Somo:Hasira Haitendi njema

SOMO: HASIRA HAITENDI NJEMA SIKU ZOTE.

Matendo;26;11 Warumi:2:5-8 Waefeso:4:26-31 Yakobo:1:20

Nawakaribisha Wanangu Popote ulipo SoMo la Leo Jumapili ya Leo Tunataka Tujifunze madhara ya Hasira Na Hasira isivyo nashukurani haiwezi kukumbuka wema hata mazuri Hata Kidongo

Lengo: Nikuwaponya watu Wenye Hasira Wameshindwa Kuendelea Kutokana na Hasira Zao Wamepishana na Baraka Zao Kutokana na Hasira.

MAONO YA SOMO: Hasira Isiwemo ndani Yako ili kuponya Nafsi yako.

MAAANA YA HASIRA:
Hasira ni Kughadhibika Yaani Kupaniki kwa Ajiri ya Kitu Fulani.
KUPOKEA Taarifa tofauti nakuitafisiri Tofauti inamfanya mtu Akasirike na Kupaniki

MATOKEO YA HASIRA
Yapo Mambo matatu tu Yanamtesa Mwanadamu kwa Mwanadamu

1;Hasira itakupa matokeo Ya Uadui Juu ya Mwanadamu MWEZAKO.
Hi roho itakuwa na nguvu kukupa Mawazo machafu Juu ya MWEZAKO.

2:Hasira Itakupa matokeo Ya Kumtafisiri Tofauti Mwanadamu mwezako
Hii roho itakufanya kila akiongea yule mtu kwa Kuwa unahasira nae utamwelewa tofauti Akili na Ufahamu Utaleta tafsiri isiyo Sahihi.

3:Hasira Itakupa Matokeo Mabaya utawaza Kuua Utawaza Kumdhuru yule mtu unaemchukia na utatekeleza hivyo.
Hii Ni Roho itakuambia ufanye kitu kibaya kwake kutakana unahasira nae huyo mtu.

KWANINI TUNASEMA HASIRA  HAITENDI NJEMA

Ukiwa na Hasira hutawaza njema Juu ya huyo mtu unaemchukia

1:Utaua Kimawazo
2:Utazini Kimawazo
3:Utavunja Agano Kimawazo
4:Utahesabu Mabaya Kwake
5:Utamununia Bure
6;Amani Naye itakosekana
7:Utafanya Maamuzi mazito Zidi Yake
8:Utamchekea Kwa Nje Moyoni Kumbe Unahasira nae.
9:Utajenga mbifu nae Mara kwa Mara
10:Utafuta mazuri Yote kwake.

TUFANYE NINI TUPONE NA HIZI HASIRA.

Fata njia HIZI uiondoe Hasira ndani yako na Utaona raha ya kuishi bila Hasira Mambo mengi yanafunguka.

1:Jichanganye na Watu uongee nao
2:Weka Sifa au Bint Cheza TU
3:Nenda Kalale pumzika tu
4;Kaa Kimya Nyamaza
5:Mweleze Juu ya anapokuuzi
6:Tafuta Amani nae Kupitia Neno la Mungu Mafundisho mbalimbali Kama Nguvu ya MSAMAHA.

Naitwa Mchungaji Richard
Nawatakia siku njema

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.