Somo: Mahusiano Kati ya Maombi na Imani
SOMO: MAHUSIANO YALIYOPO KATI YA MAOMBI NA IMANI.
Tufunue Biblia Zetu:Waebrania:11:1-20 Mathayo:15;20-30,
1Timotheo:1:5-13
Imani: Ni uhakika wa Kupokea na kuwasilisha kiroho kuleta Matokeo ya kimwili.
Maombi; Ni mawasiliano ya Kupokea na Kutoa haja ya kitu kiroho kuleta kimwili:
MAHUSIANO;
Maombi hutengemea imani na imani hutengemea maombi
Huwezi Kupata Matokeo ya unachokiomba Endapo hauna Matarajio ya unachokiomba.
Huwezi Kupokea majibu Endapo maneno yako unayotamka Ni yakukata tamaa lakini ndani yako Imani ikawa haijakata tamaa
Kumbe Neno linaleta Matokeo ya unachokiamini Kwa MUNGU sio Imani ndio inaleta Matokeo Imani Ni uhakika unachokiamini Neno Ni Uhakika unachokitamka ndani yako.
Mfano wewe ukawa huolewi maneno yako mengi yakawa nitaolewa Tena ndoa yangu itakuwa Kubwa Kile unachokitamka kitatimia lakini ukawa unaamini utaolewa Kinywa Chako ukawa unatamka Kuolewa Ni mpango wa MUNGU Mimi nishajikatia Tamaa ya Kuolewa Kupitia Maneno yako hutapokea hata uombeajwe.
CHAKULA CHA KUKUZA IMANi
1:Shuhuda
2:Maombi
3:Neno la MUNGU
4:Sifa na Kuabudu
5:Mafundisho yanayokupa mwanga.
VITU VINAVYOUA Majibu YAKO Usijibiwe
1:UZINIFU
2:Wizi wa Fungu la Kumi
3:Hofu
4;Kukosa Mafundisho ya Neno la MUNGU
5:Kukosa Maombi.
VITU VINAVYOKUFANYA UJIBIWE
1:moyo wa Toba
2:Ujasiri na ushujaa wa kuvuka Mapito
3:Uaminifu wa Kutoa Fungu la Kumi
4:Maneno ya kujitabiria mwenyewe
5;Kuwa na Mlezi wa kiroho na Madhabahu Kupitia huyo mchungaji unatoa Fungu la Kumi kwa Uaminifu.
UNASHAURIWA
Fanya maisha yako ya wokovu yawe na Madhabahu moja na Mlezi wako we kiroho utakaye kuwa unamueleza anakuongoza kiroho na Tulia katika Madhabahu moja ili ufanye MUNGU akuhudumie usiwe na walezi wengi wa kiroho.
HITIMISHO
Fanyia kazi Masomo yanayokuwa yanakuinjia utaponywa roho yako Nafsi yako na utapokea.
WITO
Chukua Muda kurudia SoMo hili Mara tatu ulielewe
Simu za kuongea nami Bishop Richard Piga Simu+255759861768 Jioni Saa:12;00
Maoni
Chapisha Maoni