKA MAADILI YA MUNGU
SOMO: CHANGAMOTO YA KIJANA KUTEMBEA KATIKA MAADILI YA MUNGU
Tufungue Biblia Zetu: Mathayo:19:20-22,✍️Torati:22:16
✍️Mwanzo:21:14-20✍️1wafalme:1:1-4✍️Zaburi:37:25
Karibuni Katika Mafundisho ya Neno la MUNGU Popote ulipo Kila Kona Ya nchi Kwa Majina Yangu Naitwa Mchungaji Richard Ninaishi Tanzania🇹🇿 Africa
Leo Naongelea Changamoto Mbalimbali Tunazozipata Vijana Katika Maadili yakutembea na MUNGU na Jinsi Ambavyo Tunavyoweza Kujinasua Sisi Kama Vijana: Tukadumu Kutembea Katika Maisha Yenye utaratibu wa Kitakatifu Mbele Za MUNGU.
Sisi Vijana Tunapaswa Tujitambue Na Kuelewa Mambo haya YAFATAYO Yatakayotuongoza Kuishi maisha Yenye Maadili mbele Za MUNGU.
MAMBO MATATU YASHIKE KIJANA ILI UTEMBEE KATIKA MAADILI YA MUNGU
1: HESHIMA MBELE ZA MUNGU:
Ninaposema heshima mbele Za MUNGU namanisha Muonekano wetu Nyumbani Kwa Bwana Ushiriki Wetu Katika Nyazifa Mbalimbali ndani ya Kanisa Kijana Unaheshimu nafasi Yako uliyo nayo ndani ya Kanisa Unaifanya Kazi Kwa Moyo Wote au Mpaka Usukumwe Au Unalazimishwa.
Kazi ya MUNGU inatupasa tuiheshimu na Tujitoe Kufanya Kija wewe Hupaswi uwe ndani ya Kanisa uachie Wazee wafanye kazi Wakati wewe Upo chukua heshima Watu wafurahie uwepo wako ndani ya Kanisa na nje.
2:UAMINIFU MBELE ZA MUNGU
Ninaposema Vijana Tunapaswa Tuwe waaminifu kwa MUNGU Vijana Sisi ndani ya Kanisa Ni mhimu Sana Cha Ajabu Kijana kila Jumapili unachelewa KANISANI Wegine ndio kwanza Jumapili haendi KANISANI kwa Kuwa hajawahi Kuambiwa Ahubiri Kanisani
Kijana unatakiwa umwamini MUNGU na ufanye Kuwa pumziko la nafsi Yako acha Kusuasua Katika Utoaji wa Fungu la Kumi Acha Kujiweka nyuma Kuwa kihelehele wa Kwanza Kwa Yesu Baraka Zote wewe ndio uwe wa Kwanza Usiaze kuwaachia Wazee Wakati Upo wewe Kijana mwezangu.
3:NIDHAMU MBELE ZA MUNGU.
Ninaposema NIDHAMU simanishi Kuwa hauna Nidhamu namanisha Nidhamu Yako mbele Za MUNGU ukiwa unaenda Kanisani unavaa nguo zenye Nidhamu au Unavaa tu Ukiwa Kanisani unakaa kinidhamu ukiwa Kanisani Unanidhamu kwa Wazee au wazee wakija wamechewa ibadani huwapishi viti Ukiangizwa na Baba Yako wa Kiroho unatenda
Wapo Vijana Kanisani Akienda Hana Nidhamu nguo Ambazo agezivaa Yupo Disco au Kumbi za harusi au Sherehe Anakuja nazo Kanisani ukimwagalia Bint anaheshima Zake lakini uvaaji wake TU unamfanya kila mtu ndani ya Kanisa amtafiri vibaya. Kijana Anaenda Kugombana na mtu huko nje Anakosa Nidhamu unajikuta Matendo Yako na Njia zako unachafua Sifa nzima ya Kanisa Kutokana ukiwa huko nje kijana ugomvi Ni wako Lugha chafu Ni wewe dharau watu Ni wewe unajikuta Unaharibu Imani na Sifa ya Wewe Kuitwa unamaadili mazuri kwa MUNGU.
MAMBO MATATU YANAYOKUFANYA KIJANA UPITE NJE YA UTARATIBU WA MUNGU
1;MUDA WA KIJANA
Kijana Anamuda wake wa Kuwa Kanisani muda huo ukipita ataanza Kuwaza nje ya Kanisa pia Kijana Bado muda wake unavitu vingi unajikuta Yupo Kanisani lakini Hayupo kiakili Kanisani. Kijana huvutwa na Dunia na Changamoto Mbalimbali humfanya ziuharibu muda wake na Mungu.
Kijana unapaswa Ujijegee muda wako na usiufanye muda wako mwingi uwe nje ya Mungu Kaa Tulia na Mungu.
2:RATIBA YA KIJANA
Kijana Yupo ndani yakanisa lakini anaratiba zake nyigi Kijana Yupo Kwenye Maombi lakini Bado anaratiba nyigine Kijana Changamoto Kubwa kwenye ratiba Yake IPO nje ya Mungu muda Wote. Hata Kama ataingia Kanisani Bado ataratibu shughuli Zigine nje ya Kanisa.
3:MAAMUZI YA KIJANA
Kijana Anamaamuzi Yake yaliyo nje ya utaratibu wa Mungu Kijana Anamaamuzi Yake yaliyo nje na Mwelekeo wa Maisha Yake Kijana Changamoto Kubwa kwenye Maamuzi yaliyosahihi.
HITIMISHO
Kila kijana Ni Wajibu Kuweka muda ratiba na Maamuzi Sahihi kwa Mungu
Tuepuke Kutembea nje ya utaratibu wa Mungu ili kujiwekea Sifa Nzuri kwa jamii na kanisa.
Wito
Tumia Namba HIZI Kuongea na Pastor Richard Piga Jioni saa 12 00
+255759861768
Maoni
Chapisha Maoni