SOMO: VIPINDI VITATU VYA KUFAULU KWENYE NDOA YAKO
SOMO:VIPINDI MHIMU UTAKAVYOVIPITIA MWANANDOA UINGIAPO KWENYE NDOA.
Mehali:14:1-5 Waefeso;5;20-25
KARIBUNI Katika Wanandoa Tuongee+18
Wakubwa tu na wanaojiandaa kuingia Kwenye ndoa au waliopo ndani ya ndoa.
Naitwa Pastor Richard
Simu Ya Kuongea Nami Pastor Richard+255759861768
NDOA HUHITAJI SEMINA NA DARASA LA KILA SIKU LEO TUNAONGELEA VIPINDI VITATU VYA KUFAULU KWENYE NDOA YAKO.
Kuna Mambo matatu ukiyavuka hayo Basi utaitwa mshindi wa ndoa Yako
1:KIPINDI CHA UTOTO KATIKA NDOA YENU.
Katika kipengele hiki KILA mmoja anahamu na mwezake na hamu ya kuishi maisha ya ndoa kwa hiyo Kipindi mtaitana Baby Sweetheart My Lotion KILA Aina ya maneno mazuri mtafurahiana nakucheka.
Kipindi hiki huwa bado Mambo yapo motomoto ya Kuolewa au Kuoa
Hiki Kipindi huwa ndio yakuaza kujuana Vyema Tabia Zenu ndani ya ndoa huhitaji Mfanye haya Mambo mawili;
a)Muelekezane na Kurekebishana.
b)Kuchunguza Tabia ambazo za kukemea kwa mwezi wako.
c)Muombe MUNGU nakuongozana Kumjua MUNGU.
Hiki huitwa Kipindi Cha utoto sababu KILA Kitu mnakuwa wageni halafu kudanganyana kuchukiachukia bila sababu.
2: KIPINDI CHA UJANA WA NDOA YENU.
Katika Ndoa hufikia Kipindi mnaanza kuchokana Tabia maana utamwambia mtu hatakuelewa utatamani akufanyie aliyokuwa anakufanyia Hakuna hatafanya Kauli zinabadilika Hata changamoto zinaongezeka maneno ya watu yataingia na Wegine watakuambia umuache Wegine watatuma sms kwa Makusudi ili wawagombanishe Mmeo atabadilika mkeo nae atabadilika.
Ukiona Kipindi hiki ufanye haya
1:Vumilia na Zidisha upendo kwake
2:Muombee Kwa MUNGU
3;Usiruhusu Mtu akuletee maneno uyapokee.
4;Usielewe au Kuamini Hakupendi mbali nikipindi tu.
5;Usimrudishie Matendo mabaya wewe Endelea kuwa Kama zamani.
Ukifanya Hivi utavuka hiki Kipindi huitwa Kipindi Cha ujana kwa kuwa mnakuwa mmeshazoeana kwenye ndoa KILA mwanandoa Tabia zake alizokuwa anazificha anaanza kuzianika.
3: KIPINDI CHA UZEE WA NDOA YENU.
Hiki Kipindi huwa mmeshakomaa kwenye maisha ndoa mmevuka hivyo Vipindi ndoa Yenu imetikiswa haijavunjika Shetani Amefanya KILA mbinu Wapi.
Huyu ndio huitwa mwanandoa AMBAYE ameipigania ndoa Yake ufanye Nini ufikie hapa.
1:UAMINIFU Mwamini mweza wako 100%
2:MPENDE MWENZI WAKO 100%
3:YATUZE MADHAIFU YAKE
4:USIWAELEZE NJE KASORO ZENU ZITATUENI WENYEWE.
5:TUNZA SIRI ZA MWEZAKO USIMSEME VIBAYA.
HITIMISHO
Je ndoa Yako IPO Kipindi kipindi kipi?? Endelea Kuipigania ndoa yako ufikie kwenye uzee
WITO
Wanandoa Tuongee Na Kupeana Semina Kila Mara Ili Kujenga Ndoa Zetu
Maoni
Chapisha Maoni