SOMO:MAMBO YANAYOVUNJA NDOA

SHULE YA WANANDOA NA WANAOJIANDAA KUINGIA.

SOMO: MAMBO YANAYOVUNJA NDOA NYINGI AU KUTOELEWANA KWA WANANDOA

MWALIMU; PASTOR RICHARD
Nipo; Morogoro Veta Dakawa
Simu+255759861768 Kwa ushauri na msaada piga Jioni 12;00

Haya nayoenda kueleza unatakiwa uwe makini nayo ili kuifanya ndoa Yako iwe Bora na yakuingwa.
Tusimame mithali;14;1,
2Yohana:1
10 Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu,

1: MARAFIKI,WACHUMBA,NA MAWASILIANO YA SIMU ZISIZO NA FAIDA.
Vijana wengi wanaingia kwenye ndoa wanajua ndoa nikuvaa shera na suti hawajui Ni maisha mapya yanayoitaji ujenge Safu mpya sio marafiki uliokuwa nao kabla hujaolewa au Kuoa na uagalie Hata watu utakaoanzisha urafi nao.

✍️✍️UNASHAURIWA✍️✍️
Uwe na marafiki wenye hofu ya Mungu, Wanaozilea ndoa zao vizuri,Wenye ushauri mzuri wa Kiroho na kimwili.
Badilisha laini zako na vunja laini ya zamani uaze mawasiliano na watu wapya Kabisa hakikisha Kama ulikuwa na wachumba au na mawasiliano ya Siri achana nayo.

HATUA HII UTAKUWA UMEPONYA NDOA YAKO
Ukiacha marafiki na wachumba au mawasiliano ya zamani ndoa Yako haiwezi Kuwa na Amani Hata siku moja utalalamika kila siku

2:FEDHA (UCHUMI)

Tatizo jigine la Wanandoa linawaumiza Kichwa na hujaribu kulitatua kwa Akili zao Ni suala la Fedha Matumizi mabaya ya fedha Matumizi ya fedha Bila kushirikishana  pia Uchumi wao kuyumba na kuteteleka.

UNASHAURIWA.

Wanandoa mnapaswa mtembee na Mungu na Maombi ndio iwe Pumzi yenu.

1:Hakikisheni Mnatoa Fungu la Kumi Kanisani au Kwa Baba Yenu wa Kiroho

2;Ombeeni milango ya Uchumi nakumshirikisha Mlezi wenu mnapotoa Fungu la kumi

3:Simameni na Maombi nakuepuka Matumizi mabaya ya Fedha.


3:WAZAZI PANDE MBILI

Nimekuwa Mwalimu na kujifunza mengi Kutokana nakutatua ndoa Nyigi nakuzijenga ndoa Nyigi Kupitia kipawa alichokiweka Mungu ndani Yangu.

Nilichojifunza Wanandoa Wengi Huwa Wanashindwa Kuelewa ndoa inajengwa na watu wawili mwanaume au Mwanamke hurusiwi ukishaolewa unaaza Kutoa maneno na kuwaeleza Nyumbani kwenu Kuwa MKE wangu anafanya hivi au Mwanamke kufanya hivi.

Wanandoa hutakiwa wajenge Familia Yao na Kujijenga Kwao Sio Kuaza Utake kwenda Kumjegea mama Yako au wazazi wako kabla hamjajega Kwenu

Wazazi nao Wapo wasiojielewa nakutambua watoto wao TU wakishawaozesha watoto hawajaweka maisha Yao vizuri Mzazi Anaenda Kukaa na watoto hapo hapo Mkamwana au mkulima wazazi mnachangia kuyumbisha ndoa za watoto wenu 

Mama unatakiwa uwe Mbali na mme wa mwanao usilete mazaoea Baba nae awe Mbali na Mkamwana wako.

Wanandoa nanyi mnatakiwa muwe makini na Pande mbili Zisiingie zikajenga mazoea Muweke mipaka ya Kutokuwa namazoea Sana.


4:NYUMBA NA WATOTO

Katika Jambo Ambalo linaumiza vichwa ndoa Nyigi nakuondoa Heshima na maelewano mazuri kwa Wanandoa Ni Suala la Ujezi yaani kutokupanga wanawake wengi huchukia maisha ya kukaa na ndoa au mmewe kwenye Nyumba ya kupanga Na Wanaume wengi hutengemea wapate familia yaani watoto wanapooa ikitokea mtazamo wao umeenda kinyume ndani Vituko huanza na kashifa mbalimbali huaza.


UNASHAURIWA

Hatua za Mafanikio msitake kwenda kwa kuinga ndoa ya Mtu Fulani Simameni kuweka Password Yenu ya ndoa ili aliye nje ainge kwenu

Muombeni Mungu mtabarikiwa watoto watafuteni Wachungaji waaombee


5:TENDO LA NDOA

Ndoa Nyigi zimevunjika kwa Kuwa na tendo la ndoa lisiloridhisha au kutoshelezana Hali hii Hufanya Wanaume wapate wanaume nje au wanawake nje kuwe Nyumba ndogo.

Nataka Nikuambie Usipomridhisha na Kumtosholeza mmeo au mkeo ukaleta utakatifu mpaka kwenye tendo la ndoa au Maombi ndoa Yako usishagae ikivunjika au huyo mwanamme kukimbia nakuenda kuazisha Mwanamke mwingine.

UNASHAURIWA ✍️✍️

Ajibika ipasavyo kwenye Tendo la ndoa na Jifunze ubunifu kila siku wakubadili Hata MIKAO ya Tendo la ndoa na hakikisha mnalizishana ulokole weka pembeni hudumia mkeo au mmeo 

6: UAMINIFU

Jitaidi Kutunza nakulinda Uaminifu maana Uaminifu ukiondoa Kuurudisha gharama sana

UNASHAURIWA

Uwe Mwaminifu kwa mwezako muwekeane Password ya Kuaminiana Kila mmoja 

7:JIAMINI UNAPENDWA

Wanandoa Wengi wana wivu hawajiamini Kama Wanapendwa na wapenzi wao 

Unapaswa ujiamini UNAPENDWA Upo peke yako.


HITIMISHO

Tukizingatia haya ndoa zetu mahusiano yetu tutayaponya nakuwa mfano kwa Wengine mpaka watakuuliza umepata wapi shule

Kwa Ushauri na Maombezi mpigie Jioni Pastor Richard

SAA:12:00 mpaka Saa 8 00 Usiku Simu+255759861768

@2020 Pastor Richard


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.